Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 24


TJS, Luka 24:2–4. Linganisha Luka 24:2–5

Wanawake wanawaona malaika wawili kwenye kaburi la Yesu.

2 Na walikuta jiwe limeviringishwa mbali kutoka kaburini, na malaika wawili wamesimama karibu nalo wakiwa katika mavazi yanayongʼaa.

3 Na wakaingia kaburini, na hawakuuona mwili wa Bwana Yesu, walikanganyikiwa sana na tukio kama hilo;

4 Na waliogopa, na wakainamisha nyuso zao chini ardhini. Bali tazama malaika wakawaambia, Kwa nini mnawatafuta walio hai miongoni mwa wafu?