Misaada ya Kujifunza
TJS, Waebrania 7


TJS, Waebrania 7:3. Linganisha na Waebrania 7:3

Melkizedeki alikuwa kuhani kwa mfano wa Mwana wa Mungu. Wale wote wapokeao ukuhani huu wanaweza kuwa kama Mwana wa Mungu.

3 Kwa maana Melkizedeki huyo alitawazwa kuwa kuhani kwa mfano wa Mwana wa Mungu, mfano ambao ulikuwa hauna baba, hauna mama, hauna nasaba, ukiwa hauna mwanzo wa siku, wala mwisho wa uhai. Na wale wote wanaotawazwa katika ukuhani huu hufanywa kama vile kwa Mwana wa Mungu, nao hukaa kama makuhani daima.

TJS, Waebrania 7:19–21. Linganisha na Waebrania 7:19–21

Sheria ili watayaarisha watu kwa ajili ya Yesu, ambaye ni “mdhamini wa agano bora zaidi.”

19 Kwani sharia ilitolewa bila kiapo na haikukamilisha chochote, bali ilikuwa tu mwanzo katika matumaini mema; na kwa hiyo tunamkaribia Mungu;

20 Kwa sababu kuhani huyu mkuu alikuwa na kiapo, na kwa kadiri hii Yesu alifanywa mdhamini wa agano bora zaidi.

21 (Kwani makuhani hao walifanywa bila kiapo; lakini yeye pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa na hata tubu, Wewe ni kuhani milele kwa mfano wa Melikizedeki;)

TJS, Waebrania 7:25–26. Linganisha na Waebrania 7:26–27

Yesu anajitolea Yeye mwenyewe kuwa dhabihu isiyo na dhambi kwa ajili ya dhambi zetu.

25 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiye na waa lolote, aliyejitenga na watenda dhambi na alifanywa kuwa mtawala juu ya mbingu;

26 Na siyo kama wale makuhani wakuu ambao walitoa dhabihu kila siku, kwanza kwa ajili ya dhambi zao wenyewe, na kisha kwa ajili ya dhambi za watu; maana yeye hahitaji kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kwa maana yeye hakuijua dhambi yoyote; bali kwa ajili ya dhambi za watu. Na hii alifanya mara moja, alipojitoa nafsi yake.