Misaada ya Kujifunza
TJS, Mwanzo 14


JST, Mwanzo 14:25–40. Linganisha na Mwanzo 14:18–20

Melkizedeki anambariki Abram. Huduma kuu ya Melkizedeki na nguvu na baraka za Ukuhani wa Melkizedeki zaelezwa.

25 Na Melkizedeki akapaza sauti yake na kumbariki Abramu.

26 Sasa Melkizedeki alikuwa mtu wa imani, aliyetenda haki; na alipokuwa mtoto alimwogopa Mungu, na alifunga vinywa vya samba, na alizima nguvu za moto.

27 Na hivyo, baada ya kuwa amethibitishwa na Mungu, alitawazwa kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa agano ambalo Mungu alilifanya na Henoko.

28 Ulikuwa kwa mfano wa Mwana wa Mungu; mfano ambao ulikuja, siyo na mwanadamu, wala sio kwa mapenzi ya mwanadamu; wala siyo ya baba wala mama; hauna mwanzo wa siku wala mwisho wa miaka; bali kwa njia ya Mungu;

29 Nao ulitolewa kwa wanadamu kwa wito wa sauti yake mwenyewe, kulingana na mapenzi yake mwenyewe, kwa wengi kadiri walivyoamini katika jina lake.

30 Maana Mungu akiwa ameapa kwa Henoko na kwa uzao wake kwa kiapo cha nafsi yake; kwa kila mmoja atakaye kuwa ametawazwa kwa mfano na wito huu awe na uwezo, kwa imani, kuivunja milima, kuzigawanya bahari, kuyakausha maji, kuzibadilisha njia zake;

31 Kuyazuia kwa mafanikio majeshi ya mataifa, kuigawa dunia, kuvunja kila kamba, kusimama katika uwepo wa Mungu; kufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake, kulingana na amri yake, kuzitiisha himaya na wenye nguvu; na hii ni kwa mapenzi ya Mwana wa Mungu ambaye alikuwepo kabla ya kuweko kwa msingi wa ulimwengu.

32 Na wanadamu wakiwa na imani hii, wakafikia mfano huu wa Mungu, walihamishwa na kutwaliwa mbinguni.

33 Na sasa, Melkizedeki alikuwa kuhani wa mfano huu; kwa sababu hiyo akapata amani katika Salemu, naye aliitwa Mfalme wa amani.

34 Na watu wake walitenda haki, na wakaipata mbingu, na wakautafuta mji wa Henoko ambao Mungu aliutwa, akiutenganisha na dunia, akiwa ameuhifadhi hadi siku za mwisho, au mwisho wa ulimwengu;

35 Naye alisema, na kuapa kwa kiapo, kwamba mbingu na dunia zitakunjamana pamoja; na wana wa Mungu watajaribiwa kama vile kwa moto.

36 Na huyu Melkizedeki, hivyo akiwa ameistawisha haki, alikuwa akiitwa mfalme wa mbinguni na watu wake, au kwa maneno mengine, Mfalme wa amani.

37 Naye alipaza sauti yake, na akambariki Abramu, akiwa kuhani mkuu, na mtunzaji wa ghala ya Mungu;

38 Yeye ambaye Mungu alimteuwa kupokea zaka kwa ajili ya maskini.

39 Kwa sababu hiyo, Abramu alilipa kwake yeye zaka ya vile vyote alivyokuwa navyo, ya utajiri wote aliomiliki, ambao Mungu alimpa zaidi ya kile ambacho yeye alikihitaji.

40 Na ikawa, kwamba Mungu akambariki Abramu, na akampa utajiri, na heshima, na nchi kwa ajili ya milki isiyo na mwisho; kulingana na agano ambalo yeye alilifanya, na kulingana na baraka ambazo Melkizedeki alimbariki nazo.