Maswali na Majibu
“Je, ninawezaje kupata ushuhuda imara juu ya Joseph Smith na Urejesho?”
“Kitu ambacho nimefanya ili kuimarisha ushuhuda wangu juu ya Urejesho ni kusoma tukio la ono la kwanza kila usiku kabla ya kulala. Ninaposoma kuhusu Joseph kukombolewa na kusimama katika uwepo wa Mungu, ninahisi kuwa karibu na nuru ya Mungu, na hiyo inanisaidia kujua kuwa Yeye yupo.”
Eve T., 16, Chorley, Uingereza
“Nilipogundua kwamba sikuwa na ushuhuda juu ya Joseph Smith, nilianza kusoma Watakatifu. Niligundua jinsi uzoefu wa Joseph ulivyokuwa wenye nguvu na wa kimiujiza. Pia nilimhisi Roho pamoja nami wakati niliposali kuhusu Kitabu cha Mormoni. Nilianza kuwasaidia wamisionari, na sasa siwezi kuacha kuwashuhudia watu kuhusu Joseph Smith na Urejesho.”
Abishi N., 18, Negros Oriental, Ufilipino
“Nabii alituambia tujifunze maisha ya Kristo ili kutusaidia kupata ushuhuda juu Yake na Upatanisho Wake. Vivyo hivyo kuhusu Joseph Smith. Ninapojifunza maisha yake, ninaweza kupata ushuhuda imara juu ya Urejesho na juu ya Joseph kama nabii wa kwanza wa kipindi chetu. Ninaweza pia kuelewa vyema kwa nini Kanisa la Yesu Kristo lilipaswa kurejeshwa.”
Asher W., 17, Louisiana, Marekani
“Fanya kitu ambacho Joseph alifanya na mwombe Mungu! Kuwa mvumilivu; jibu litakuja.”
Anna W., 17, Colorado, Marekani
“Sala ni njia rahisi sana ya kupata ushuhuda juu ya Joseph Smith na Urejesho. Bwana amejibu sala hii kwa ajili yangu mwenyewe na kwa wengine wengi—atafanya vivyo hivyo kwako. Pia, jifunze shuhuda zenye nguvu za mashahidi katika Kitabu cha Mormoni.”
Andrew N., 18, Washington, Marekani