Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2025
Mtegemee Yeye
Angalia video ya dhima ya vijana kwa mwaka huu na uone jinsi unavyoweza kumtegemea Kristo.
Wakati mwingine maisha yanaweza kuonekana kukuzidia. Au ya kuogopesha. Au magumu.
Katika nyakati hizi (na kila wakati mwingine) tunaweza kumgeukia Yesu Kristo.
Anatualika tumtegemee Yeye, tusiwe na shaka, na tusiogope.
Tazama video ya dhima ya vijana kwa mwaka huu na fikiria kuhusu kile unachoweza kufanya ili kumtegemea Yeye.
Kristo anataka kukusaidia wewe! Ataongoza njia yako, atakupa amani akilini mwako, na kukujaza na shangwe!