Kujifunza Kutumia Teknolojia kwa Usalama
Kila wakati ninapotumia teknolojia, ninafanya uchaguzi.
Penda. Fuata. Jisajili. Ondoa.
Kila wakati ninapotumia teknolojia, ninafanya uchaguzi. Ninaweza kuitumia ili kunisaidia kukua, kujifunza ujuzi mpya, na kuunganika na watu wengine – au ninaweza kujenga tabia zisizo na afya.
Ndiyo sababu ninashiriki kile kinachonisaidia kusimamia teknolojia: Dhumuni, Panga, na Tulia. Kukumbuka maneno haya matatu kunanisaidia kuwa na michangamano salama na yenye usaidizi. Ninavishiriki vitu hivi kwa sababu nadhani vinaweza kukusaidia pia.
Kumbuka:
-
Teknolojia ina lengo.
-
Nina mpango wa kutumia teknolojia.
-
Ninaweza kutulia na kujipa muda kidogo.