2010–2019
Huduma ya Upatanisho
Oktoba 2018


Huduma ya Upatanisho

Ninashuhudia juu ya amani ya nafsi ambayo upatanisho na Mungu na kila mmoja utaleta kama tu wanyenyekevu na wenye ujasiri kuuafuta.

Aprili iliyopita, Rais Russell M. Nelson alipotambulisha wazo la kuhudumu, alisisitiza kwamba ilikuwa ni njia moja ya kutii amri kuu za kumpenda Mungu na kupendana sisi kwa sisi.1 Sisi, kama maafisa wa Kanisa, kwa wazi tunawaunga mkono na kuwapongeza juu ya mwitikio mkubwa mlioanza katika suala hilo. Tunawashukuru kwa kumfuata nabii wetu mpendwa katika jitihada hii ya kupendeza na kupendekeza kwamba msisubiri maelekezo mengine mengi zaidi. Rukeni tu ndani ya bwawa na muogelee. Waelekeeni wale wenye uhitaji. Msisimame mkishangaa ikiwa mnapaswa kuogelea kichali au kupiga kasia mbele. Kama tutafuata kanuni muhimu ambazo zimefundishwa, tukifungamana na funguo za ukuhani, na kumtafuta Roho Mtakatifu kutuongoza, hatuwezi kushindwa.

Asubuhi hii ninapenda kuzungumzia kipengele cha kibinafsi zaidi cha kuhudumu ambacho siyo cha kupangiwa, hakihusishi ratiba ya usahili, na hakina mtitiriko wa utoaji ripoti isipokuwa mbinguni. Acha nishiriki mfano mmoja rahisi wa aina hiyo ya kuhudumu.

Grant Morrell Bowen alikuwa mume mchapa kazi, mwenye bidii na baba ambaye, kama wengi ambao walipata kipato katika ardhi, aliyumba kiuchumi wakati zao la viazi vya eneo lao lilipokuwa duni. Yeye na mke wake, Norma, walichukua ajira nyingine, hatimaye kuhamia jiji lingine, na kuanza jitihada zao kurudi kwenye kutengemaa kiuchumi. Hata hivyo, katika tukio la bahati mbaya sana, Kaka Bowen aliumizwa sana wakati, katika usahili wa kibali cha hekaluni, askofu alikuwa na mashaka kuhusu tamko la Morrell kwamba alikuwa mlipa zaka‑kamili.

Sijui yupi kati ya wanaume hawa wawili alikuwa na ukweli sahihi siku hiyo, lakini ninajua Dada Bowen alitoka nje ya usahili ule akiwa na kibali chake kipya cha hekaluni, wakati Kaka Bowen akitoka nje kwa hasira ambayo ingemuondoa Kanisani kwa miaka 15.

Bila kujali nani alikuwa sahihi kuhusu zaka, ni wazi wote Morrell na askofu walisahau amri ya Mwokozi ya “patana na mshitaki wako upesi”2 na ushauri wa Paulo wa “jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.”3 Ukweli ni kwamba hawakupatana na jua lilikuchwa na uchungu wa Kaka Bowen kwa siku nyingi, kisha wiki, kisha miaka, ikithibitisha jambo lililosemwa na mmoja wa wenye hekima wa Rumi ya kale, ambaye alisema, “Hasira, kama haitazuiliwa, huwa kawaida [haribifu] zaidi kuliko jeraha lililoisababisha.”4 Lakini muujiza wa upatanisho daima upo kwetu, na kwa upendo kwa familia yake na Kanisa alilojua kuwa ni la kweli, Morrell Bowen alirudi kwenye ushiriki hai Kanisani. Acha niwaambie kwa ufupi hilo lilitokeaje.

Brad kijana wa Kaka Bowen ni rafiki yetu mzuri na Sabini wa Eneo mwaminifu anayehudumu Idaho ya kusini. Brad alikuwa na miaka 11 wakati wa tukio hili, na kwa miaka 15 aliangalia uaminifu wa kidini wa baba yake ukififia, ushahidi wa mavuno mabaya yakivunwa mahali ambapo hasira na kutokuelewana vilikua vimepandwa. Kitu fulani kilihitaji kufanywa. Hivyo wakati sherehe ya Shukrani ilipokaribia mnamo 1977, Brad, mwanafunzi wa miaka 26 katika Chuo Kikuu cha Brigham Young; mke wake, Valerie; na mtoto wa kiume, Mic, walijipakia ndani ya gari lao la kiuanafunzi na, bila kujali hali mbaya ya hewa, walielekea Billings, Montana. Siyo hata mgongano katika kingo za theluji karibu na West Yellowstone kungewazuia watatu hawa kufanya huduma yao kwa kufika kwa Kaka Bowen mkubwa.

Walipofika, Brad na Pam dada yake waliomba muda wa faragha na baba yao. “Umekua baba mzuri,” Brad alianza kwa hisia fulani, “na daima tumejua ni kiasi gani unatupenda. Lakini kitu fulani hakiko sawa, na kimekuwa kwa muda mrefu. Kwa sababu uliumizwa mara moja, familia hii yote imekuwa ikiumia kwa miaka. Tumevunjika, na ni wewe pekee unayeweza kutuunganisha. Tafadhali, baada ya muda wote huu, unaweza kutafuta katika moyo wako kuweka kando tukio lile la bahati mbaya na askofu na kuiongoza tena familia hii katika injili kama ulivyofanya awali?”

Kulikuwa kimya kabisa. Kisha kaka Bowen akawatazama wawili hawa, ambao walikuwa mifupa katika mfupa wake na nyama katika nyama yake,5 na kusema kwa upole, “Ndiyo. Ndiyo, nitafanya.”

Kwa furaha lakini kwa mshtuko wa jibu lisilotarajiwa, Brad Bowen na familia yake walimtazama mume na baba yao akienda kwa askofu wake wa wakati huo katika roho ya upatanisho kuweka mambo sawa katika maisha yake. Kwa mjibizo mkamilifu kwa matembezi haya ya ujasiri lakini yasiyotarajiwa, askofu, ambaye alitoa mialiko ya kujirudia kwa Kaka Bowen kurudi, alirusha mikono yake kumzunguka Morrell na kumkumbatia—kumkumbatia kwa muda mrefu, mrefu, mrefu sana.

Kadiri ya wiki chache tu—haichukui muda mrefu—Kaka Bowen alishiriki tena kikamilifu Kanisani na alijiweka mwenye kustahili kurudi hekaluni. Mapema vya kutosha alikubali wito wa kusimamia tawi dogo lililojitahidi la watu 25 na kulikuza kwenye mkusanyiko uliostawi wa zaidi ya watu 100. Yote haya yalifanyika karibu nusu karne iliyopita, lakini matokeo ya ombi la kuhudumu la kijana na binti kwa baba yao na utayari ule wa baba kusamehe na kusonga mbele licha ya mapungufu ya wengine vimeleta baraka ambazo zinaendelea kuja—na zitakuja daima—kwenye familia ya Bowen.

Akina kaka na kina dada, Yesu ameomba kwamba “tuishi pamoja katika upendo”6 bila “ugomvi miongoni mwenu.”7 “Yule ambaye ana roho ya ubishi siye wangu,” Yeye aliwaonya Wanefi.8 Hakika, kwa kiasi kikubwa, uhusiano wetu kwa Kristo utaamuliwa—au angalau kuathiriwa—kwa uhusiano wetu na kila mmoja wetu.

“Ikiwa … utatamani kuja kwangu,” Yeye alisema, “na ukumbuke kwamba ndugu yako anacho kitu dhidi yako—

“Nenda njia yako kwa ndugu yako, na kwanza ondoa tofauti na [yeye], na hapo uje kwangu, na moyo wa lengo moja, na nitakupokea.9

Hakika kila mmoja wetu angeweza kutaja kwa mpangilio usio na mwisho makovu ya zamani na kumbukumbu ya huzuni na maumivu ambayo wakati huu hasa bado yanaharibu amani katika moyo wa mtu au familia au ujirani. Kama tumesababisha maumivu hayo au tumepokua wapokeaji, vidonda hivyo vinahitaji kuponywa ili maisha yaweze kuwa na thawabu kama Mungu anavyokusudia yawe. Kama vile chakula ndani ya jokofu lako ambacho wajukuu zako hukiangalia kwa makini kwa niaba yako, masikitiko hayo ya zamani yamepita kwa muda mrefu mwisho wake wa matumizi. Tafadhali usiyape nafasi ya thamani tena katika nafsi yako. Kama Prospero alivyosema kwa Alonso mwenye majuto katika The Tempest, “Acha tusiipe mzigo kumbukumbu yetu kwa uzito ambao umepita.”10

“Achilieni nanyi mtaachiliwa,”11 Kristo alifundisha katika nyakati za Agano Jipya. Na katika siku yetu: “Mimi, Bwana, nitamsamehe yule nitakaye kumsamehe, lakini ninyi mnatakiwa kuwasamehe watu wote.”12 Hata hivyo, ni muhimu kwa yeyote kati yenu anayeishi katika uchungu halisi kukumbuka kile ambacho Bwana hakusema. Yeye hakusema, “Hauruhusiwi kuhisi uchungu wa kweli au huzuni halisi kutokana na uzoefu wa kukasirisha uliowahi kupata kwenye mkono wa mwingine.” Wala Yeye hakusema, “Ili kusamehe kikamilifu unapaswa kuingia tena kwenye uhusiano wa kudhuru au kurejea tena hali ya fedheha ya kuangamiza.” Lakini bila kujali hata makwazo makubwa kabisa ambayo yanaweza kuja, tunaweza kuinuka juu ya maumivu yetu pale tu tunapoweka miguu yetu kwenye njia ya uponyaji wa kweli. Njia hiyo ni ya msamaha aliyotembea Yesu wa Nazareti, ambaye anatuita kila mmoja wetu, “Njoo, unifuate.”13

Katika mwaliko huo wa kuwa mfuasi Wake na kujaribu kufanya kama Yeye alivyofanya, Yesu anatuomba kuwa vyombo vya neema Yake—kuwa “wajumbe kwa ajili ya Kristo” katika “huduma ya upatanisho,” kama Paulo alivyoelezea kwa Wakorintho.14 Mponyaji wa kila jeraha, Yeye ambaye hurekebisha kila kosa, anatuomba kufanya Naye kazi katika jukumu la kuogofya la kuleta upatanishi katika ulimwengu ambao hautaupata kwa njia nyingine yoyote.

Hivyo, kama Phillips Brooks alivyoandika: “Ninyi ambao mnaruhusu huzuni za kutokuelewana kuendelee mwaka hadi mwaka, mkinuia kuziondoa siku moja; ninyi ambao mnafanya huzuni ya ugomvi kuendelea kuwa hai kwa sababu hamuwezi hasa kufanya maamuzi kwamba sasa ni siku ya kutoa dhabihu kiburi chenu na [kuyamaliza]; ninyi ambao mnawapita watu kwa kinyongo mtaani, bila kuongea nao kwa sababu ya chuki ya kipuuzi … ; ninyi mnaoruhusu … maumivu ya moyo ya [mtu fulani] kwa neno la shukrani au huruma, ambalo mnakusudia kulitoa … siku moja, … nendeni haraka na kutenda vitu ambavyo mnaweza msipate nafasi ya pili ya kuvitenda.”15

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, ninashuhudia kwamba kusamehe na kuacha makwazo, ya zamani au ya sasa, ni kitovu cha utukufu wa Upatanisho wa Yesu Kristo. Ninashuhudia kwamba mwishowe uponyaji huo wa kiroho unaweza kuja kutoka tu kwa Mkombozi wetu mtakatifu, Yeye ambaye huarakisha kutupa msaada “na uponyaji katika mbawa zake.”16 Tunamshukuru Yeye, na Baba yetu wa Mbinguni aliyemtuma, kwamba kufanywa upya na kuzaliwa upya, wakati ujao ulio huru kutokana na huzuni ya zamani na makosa yaliyopita, siyo tu vinawezekana bali tayari vimenunuliwa, na kulipiwa, kwa gharama ya mateso inayoashiriwa na damu ya Mwanakondoo aliyoimwaga.

Kwa mamlaka ya kitume yaliyoidhinishwa kwangu na Mwokozi wa ulimwengu, ninashuhudia juu ya amani ya nafsi ambayo upatanisho na Mungu na kila mmoja utaleta kama tu wanyenyekevu na wenye ujasiri kuutafuta. “Acheni kugombana ninyi kwa ninyi,” Mwokozi alisihi.17 Kama unafahamu dhara la zamani, lirekebishe. Jalianeni kwa upendo.

Rafiki zangu wapendwa, katika huduma yetu ya pamoja ya upatanisho ninawaomba tuwe wapatanishi—tupende amani, tutafute amani, tutengeneze amani, tuitunze amani. Ninafanya ombi hilo katika jina la Mfalme wa Amani, ambaye anajua kila kitu kuhusu “kujeruhiwa katika nyumba ya rafiki [zake]”18 lakini ambaye bado alipata nguvu ya kusamehe na kusahau—na kupona—na kuwa na furaha. Kwa hilo ninaomba, kwa ajili yenu na kwa ajili yangu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, amina.