Dhumuni
Ninaweza kutumia teknolojia kwa dhumuni. Teknolojia hainitawali mimi.
Teknolojia inaniunganisha na baadhi ya watu wa kushangaza (na karibu video milioni mbili za paka). Lakini wakati mwingine mimi huzama katika kutazama tena na tena au kujibu watu. Wakati wowote hili linapotokea, inanisaidia kukumbuka kwamba mimi ninaitawala teknolojia. Teknolojia hainitawali mimi. Ninaweza kuitumia kwa kile ninachohitaji na kisha kuendelea na kitu kingine.
Hapa kuna baadhi ya maswali ambayo yalinisaidia:
-
Kwa nini ninatumia kifaa hiki hivi sasa?
-
Je, ninajisikia vizuri kuhusu kile ninachokifanya?
-
Nitatumia muda kiasi gani kwenye kifaa hiki?
Wakati mwingine ni vigumu kwangu kuelezea jinsi ninavyojisikia. Video hii ilinisaidia kuiweka katika maneno. Labda inaweza kukusaidia pia.
3:18