Misaada ya Kujifunza
TJS, Mwanzo 17


TJS, Mwanzo 17:3–12. Linganisha na Mwanzo 17:3–12

Watu washindwa kutii ibada za injili, ikijumuisha ubatizo. Mungu amwelezea Ibrahimu juu ya agano la tohara na umri wa uwajibikaji wa watoto.

3 Na ikawa, kwamba Abramu akaanguka kifudufudi, na kulilingana jina la Bwana.

4 Na Mungu alizungumza naye, akisema, Watu wangu wamepotoka nje ya maagizo yangu, na hawakuzishika ibada zangu ambazo niliwapa baba zao;

5 Na wao hawakutii mpako wangu wa mafuta, na uzamisho, au ubatizo ambao niliwaamuru;

6 Bali wamezigeuza amri, na wamejitwalia wenyewe kuoshwa kwa watoto, na damu ya kunyunyiza;

7 Na wamesema kwamba damu ya Habili mwenye haki ilimwagwa kwa ajili ya dhambi; na hawakujua katika hili wao wanawajibika mbele zangu.

8 Lakini kwako wewe, tazama, nitafanya agano langu na wewe, na utakuwa baba wa watu wengi.

9 Na agano hili ninalolifanya, kwamba watoto wako watajulikana miongoni mwa mataifa yote. Wala jina lako kamwe halitaitwa Abramu, bali jina lako litaitwa Abrahamu; kwani, nimekufanya wewe kuwa baba wa watu wengi.

10 Na nitakufanya wewe uwe na uzao mwingi, na nitafanya mataifa mengi kutoka kwako, na wafalme watatoka kwako na wa uzao wako.

11 Nami nitafanya nawe agano la tohara; nalo litakuwa agano langu kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao; ili upate kujua milele kwamba watoto hawawajibiki mbele zangu hadi wamefikia umri wa miaka minane.

12 Nawe utatii kuyashika maagano yangu yote ambayo nimeagana na baba zako; nawe utazishika amri ambazo nimekupa wewe kwa kunywa changu mwenywe, nami nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.

TJS, Mwanzo 17:23–24. Linganisha na Mwanzo 17:17–18

Ibrahimu alifurahia unabii juu ya kuzaliwa kwa Isaka kulipotabiriwa na anamwombea Ismaili.

23 Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi na kufurahi, na akasema moyoni mwake, Mtu wa umri wa miaka mia kwake atazaliwa mtoto, naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa.

24 Na Ibrahimu akamwambia Mungu, lau Ishmael angeishi kwa uadilifu mbele zako!