2010–2019
Sasa Ndiyo Wakati
Oktoba 2018


Sasa Ndiyo Wakati

Kama kuna chochote katika maisha yako unahitaji kufikiria, wakati ndio sasa.

Miaka kadha iliyopita, wakati nikijiandaa kwa ajili ya safari ya kibiashara, Nilianza kuhisi maumivu kifuani. Kutokana na mashaka, mke wangu aliamua kufuatana nami. Kwenye sehemu ya kwanza ya masafa yetu ya mruko, maumivu yalizidi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kwangu kupumua. Wakati tulipotua, tuliondoka uwanja wa ndege na kwenda kwenye hospitali ya eneo lile, ambako, baada ya uchunguzi mwingi, daktari aliyekuwa aki tuhudumia alisema tulikuwa salama kuendelea na safari yetu.

Tulirudi uwanja wa ndege na kuingia kwenye ndege kuelekea mwisho wa safari yetu. Tulipokuwa tukitua, rubani akitumia mawasiliano ya ndani ya ndege aliniomba nijitambulishe. Msaidizi wa ndege alikuja, akasema wamepokea mwito wa dharura muda ule, na aliniambia kulikuwa na gari la wagonjwa linasubiri uwanjani kutuchukuwa kutupeleka hospitalini.

Tuliingia katika gari la wagonjwa na tulikimbizwa kwenye chumba cha dharura kwenye eneo lile. Pale, tulikutana na madaktari wawili wenye wasiwasi ambao walieleza kwamba ugonjwa wangu umebainiwa kimakosa na ukweli hasa nilikuwa na pulmonary ambolism mbaya, au donge hatari la damu,katika pafu langu,ambalo lilihitaji uangalizi wa tiba mara moja. Madaktari walitufahamisha kwamba wagonjwa wengi hawaponi kutokana na hali hii. Tukijua tulikuwa mbali na nyumbani na hatuna hakika kama tulikua tayari kwa matukio ya kubadilisha maisha kama yale, madaktari walisema kwamba kama kulikuwa na chochote katika maisha yetu ambacho tulihitaji kufikiria, wakati ulikuwa ni sasa.

Ninakumbuka vyema jinsi takribani mara moja katika wakati ule wa wasiwasi mtazamo wangu wote ulibadilika. Kilichoonekana ni muhimu sana muda mfupi hapo mwanzo sasa kilikuwa na mvuto mdogo sana. Mawazo yangu yalitoka kwa kasi kutoka starehe na uangalizi wa maisha haya kwenda kwenye mtazamo wa milele—mawazo ya familia, watoto, mke wangu, na hatimaye tathmini ya maisha yangu mwenyewe.

Jinsi gani tulikua tunafanya kama familia na kibinafsi? Je, tulikuwa tukiishi maisha yetu kithabiti na maagamo tuliyoyafanya na matarajio ya Bwana, au pengine bila kukusudia tuliruhusu uangalizi wa dunia kutuvuta kutoka vitu hivyo ambavyo ni vya maana sana?

Ningependa kuwaalika ninyi kufikiria somo muhimu tulilojifunza kutokana na uzoefu huu: kupiga hatua nyuma kutoka ulimwenguni na kutathmini maisha yako. Au kwa maneno ya daktari, kama kuna chochote katika maisha yako unahitaji kufikiria, wakati ndio sasa.

Kutathmini Maisha Yetu

Tunaishi katika ulimwengu wa taarifa nyingi kupita kiasi, zilizotawaliwa na uvutaji wa mawazo unaoongezeka ambao unafanya zaidi na zaidi vigumu kuchagua kupitia vurugu za maisha haya na kufokasi kwenye vitu vya thamani ya milele. Maisha yetu ya kila siku yana shambuliwa na vichwa vya habari vinavyonyakua umakini wetu, vinavyoletwa na teknolojia zinazobadilika kwa haraka.

Ila tuchukuwe muda kutafakari, tunaweza tusielewe athari ya mwendo huu wa haraka wa mazingira juu ya maisha yetu ya siku zote na chaguzi tunazofanya. Tunaweza kukuta maisha yetu yameharibiwa na taarifa zilizoingia ghafla zilizojazwa katika vichekesho, video, na vichwa vya habari dhahiri. Japokuwa ni vya kuvutia na kufurahisha, vingi vya hivi vina athari ndogo kwenye maendeleo yetu ya milele, na bado vinatengeneza jinsi tunavyoona uzoefu wetu wa maisha haya ya duniani.

Vivutio hivi vya kiulimwengu vingeweza kufananishwa na vile katika ndoto ya Lehi. Tunapoendelea kwenye njia ya agano na mkono wetu kwa uthabiti umeshikilia kwenye fimbo ya chuma, tunawasikia na kuwaona wale “wanaodhihaki na kuonesha kwa vidole vyao” kutoka kwenye jengo kubwa na pana (1 Nefi 8:27). Tunaweza kwa kufahamu tusikusudie kufanya hivyo, lakini wakati mwingine tunasimama na kuhamisha kukaza kwetu macho kuona vurugu hizi ni za nini. Baadhi yetu tunaweza hata kuachia fimbo ya chuma na kusogea karibu zaidi kwa ajili ya kuangalia vyema zaidi. Wengine wanaweza kupotea kabisa “kwa sababu ya hao ambao walikuwa wakiwakejeli” (1 Nefi 8:28).

Mwokozi alitutahadharisha “jiangalieni … mioyo yenu isije ikalemewa na … masumbufu ya maisha haya” (Luka 9:34) Ufunuo wa siku za leo unatukumbusha kwamba wengi huitwa, lakini wachache huteuliwa. Hawateuliwi “Kwa sababu mioyo yao imekuwa … juu ya mambo ya ulimwengu huu, na kutafuta kupata heshima kutoka kwa wanadamu” (Mafundisho na Maagano 121:35; ona pia mstari wa 34) Kutathmini maisha yetu kunatupa fursa ya kupiga hatua kutoka kwenye ulimwengu, kutafakari pale tulipo kwenye njia ya agano, na, kama ni muhimu, kufanya marekebisho kuhakikisha mshiko madhubuti na kukaza macho kuelekea mbele.

Hivi karibuni,katika ibada ya vijana ulimwenguni kote, Rais Russell M. Nelson aliwataka vijana kupiga hatua kutoka kwenye ulimwengu, kujitoa kutoka kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa na mfungo wa siku saba. Na jioni ya jana, ametoa mwaliko sawa na huo kwa akina dada kama sehemu ya kikao cha wanawake cha mkutano. Kisha aliwataka vijana kugundua tofauti yoyote kwenye jinsi wanayohisi, kile wanachofikiri, au hata jinsi wanavyofikiri. Kisha aliwaalika “kufanya tathmini kamili na Bwana … kuhakikisha kwamba miguu yako imesimama kiuthabiti kwenye njia ya agano.” Aliwatia moyo kwamba kama kulikuwa na vitu katika maisha yao ambavyo vilihitaji kubadilika, “leo ni muda muafaka kubadili.”1

Katika kutathmini vitu katika maisha yetu vinavyohitaji mabadiliko, tungeweza kujiuliza wenyewe swali la kiutendaji: Ni kwa jinsi gani tunaweza kuinuka juu ya vivutio vya ulimwengu huu na kubaki tumeimarika kwenye maono ya milele mbele yetu?

Katika hotuba ya mkutano mnamo 2007 yenye kichwa vya habari “Nzuri, Nzuri kiasi, Nzuri zaidi,” Rais Dallin H. Oaks alifundisha jinsi ya kuweka kipaumbele cha chaguzi miongoni mwa matakwa yetu mengi ya kiulimwengu yanayopingana. Alishauri, “Hatuna budi kuacha baadhi ya vitu vizuri ili tuchague vingine ambavyo ni vizuri kiasi au vizuri zaidi kwa sababu vinajenga imani katika Bwana Yesu Kristo na kuimarisha famila zetu.”2

Naomba nipendekeze kwamba vitu vizuri zaidi katika maisha haya kiini chake ni juu ya Yesu Kristo na kuelewa kweli za milele za jinsi Yeye alivyo na jinsi sisi tulivyo katika mahusiano yetu na Yeye.

Tafuta Ukweli

Tunapotafuta kumjua Mwokozi, hatupaswi kupitia juu juu ukweli wa msingi wa sisi ni nani na kwa nini tupo hapa. Amuleki anatukumbusha kwamba “maisha haya ndiyo wakati … wa kujitayarisha kukutana na Mungu,” muda “ambao tumepewa kujitayarisha kwa ajili ya milele” (Alma 34:32–33). Kama msemo unaojulikana vyema unavyotukumbusha, “Sisi sio binadamu tulio na uzoefu wa kiroho. Sisi ni viumbe vya kiroho tulio na uzoefu wa kibinadamu.”3

Kuelewa asili yetu takatifu ni muhimu kwa maendeleo yetu ya milele na kunaweza kutuweka huru kutoka kwenye vivutio vya maisha haya. Mwokozi alifundisha:

“Ninyi mkikaa katika neno langu,mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;

“Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:31–32).

Rais Joseph F. Smith alitangaza, “Mafanikio makubwa sana binadamu anayoweza kufanya katika ulimwengu huu ni kujizoesha wenyewe na ukweli wa milele, kikweli kweli, kikamilifu, kwamba hakuna mfano au tabia ya kiumbe chochote kinachoishi katika ulimwengu kinaweza kuwageuza mbali kutoka kwenye ufahamu ambao wameupata.”4

Katika ulimwengu leo, mdahalo juu ya ukweli umefikia hali ya kusisimua sana, na pande zote zikidai ukweli kama vile ulikuwa wazo linalohusiana lililo wazi kwa tafsiri binafsi. Kijana mdogo Joseph Smith aligundua kwamba kulikuwa na “mchafuko mkubwa na mzozo” katika maisha yake “kwamba ilikuwa ni vigumu … kuweza kufikia uamuzi wa nani ni sahihi na nani si sahihi” (Historia ya Joseph Smith—1:8). Ilikuwa “Katikati ya vita hivi vya maneno na makelele ya maoni” kwamba alitafuta mwongozo mtakatifu kwa kutafuta ukweli (Historia ya—Joseph Smith 1:10).

Katika mkutano mkuu wa April, Rais Nelson alifundisha, “Kama tunatakiwa kuwa na matumaini yo yote ya kupekua kupitia sauti nyingi sana na falsafa za watu ambazo zinashambulia ukweli, lazima tujifunze kupokea ufunuo.”5 Lazima tujifunze kutegemea kwenye Roho wa Ukweli, ambae “ilimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa hawamuoni, wala haumtambui” (Yohana 14:17).

Wakati ulimwengu ukisogea kwa haraka kwenye ukweli mbadala, lazima tukumbuke maneno ya Yakobo kwamba “Roho huzungumza ukweli wala sio uwongo. Kwa hivyo, huzungumza kuhusu vile vitu vilivyo, na vile vitu vitavyokuwa; kwa hivyo, tunadhihirishiwa vitu hivi wazi wazi, kwa wokovu wa nafsi zetu” (Yakobo 4:13).

Tunapopiga hatua kutoka ulimwenguni na kutathmini maisha yetu, sasa ndio muda wa kufikiria mabadiliko gani tunahitahi kufanya. Tunaweza kuwa na tumaini kubwa katika kujua kwamba Mfano wetu, Yesu Kristo, mara nyingine tena ameongoza njia. Kabla ya kifo Chake na Kufufuka, alipokuwa akifanya kazi kuwasaidia wale waliokuwa wamemzunguka kuelewa wajibu Wake mtakatifu, Aliwakumbusha “kwamba ndani yangu mnaweza kupata amami. Ulimwenguni mnayo dhiki: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33). Kwa yeye, mimi ninatoa ushahidi katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli” (ibada ya vijana ulimwenguni kote, June 3, 2018), hopeofisrael.lds.org.

  2. Dallin H. Oaks, “Nzuri, Nzuri kiasi, Nzuri zaidi,” Liahona, Nov. 2007, 107.

  3. Mara nyingi hupata sifa kwa Pierre Teilhard de Chardin

  4. Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph F. Smith(1998), 42.

  5. Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa Kanisa, Ufunuo kwa ajili Ya Maisha Yetu,”Liahona,Mei 2018, 96.