Misaada ya Kujifunza
TJS, 1 Timotheo 3


TJS, 1 Timotheo 3:15–16. Linganisha na 1 Timotheo 3:15–16

Kanisa limeanzishwa juu ya kanuni kuu kwamba Yesu alikuwa mwili wa kufa, alifundisha injili, na alirudi kwa Baba yake. Angalizo: ugumu wa kueleza mabadiliko katika mistari ifuatayo inasisitiza kwamba “nguzo na msingi la ukweli” ni Yesu Kristo.

15 Lakini kama nikingojea kwa muda mrefu ili muweze kujua jinsi mnavyotakiwa kujiheshimu katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai.

16 Nguzo na msingi wa ukweli ni, (na bila mabishano, makubwa mno maajabu ya Uungu,) Mungu alidhihirika katika mwili, na kujithibitisha katika Roho, alionekana na malaika, alihubiri kwa wayunani, aliaminiwa ulimwenguni, alipokelewa kwenye utukufu.