Vijana
Panga


Panga

Hand holding a smartphone

Ninapopanga mapema, ninajisikia vizuri zaidi na kufanya chaguzi bora.

Ninapenda kupiga gitaa, na mimi ni mzuri sana kwenye hilo. Wakati wowote ninapokuwa na tamasha siku za usoni, najua kwamba lazima nifanye mazoezi na kujipanga mapema. Na ni vivyo hivyo kwa teknolojia: ninapojipanga mapema, ninajisikia vizuri na kufanya chaguzi bora.

Nilikuja na baadhi ya sheria rahisi ambazo hunisaidia kubakia kwenye mpango wangu:

  • Ninajiwekea ukomo kila siku wa muda wa skrini.

  • Nina “wafuata” na kuwasiliana na wanafamilia na marafiki wa karibu tu.

  • Nina maeneo nyumbani ambapo vifaa vya kielektroniki havitumiki, kama vile chumba changu cha kulala na bafuni kwangu.

  • Nilitenga mahali pa kuchajia kwa ajili ya familia, kwa hivyo vifaa vya kila mtu vinachajiwa na havitumiwi wakati wa usiku.

  • Ninatumia vichujio kuzuia programu tumizi na maudhui yasiyofaa au yasiyo salama.

Hakuna uamuzi ulio wa wazi wa kilicho sahihi au kisicho sahihi kwa kila uchaguzi ninaoweza kuufanya kwa teknolojia. Lakini kupanga mapema kunasaidia. Na ninaweza kuzungumza na rafiki zangu na familia yangu kuhusu mawazo yao pia.

Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi

Icons