Misaada ya Kujifunza
TJS, Ufunuo 2


TJS, Ufunuo 2:22. Linganisha na Ufunuo 2:22

Waovu wanatupwa jehanamu.

22 Tazama, naye nitamtupa katika jehanamu, nao wale watendao uzinzi pamoja naye nitamtupa katika taabu kuu, isipokuwa watubu matendo yao.

TJS, Ufunuo 2:26–27. Linganisha na Ufunuo 2:26–27

Wale wanaoushinda ulimwengu kwa kutii amri za Kristo watatawala falme katika ulimwengu ujao kwa imani, usawa, na haki.

26 Na kwa yule ambaye atashinda, na kutii amri zangu mpaka mwisho, nitampa uwezo juu ya falme nyingi;

27 Na atazitawala kwa neno la Mungu; na zitakuwa katika mikono yake kama vyombo vya udongo mikononi mwa mfinyanzi; na atawatawala kwa imani, kwa usawa, na haki, kama vile nilivyopokea kutoka kwa Baba.