Misaada ya Kujifunza
TJS, Yohana 13


TJS, Yohana 13:8–10. Linganisha na Yohana 13:8–10

Yesu anaosha miguu ya Mitume ili kutimiza sheria ya Wayahudi.

8 Petro akamwambia, Wewe hutakiwi kuniosha miguu yangu. Yesu akamjibu, Kama sitakuosha, wewe huna shirika nami.

9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, bali pia mikono yangu na kichwa changu.

10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuosha mikono yake na kichwa chake hana haja ila kuosha miguu yake, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. Hii ilikuwa ni desturi ya Wayahudi chini ya sheria; hivyo basi, Yesu alifanya hivyo ili sheria ipate kutimizwa.