Maandiko
Ushuhuda wa Mashahidi Wanane


Ushuhuda wa Mashahidi Wanane

Ijulikane kwa mataifa yote, makabila, lugha, na watu, ambao kwao kazi hii itawajia: Kwamba Joseph Smith, Mdogo, mfasiri wa kazi hii, ametuonyesha mabamba ambayo tayari yameelezwa, ambayo yana muonekeno wa dhahabu; na tumegusa kwa mikono yetu kurasa ambazo yeye Smith ametafsiri; na pia kuona michoro juu yake, vyote vikiwa na muonekeno wa kazi ya kale, na ya ustadi wa hali ya juu. Na kwa hili tunatoa ushuhuda kwa maneno ya kiasi, kwamba Smith aliyetajwa ametuonyesha, kwani sisi tumeyaona na kuyainua, na kujua kwa uhakika kwamba Smith aliyetajwa anayo mabamba ambayo tayari tumeyaeleza. Na tunaupatia ulimwengu majina yetu, ili kushuhudia kwa ulimwengu yale ambayo tumeyaona. Na hatudanganyi, Mungu akishuhudia hili.

Christian Whitmer

Jacob Whitmer

Peter Whitmer, Mdogo

John Whitmer

Hiram Page

Joseph Smith, Mkubwa

Hyrum Smith

Samuel H. Smith