Maandiko Matakatifu
Alma 39


Amri za Alma kwa mwana wake Koriantoni.

Yenye milango ya 39 hadi 42.

Mlango wa 39

Dhambi ya ngono ni machukizo—Dhambi za Koriantoni ziliwazuia Wazoramu kupokea neno—Ukombozi wa Kristo utaponya waumini ambao waliutangulia. Karibia mwaka 74 K.K.

1 Na sasa, mwana wangu, nina vitu vingi zaidi kukuzungumzia kuliko yale niliyomzungumzia kaka yako; kwani tazama, hujachunguza unyofu wa kaka yako, uaminifu wake, na bidii yake kwa kutii amri za Mungu? Tazama, si yeye amekuonesha mfano mzuri?

2 Kwani hukutii maneno yangu kama vile kaka yako alivyofanya, miongoni mwa watu wa aWazoramu. Sasa hii ndiyo ninayo dhidi yako; uliendelea kujivuna kwa sababu ya nguvu yako na hekima yako.

3 Na hii siyo yote, mwana wangu. Ulifanya yale ambayo yalikuwa ya kusikitisha kwangu; kwani uliacha huduma, na ukaenda kwenye nchi ya Sironi ndani ya mipaka na nchi ya Walamani, kumtafuta akahaba Isabeli.

4 Ndiyo, aaliiba mioyo ya wengi; lakini hii sio kisingizio kwako, mwana wangu. Ungeendelea kuhudumu pale ambapo uliaminiwa.

5 Hujui, mwana wangu, kwamba avitu hivi ni machukizo machoni mwa Bwana; ndiyo, ni machukizo kuliko dhambi zote isipokuwa ile ya kumwaga damu ya wale wasio na hatia au kumkana Roho Mtakatifu?

6 Kwani tazama, ikiwa autamkana Roho Mtakatifu wakati amekuwa ndani yako, na unajua kwamba unamkataa, tazama, hii ni dhambi ambayo bhaiwezi kusamehewa; ndiyo, na yeyote auaye dhidi ya mwangaza na taarifa ya Mungu, si rahisi kwake kupata cmsamaha; ndiyo, nasema kwako, mwana wangu, kwamba si rahisi kwake kupata msamaha.

7 Na sasa, mwana wangu, ningemsihi Mungu kwamba hungekuwa na ahatia ya kosa kubwa hivyo. Singetaka kuendelea kukuzungumzia makosa yako, na kuumiza roho yako, kama haingekuwa kwa faida yako.

8 Lakini tazama, huwezi kuficha makosa yako kwa Mungu; na isipokuwa utubu zitakuwa ushahidi dhidi yako katika siku ya mwisho.

9 Sasa mwana wangu, ningetaka kwamba utubu na kusahau dhambi zako, na usiende tena kupendeza atamaa ya macho yako, lakini bujikataze mwenyewe kwa vitu hivi vyote; kwani usipofanya hivi huwezi kwa vyovyote kurithi ufalme wa Mungu. Ee, kumbuka, na ujichukulie juu yako, na ujikatishe mwenyewe katika vitu hivi.

10 Na nina kuamuru ujichukulie kushauriana na kaka zako wakubwa katika shughuli zako; kwani tazama, wewe ungali ndani ya ujana wako, na unahitaji kulishwa na kaka zako. Na kusikiliza ushauri wao.

11 Usiamini kudanganywa na kitu kilicho bure na cha kipumbavu; usikubali ibilisi apoteze moyo wako kufuata hao makahaba waovu. Tazama, Ee mwana wangu, ni jinsi gani uovu mkuu uliwaletea aWazoramu; kwani wakati walipoona bmwenendo wako hawakuamini maneno yangu.

12 Na sasa Roho wa Bwana huniambia mimi: aAmuru watoto wako watende mema, la sivyo wataongoza mioyo ya wengi kwenye maangamizo; kwa hivyo nakuamuru, wewe mwana wangu, kwa heshima ya Mungu, kwamba ujiepushe kutoka uovu wako;

13 Kwamba umtazamie Bwana na akili, nguvu, na uwezo wako wote; kwamba usipoteze mioyo ya watu mara nyingine kwa uovu; lakini urudi kwao, na akukiri makosa yako na ule ubaya ambao umetenda.

14 aUsitafute utajiri wala vitu visivyo vya maana vya ulimwengu huu; kwani tazama, hutavibeba wakati wa kifo.

15 Na sasa, mwana wangu, ningesema machache kwako kuhusu kuja kwa Kristo. Tazama, nakwambia, kwamba ni yeye kwa kweli atakayekuja kuondoa dhambi za ulimwengu; ndiyo, anakuja kutangaza habari njema ya wokovu kwa watu wake.

16 Na sasa, mwana wangu, hii ndiyo huduma ambayo uliitiwa, kutangaza hizi habari njema kwa watu hawa, kutayarisha akili zao; kwa usahihi zaidi afadhali kwamba wokovu uwajie, kwamba watayarishe akili za awatoto wao kusikiliza neno wakati wa kuja kwake.

17 Na sasa nitatuliza kidogo akili yako kwa jambo hili. Tazama, unashangaa kwa nini hivi vitu vijulikane mbele. Tazama, nakwambia, si roho wakati huu ina thamani kwa Mungu vile roho itakuwa wakati wa kuja kwake?

18 Si ni lazima mpango wa ukombozi ufunuliwe kwa watu hawa na kwa watoto wao pia?

19 Je, si ni rahisi wakati huu kwa Bwana kutuma malaika wake kututangazia habari hii njema kama vile kwa watoto wetu, au kama vile baada ya kuja kwake?