Misaada ya Kujifunza
TJS, Ufunuo 1


TJS, Ufunuo 1:1–8. Linganisha na Ufunuo 1:1–8

Yohana Mtume anapokeamafunuo yaliyomo katika kitabu cha ufunuo. Anatembelewa na Yesu Kristo na malaika.

1 Ufunuo wa Yohana, mtumishi wa Mungu, uliotolewa kwake na Yesu Kristo, ili kumwonyesha mtumishi wake mambo ambayo lazima yatatokea baada ya muda mfupi, ambao aliupeleka na kuonyeshwa kwa mtumishi wake Yohana kwa njia ya malaika,

2 Yeye aliyelishuhudia neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, na mambo yote aliyoyaona.

3 Heri yao wasomao, na wao wasikiao na kuyaelewa maneno ya unabii huu, na kuyashika mambo yale yaliyoandikwa ndani yake, kwa maana wakati wa ujio wa Bwana unakaribia.

4 Sasa huu ni ushuhuda wa Yohana kwa watumishi saba wanaoyasimamia yale makanisa saba katika Asia. Neema na iwe kwenu, na amani kutoka kwake yeye aliyeko, na aliyekuwako, na atakayekuja; ambaye amemtuma malaika wake kutoka mbele ya kiti chake cha enzi, ili kuwashuhudia wale watumishi saba walio juu ya makanisa saba.

5 Kwa hiyo, Mimi, Yohana, shahidi mwaminifu, natoa taarifa ya vitu ambavyo nilipewa na malaika, na kutoka kwa Yesu Kristo mzaliwa wa kwanza wa wafu, na Mwana mfalme wa wafalme wa dunia.

6 Na kwa yeye ambaye alitupenda, utukufu uwe juu yake; aliyetuosha dhambi zetu kwa damu yake, na ametufanya wafalme na makuhani kwa Mungu, Baba yake. Utukufu na mamlaka yawe kwake milele na milele. Amen.

7 Kwani tazama, anakuja mawinguni na elfu kumi na elfu kumi ya watakatifu wake katika ufalme yake, wamevalishwa na utukufu wa Baba yake. Na kila jicho litamwona; na wale waliomchoma, na ndugu wote wa dunia wataomboleza kwa sababu yake. Naam, Amina.

8 Kwani anasema, Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, Bwana, aliyeko, na aliyekuweko, na atakayekuja, Mwenyezi.