Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 14


TJS, Luka 14:35–37. Linganisha na Luka 14:34

Wale wanaomjua Musa na manabii wanamwamini Yesu.

35 Kisha baadhi yao walikuja kwake, wakisema, Bwana Mwema, tuna Musa na manabii, na yeyote yule anayeishi kulingana na maandiko yao, hatakuwa na Maisha?

36 Na Yesu akajibu, akasema, Hamumjui Musa, wala manabii; kwani kama mngewajua, mngeniamini; kwani kwa dhamira hii yaliandikwa. Kwani nimetumwa ili muweze kuwa na maisha, Kwa hiyo nitafananisha na chumvi iliyo mzuri;

37 Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itaungwa vipi?