Misaada ya Kujifunza
TJS, Mwanzo 21


TJS, Mwanzo 21:31–32. Linganisha na Mwanzo 21:32–34

Ibrahimu humwabudu Mungu wa milele.

31 Kisha Abimeleki, na Fikoli, mkuu wa majeshi yake, walisimama, na walipanda kijisitu cha kuabudia sanamu katika Beer-sheba, na pale walimwomba Bwana; na walirudi katika nchi ya Wafilisti.

32 Na Ibrahimu alimwabudu Mungu wa milele, na alikaa katika nchi ya Wafilisti kwa siku nyingi.