Maandiko Matakatifu
3 Nefi 22


Mlango wa 22

Katika siku za mwisho, Sayuni na vigingi vyake vitaimarishwa, na Israeli itakusanywa kwa huruma na wororo—Watafaulu—Linganisha Isaya 54. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Na ndipo ile ambayo imeandikwa itatimizwa: Imba, ewe tasa; wewe usiyepata kujifungua mtoto; anza akuimba na ulie kwa sauti, wewe ambaye hukujifungua mtoto; kwani wengi ni watoto wa tasa, kuliko watoto wa mke aliyeolewa, asema Bwana.

2 Panua mahali pa hema lako, na acha watandaze mapazia ya maskani yako; tumia nafasi yote, ongeza urefu wa kamba zako, na vikaze avigingi vyako;

3 Kwani utaenea kwenye upande wa kulia na kwenye upande wa kushoto na uzao wako utawamiliki aWayunani na kufanya miji ya ukiwa kumilikiwa.

4 Usiogope, kwani hutaaibika; wala kuteketezwa, kwani hutawekwa aaibu; kwani utasahau aibu ya ujana wako, na hutakumbuka aibu ya ujana wako, na hutaweza kukumbuka mashtumu ya ujane wako tena.

5 Kwani muumba wako, mume wako, Bwana wa Majeshi ndilo jina lake; na Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli—ataitwa Mungu wa dunia yote.

6 Kwani Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, na mke wa ujana, wakati ulikataliwa, asema Mungu wako.

7 Kwa muda mfupi nimekuacha, lakini kwa rehema nyingi nitakurejesha.

8 Kwa ghadhabu ndogo, nilificha uso wangu kutoka kwako kwa muda mfupi, lakini kwa wema usio na mwisho nitakuwa na ahuruma kwako, asema Bwana Mkombozi wako.

9 Kwani jambo ahili limekuwa kama bmaji ya Nuhu kwangu, kwani vile nilivyoapa kwamba maji ya Nuhu hayatafunika dunia tena, kadhalika nimeapa kwamba sitakuwa na hasira nawe.

10 Kwani amilima itaondoka, na vilima vitaondelewa, lakini wema wangu bhautaondoka kutoka kwako, wala agano langu la amani liondolewe, asema Bwana ambaye ana rehema nawe.

11 Ee uliyeteseka, uliyerushwa na tufani, bila kutulizwa! Tazama, nitaweka amawe yako na rangi nzuri, na kuweka msingi wako na johari ya thamani.

12 Na nitafanya madirisha yako ya akiki, na milango yako ya kito nyekundu, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.

13 Na watoto wako awote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa kubwa.

14 Utathibitika katika ahaki; utakuwa mbali na kuonewa, kwani hutaogopa, na mbali na hofu, kwani haitakuja karibu nawe.

15 Tazama, yamkini watakusanyika pamoja dhidi yako, sio kwa shauri langu; wote watakaokusanyika pamoja dhidi yako wataanguka kwa ajili yako.

16 Tazama, nimemuumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, na ambaye huleta chombo kwa kazi yake; na nimemuumba mharibifu kuangamiza.

17 Hakuna silaha yoyote itakayotengenezwa dhidi yako ambayo itafaulu; na kila ulimi ambao utatukana dhidi yako, utahukumu. Huu ndiyo urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inatoka kwangu, asema Bwana.