Agano la Kale 2022
Februari 28–Machi 6 Mwanzo 28–33: “Hakika Bwana Yuko Mahali Hapa”


“Februari 28–Machi 6. Mwanzo 28–33: ‘Hakika Bwana Yuko Mahali Hapa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 28–Machi 6. Mwanzo 28-33,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Hekalu la Tijuana Mexico

Februari 28–Machi 6

Mwanzo 28-33

“Hakika Bwana Yuko Mahali Hapa”

Unaposoma Mwanzo 28–33, tafakari kile unachojifunza kutokana na mifano ya Yakobo na familia yake. Andika misukumo yoyote unayoipokea.

Andika Misukumo Yako

Milango ya 28 na 32 ya kitabu cha Mwanzo inaeleza juu ya matukio ya kiroho ambayo nabii Yakobo aliyapata. Yote yalitokea nyikani lakini katika hali zilizokuwa tofauti sana. Katika tukio la kwanza, Yakobo alikuwa akisafiri kwenda nchi ya nyumbani kwa mama yake kutafuta mke na, akiwa njiani, alitumia usiku mzima juu ya mto wa mawe. Hakutegemea kumpata Bwana katika mahali kama pale pa ukiwa, lakini Mungu akajionyesha mwenyewe kwa Yakobo katika ndoto iliyobadilisha maisha, na Yakobo akatamka, “Hakika Bwana yuko mahali hapa; na sikujua hili” (Mwanzo 28:16). Miaka kadhaa baadae, Yakobo alijikuta yuko pekee yake nyikani tena. Wakati huu, akiwa njiani akirudi Kaanani, akikabiliwa na uwezekano wa kukutana vibaya na Esau kaka yake mwenye hasira. Lakini Yakobo alijua ya kuwa wakati alipokuwa akihitaji baraka, aliweza kumtafuta Bwana, hata akiwa nyikani (ona Mwanzo 32).

Unaweza ukajikuta uko pekee yako nyikani mwako ukitafuta baraka kutoka kwa Mungu. Yawezekana nyika yako ni uhusiano mgumu wa kifamilia, kama ule Yakobo aliokuwa nao. Yawezekana unajisikia uko mbali na Mungu au ukajisikia unahitaji baraka. Wakati mwingine baraka inakuja pasipo kutarajia; nyakati zingine inatanguliwa na mweleka. Bila kujali shida yako, unaweza kugundua kwamba hata katika nyika yako, “Bwana yuko katika mahali hapa.”

Picha
Learn More image
Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mwanzo 28; 29:1–18

Nimeahidiwa baraka za Ibrahimu hekaluni.

Akiwa njiani kwenda Harani kutafuta mke, Yakobo aliota ndoto ya ngazi iliyotoka ardhini hadi mbinguni, na Mungu amesimama juu yake. Katika ndoto, Mungu alifanya upya na Yakobo agano lile lile alilokuwa amefanya na Ibrahimu na Isaka (ona Mwanzo 28:10–17; ona pia Mwanzo 12:2–3; 26:1–4). Rais Marion G. Romney alishiriki wazo hili kuhusu kile ambacho ngazi inawezekana kuwakilisha: “Yakobo alitambua kwamba maagano aliyofanya na Bwana yalikuwa vipandio vya ngazi ambavyo yeye mwenyewe angepaswa kuvipanda ili kupata baraka alizoahidiwa—baraka ambazo zingempa haki ya kuingia mbinguni na kushirikiana na Bwana. … Mahekalu kwetu sisi sote ni sawa na kile Betheli ilivyokuwa kwa Yakobo” (“Temples—The Gates to Heaven,” Ensign, Machi 1971, 16).

Je, ni maneno na vifungu gani vingine katika Mwanzo 28:10–22 vinapendekeza uhusiano baina ya tukio la Yakobo na baraka za hekaluni? Unaposoma mistari hii, fikiria kuhusu maagano uliyofanya; je, ni mawazo gani yanakujia?

Unaposoma Mwanzo 29:1–18, tafakari jinsi ndoa ya Yakobo kwa Raheli ilivyokuwa muhimu kwa agano Mungu alilofanya upya na Yakobo pale Betheli (“nyumba ya Mungu”; ona Mwanzo 28:10–19). Shika hili akilini unapoendelea kusoma kuhusu maisha ya Yakobo katika Mwanzo 29–33. Je, ni kwa jinsi gani nyumba ya Bwana imekuleta karibu zaidi na Mungu?

Ona pia Yoon Hwan Choi, “Usiangalie Pembeni, Angalia Juu!Liahona, Mei 2017, 90-92.

Mwanzo 29:31–35; 30:1–24

Bwana ananikumbuka katika majaribu yangu.

Ingawa Raheli na Lea waliishi katika wakati na utamaduni tofauti na wetu, tunaweza sote kuelewa baadhi ya hisia walizokuwa nazo. Unaposoma Mwanzo 29:31–35 na 30:1–24, tafuta maneno na vifungu vya maneno vinavyoelezea rehema za Mungu kwa Raheli na Lea. Tafakari jinsi Bwana “alivyoangalia juu ya mateso [yako]” na “akakukumbuka” (Mwanzo 29:32; 30:22).

Pia ni muhimu kukumbuka kwamba ingawa Mungu anatusikia, katika hekima Yake Yeye hatupi daima kile kile tukiombacho. Zingatia kujifunza ujumbe wa Mzee Brook P. Hales “Majibu ya Maombi” (Liahona, Mei 2019, 11–14) ili kujifunza kuhusu njia mbali mbali Baba wa Mbinguni anatujibu maombi yetu.

Mengi kuhusu historia ya kiutamaduni ya hadithi hii, ona Kitabu cha Kiada cha Mwanafunzi cha Agano la Kale: Mwanzo–2 Samueli (2003), 86–88.

Picha
Yakobo na Esau wamekumbatiana

Kielelezo cha Yakobo na Esau wamekumbatiana, na Robert T. Barrett

Mwanzo 32–33

Mwokozi anaweza kutusaidia kushinda kutoelewana katika familia zetu.

Yakobo aliporudi Kanaani, alikuwa “anaogapa sana na kufadhaika sana” kuhusu jinsi ambavyo Esau angempokea (Mwanzo 32:7). Unaposoma katika Mwanzo 32–33 kuhusu Yakobo kukutana na Esau na hisia zake kuelekea kwenye hili, ungeweza kutafakari uhusiano wa familia yako mwenyewe—pengine ule unaohitaji uponyaji. Pengine hadithi hii inaweza kukuvutia kumfikia mtu fulani? Maswali kama haya yanaweza kukuongoza katika usomaji wako:

  • Je, ni kwa jinsi gani Yakobo alijiandaa kukutana na Esau?

  • Je ni kitu gani kinajitokeza kwako wewe kuhusu maombi ya Yakobo yanayopatikana katika Mwanzo 32:9–12?

  • Je, unajifunza nini kuhusu msamaha kutokana na mfano wa Esau?

  • Je, ni kwa jinsi gani Mwokozi anaweza kutusaidia kuponya uhusiano wa kifamilia?

Ona pia Luka 15:11–32; Jeffrey R. Holland, “Huduma ya Upatanisho,” Liahona, Nov. 2018, 77–79.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mwanzo 28–33.Tumia “Yakobo na Familia Yake” (katika Hadithi za Agano la Kale) ili kuwasaidia watoto kuelewa matukio kutoka katika milango hii. Labda washiriki wa familia wangeweza kupumzika kidogo kwenye kila picha na kutambulisha kile kinachofundishwa, kama vile umuhimu wa ndoa, maagano, kazi, na msamaha.

Mwanzo 28:10–22.Ungeweza kutumia ngazi (au picha yake) ili kuongelea kuhusu maagano yetu ni kama ngazi. Je, ni maagano gani tumefanya, na jinsi gani hayo yanatuleta karibu zaidi na Mungu? Washiriki wa familia wanaweza kufurahia kuchora ndoto ya Yakobo, iliyoelezewa katika Mwanzo 28:10–22.

Wimbo “Nearer, My God, to Thee” (Nyimbo za Kanisa, na. 100) ulishawishiwa na ndoto ya Yakobo. Familia yako ingeweza kuimba wimbo huu na kujadili kila mstari unafundisha nini.

Mwanzo 32:24-32.Unaweza kuwa na wanafamilia wanaopenda mieleka. Kwa nini “mieleka” ni njia nzuri kuelezea kutafuta baraka kutoka kwa Bwana? Je, Enoshi 1:1–5; Alma 8:9–10 wanapendekeza nini kuhusu kile kinachomaanisha kupiga “mieleka … mbele ya Mungu”?

Mwanzo 33:1–12.Baada ya miaka mingi ya hisia ngumu, Yakobo na Esau waliungana tena. Kama Yakobo na Esau wangeweza kuongea na sisi leo, je, wangeweza kusema nini kwetu ili kutusaidia sisi wakati kunapokuwa na ugomvi katika familia zetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Dearest Children, God Is Near You,” Nyimbo za Kanisa, na. 96.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Mtafute Yesu Kristo. Agano la Kale linashuhudia juu ya Yesu Kristo kupitia hadithi zake na ishara. Fikiria kuandika au kuwekea alama mistari inayofundisha kuhusu Mwokozi na hususan ile iliyo na maana kwako.

Picha
Yakobo akiota ndoto ya kuwaona malaika juu ya ngazi

Ndoto ya Yakobo pale Betheli, na J. Ken Spencer