Misaada ya Kujifunza
TJS, Ufunuo 12


TJS, Ufunuo 12:1–17. Linganisha na Ufunuo 12:1–17

Yohana anaelezea juu ya zile ishara za mwanamke, mtoto, fimbo ya chuma, joka na Mikaeli. Ile vita iliyoanza mbinguni inaendelea hapa duniani. Angalia mabadiliko ya mfuatano wa mistari katika TSJ.

1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni, katika mifano ya vitu vya duniani; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili.

2 Naye mwanamke alikuwa mjamzito, akilia, hali ana uchungu, na kuumwa akiwa katika kuzaa.

3 Naye akamzaa mtoto mwanamume, yeye atakayetawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma; na mtoto wake atanyakuliwa hata kwa Mungu na kwa kiti chake cha enzi.

4 Na ikaonekena ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka jekundu, likiwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake mataji saba. Na mkia wake ukazikokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha duniani. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo amle mtoto wake baada ya kuzaa.

5 Na yule mwanamke akakimbia nyikani, ambako palikuwepo mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wao wamlishe huko kwa muda wa miaka elfu moja na mia mbili na sitini.

6 Na kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na lile joka; na lile joka na malaika zake wakapigana na Mikaeli;

7 Na lile joka likashindwa dhidi ya Mikaeli, si mtoto, wala mwanamke ambaye alikuwa kanisa la Mungu, yeye aliyezaa kwa uchungu, na kuuleta ufalme wa Mungu wetu na Kristo wake.

8 Wala mahali hapakupatikana tena mbinguni kwa yule joka kuu, aliyetupwa nje; yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi, na pia huitwa Shetani, yule audanganyaye ulimwengu wote; alitupwa katika dunia; na malaika zake walitupwa nje pamoja naye.

9 Nami nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, Sasa umekuja wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na uwezo wa Kristo wake;

10 Kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye aliyewashitaki mbele za Mungu wetu mchana na usiku.

11 Maana wamemshinda yeye kwa damu ya Mwanakondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; kwa maana wao hawakuyapenda maisha yao wenyewe, bali walishika ule ushuhuda hata kifo. Kwa hiyo, shangilieni Enyi mbingu, na nyie mnaoishi ndani yake.

12 Na baada ya mambo haya nikasikia sauti nyingine ikisema, Ole wenu wakazi wa dunia, ndiyo, na wao wakaao juu ya visiwa vya bahari! kwa maana ibilisi ameshuka kwenu, akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kuwa ana wakati mchache tu.

13 Maana lile joka lilipoona ya kuwa limetupwa katika dunia, lilimtesa yule mwanamke aliyemzaa mtoto mwanamume.

14 Kwa hiyo, kwa mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aweze kuruka kwenda nyikani, katika mahali pake, hapo analishwa kwa wakati, na nyakati, na nusu ya wakati, mbali na uso wa nyoka huyo.

15 Naye nyoka akatoa kutoka kinywani mwake nyuma ya huyo mwanamke maji kama gharika, ili apate kumfanya kuchukuliwa na gharika hiyo.

16 Na dunia ikamsaidia mwanamke huyo, na dunia ikafunua kinywa chake, ikaimeza gharika hiyo aliyotoa na lile joka kutoka kinywani mwake.

17 Kwa sababu hiyo, lile joka likamkasirikia yule mwanamke, na likaenda zake kufanya vita na baki la wazao wake, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.