Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2025
Mtegemee Kristo
Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2025
Kunywa na Kamwe Usipate Kiu, na Yongsung Kim
Kuna nuru katika giza.
Na yote yanapoonekana magumu kuvumilia,
Usiogope.
Kuna amani katika mateso.
Tunapobaki upande wa Mwokozi.
Yeye ni nuru.
[Kiitikio]
Mtegemee—
Mtegemee Kristo
Ataiponya nafsi yako na kukurudishia uhai
Mtegemee—
Mwonyeshe Imani yako,
Mpe Yeye mashaka yako yote,
Nawe utaona nguvu Zake.
Mtegemee Kristo
Mtegemee Kristo
Yeye ni tumaini katika mapambano.
Wakati yote yanapoonekana zaidi kuliko unavyoweza kuvumilia,
Atachukua maumivu yako.
Atakupa ujasiri
Wakati unapoogopa na wanapokutupa gizani.
Yeye ni nuru.
[Kiitikio]
[Daraja:]
Inua macho yako kwa Mwana.
Sikia sauti Yake na uhisi upendo Wake.
Atakuonyesha wewe ni nani.
Sema sala, tuliza woga wako.
Atainua nafsi yako kama unaamini.
Fungua moyo wako.
[Kiitikio]