2010–2019
Wanawake na Kujifunza Injili Nyumbani
Oktoba 2018


Wanawake na Kujifunza Injili Nyumbani

Mwokozi ni mfano wenu mtimilifu wa jinsi mnavyotakiwa muwe sehemu kubwa katika nia Yake ya kuweka msisitizo mkubwa juu ya kujifunza injili nyumbani.

Dada zangu wapendwa, ni ajabu kukutana nanyi. Huu ni muda wa kusisimua katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Bwana anamimina elimu kwenye Kanisa Lake kama alivyoahidi angefanya.

Mnakumbuka kile alichosema: “Ni kwa muda gani maji yatembeayo yatabaki kuwa machafu? Ni nguvu gani zitazizuia mbingu? Kama vile mwanadamu asivyoweza kunyoosha mkono wake dhaifu kuusimamisha mto Missouri katika mkondo wake uliokusudiwa, au kuugeuza mtiririko wake kwenda juu, vivyo hivyo hawezi kumzuia Mwenyezi kumwaga chini elimu kutoka mbinguni juu ya vichwa vya Watakatifu wa Siku za Mwisho”1

Sehemu ya kushiriki elimu ya sasa ya Bwana inahusisha kuharakisha umiminaji Wake wa ukweli wa milele juu ya vichwa na katika mioyo ya watu Wake. Ameweka wazi kwamba mabinti wa Baba wa Mbinguni watafanya jukumu la msingi katika uharakishaji huo wa kimiujiza. Ushahidi mmoja wa muujiza ni kumwongoza Kwake nabii Wake anaishi kuweka msisitizo mkubwa kwenye maelekezo ya injili nyumbani na ndani ya familia.

Mnaweza kuuliza, “Hiyo inawezaje kuwafanya akina dada waaminifu nguvu ya msingi kumsaidia Bwana kumimina elimu juu ya Watakatifu Wake? Bwana anatoa jibu katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Mnakumbuka maneno, bali mnaweza kuona maana mpya na kutambua kwamba Bwana aliona kabla mabadiliko haya ya kusisimua ambayo sasa yanafanyika. Katika tangazo, aliwapa akina dada jukumu la kuwa waelimishashi wakuu wa injili katika familia katika maneno haya: “Akina mama kimsingi wanawajibu wa malezi ya watoto wao,”2 Hii inahusisha malezi ya ukweli wa injili na elimu.

Tangazo linaendelea: “Akina baba na kina mama wanawajibika kusaidiana kama wenza sawa.”3 Ni wenza walio sawa, sawa katika uwezo kwao kwa ajili ya ukuaji wa kiroho na kwa ajili ya kupata elimu, na kwa hiyo wameunganika kwa kusaidiana. Wako sawa katika majaliwa yao matakatifu kuinuliwa pamoja. Kwa kweli, wanaume na wanawake hawawezi kuinuliwa kila mtu peke yake.

Kwa nini, basi, binti wa Mungu katika mahusiano yaliyoungana na sawa anapokea wajibu wa msingi kulea kwa kirutubishi muhimu mno ambacho wote lazima wapate, elimu ya kweli kutoka mbinguni? Kwa jinsi ninavyoweza kuona, hiyo imekuwa njia ya Bwana tangu familia zilipoanzishwa katika ulimwengu huu.

Kwa mfano, ilikuwa Hawa aliyepokea elimu kwamba Adamu alihitaji kula tunda la mti wa elimu kwa ajili yao kutii amri zote za Mungu na kuanzisha familia. Sijui kwa nini ilikuja kwa Hawa kwanza, lakini Adamu na Hawa walikuwa wameungana kikamilifu wakati elimu ilipomiminwa kwa Adamu.

Mfano mwingine wa Bwana wa kutumia karama za kulea za wanawake ni jinsi aliyowaimarisha wana wa Helamani. Ninapata na mhemuko wakati ninaposoma maelezo na kukumbuka maneno tulivu ya mama yangu ya uhakika wakati nilipotoka nyumbani kwa ajili ya huduma ya kijeshi.

Helamani alirekodi:

“Walikuwa wamefundishwa na mama zao, kwamba kama wasingekuwa na shaka, Mungu angewaokoa.

“Na walirudia kwangu maneno ya mama zao, wakisema: Hatuna shaka kuwa mama zetu walijua.”4

Wakati sijui sababu zote za Bwana kuwapa uwajibikaji wa msingi wa malezi ya familia kwa akina dada waaminifu, ninaamini inatokana na uwezo wenu wa kupenda. Huchukua upendo mkuu kuhisi mahitaji ya mtu mwingine zaidi ya, ya kwako wenyewe. Huo ni upendo msafi wa Kristo kwa ajili ya mtu unayemlea. Hisia hiyo ya upendo msafi inakuja kutoka kwa mtu aliyechaguliwa kuwa mlezi aliyehitimu kwa ajili ya matokeo ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Wito wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, ambao mama yangu aliuonesha kwa mfano, unaonekana kwangu ni msukumo: “Hisani Haikosi Kufaulu Kamwe.”

Kama mabinti wa Mungu, mnayo hulka na uwezo mkubwa kuhisi mahitaji ya wengine na kupenda. Hiyo, kwa upande mwingine, huwafanya muwe wepesi kuhisi mino’gono ya Roho. Kisha Roho anaweza kuongoza kile unachofikiri, nini unasema, na nini unafanya kuwalea watu ili Bwana aweze kumimina elimu, ukweli, na ujasiri juu yao.

Ninyi akina dada mnaosikia sauti yangu kila mmoja yuko katika sehemu ya pekee katika safari yenu kupitia maisha. Baadhi ni wasichana wadogo katika kikao kikuu cha wanawake kwa mara ya kwanza. Baadhi ni wasichana wakubwa wakijiandaa kuwa walezi ambao Mungu angetaka wawe. Baadhi ni mmeolewa hivi karibuni ambao bado hamjapata watoto, wengine ni akina mama vijana walio na mtoto mmoja au zaidi. Baadhi ni akina mama wa vijana na wengine wenye watoto katika uwanja wa umisionari. Baadhi wana watoto ambao wamefifia katika imani na wako mbali na nyumbani. Baadhi wanaishi peke yenu bila mwenza mwaminifu. Baadhi ni kina bibi.

Bado, hali yako binafsi yoyote, wewe ni sehemu—sehemu muhimu—ya familia ya Mungu na ya familia yako mwenyewe, iwe ni hapo baadae, katika ulimwengu huu, au katika ulimwengu wa roho. Uaminifu wako kutoka kwa Mungu ni kulea kadiri uwezavyo wengi wa wanafamilia Yake na yako kadiri uwezavyo kwa upendo wako na imani yako katika Bwana Yesu Kristo.

Changamoto yako ya utendaji ni kujua nani wa kumlea, jinsi gani, na lini. Unahitaji msaada wa Bwana. Anajua mioyo ya wengine, na anajiua wakati gani ipo tayari kukubali kulelewa nawe. Maombi yako ya imani yatakuwa ufunguo wako wa mafanikio. Unaweza kutegemea kupokea mwongozo Wake.

Alitoa matumaini haya: “Mwombe Baba katika jina langu katika imani, ukiamini kwamba utapokea, na utapata Roho Mtakatifu, ambaye hudhihirisha mambo yote yaliyo muhimu.”5

Nyongeza katika maombi, mafunzo ya dhati ya maandiko yatakuwa sehemu ya uwezo wako unaokua wa kulea. Hapa kuna ahadi: “Wala msiwaze kabla nini cha kusema; bali yahifadhini katika akili zenu daima maneno ya uzima, nanyi mtapewa saa ile ile mtakayosema sehemu ile ambayo itakayokusudiwa kwa kila mtu.”6

Kwa hiyo mtachukuwa muda mwingi kuomba, kutafakari, na kuzingatia juu ya mambo ya kiroho. Mtakuwa na elimu ya ukweli iliyomiminwa juu yenu na kukua katika uwezo wenu wa kulea katika familia zenu.

Kutakuwa na muda mtakapohisi kwamba maendeleo yenu katika kujifunza jinsi gani bora zaidi ya kulea ni polepole. Itachukua imani kuvumilia. Mwokozi aliwatumia matumaini haya:

“Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu.

“Tazama, Bwana anahitaji moyo na akili yenye kukubali, na wenye kukubali na kutii watakula mema ya Sayuni katika siku hizi za mwisho.”7

Uwepo wenu usiku huu ni ushahidi kwamba mpo tayari kukubali mwaliko wa Bwana kulea wengine. Hiyo ni kweli hata kwa walio wadogo sana hapa usiku huu. Mnaweza kujua nani wa kumlea katika familia zenu. Kama mtaomba kwa dhamira ya kweli, jina au sura itakuja kwenye akili zako. Kama mtaomba ili mjue nini cha kufanya au nini cha kusema, mtahisi jibu. Kila muda unapotii, uwezo wako wa kulea unakua. Mtakuwa mnajiandaa kwa ajili ya siku mtakapowalea watoto wenu wenyewe.

Akina mama wa vijana wangeweza kuomba kujua jinsi ya kulea mwana au binti ambaye anaonekana asiyeshawishika kulelewa. Mnaweza kuomba kujua yule ambaye anaweza kuwa na ushawishi wa kiroho mtoto wako anahitaji na atakubali. Mungu anasikia na kujibu maombi ya kiroho kama hayo ya akina mama walio na wasiwasi, na Yeye huwatumia msaada.

Pia, bibi hapa usiku huu unaweza kuhisi huzuni kubwa iliyosababishawa na majaribu na matatizo ya watoto wake na wajukuu. Unaweza kuwa na ujasiri na mwelekeo kutokana na uzoefu wa familia katika maandiko.

Kutoka wakati wa Hawa na Adamu, mpaka Baba Israeli, na kwenye kila familia katika Kitabu cha Mormoni, kuna somo moja la uhakika: kamwe usiache kupenda.

Tuna mfano wa kutia moyo wa Mwokozi wakati Alipolea watoto waasi wa kiroho wa Baba yake wa Mbinguni. Hata wakati wao na sisi tunasababisha maumivu, mkono wa Mwokozi bado umenyooshwa.8 Alisema katika 3 Nefi juu ya dada na kaka Zake wa kiroho, ambao amejaribu bila mafanikio kuwalea: “Ee nyinyi … ambao ni wa nyumba ya Israeli, ni mara ngapi nimewakusanya kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa yake, na nimewalisha.”9

Kwa akina dada katika kila hatua ya safari ya maisha, katika kila hali ya familia, kupitia kila tamaduni, Mwokozi ni mfano wenu mtimilifu wa jinsi mnavyotakiwa muwe sehemu kubwa katika nia Yake ya kuweka msisitizo mkubwa juu ya kujifunza injili nyumbani.

Mtaleta hisia zenu za asili za upendo wa kweli kwenye mabadiliko katika utendaji na utekelezaji katika familia zenu. Hii italeta ukuaji mkubwa kiroho. Wakati mnapoomba pamoja na kwa ajili ya wanafamilia, mtahisi upendo wenu na wa Mwokozi kwa ajili yao. Hiyo itakuwa zaidi na zaidi karama yenu ya kiroho mnapoitafuta. Wanafamilia wenu wataihisi wakati mnapoomba kwa imani kubwa.

Wakati familia inapokusanyika kusoma maandiko kwa sauti, mtakuwa tayari mmeshayasoma na kuomba juu yake ili kujiandaa wenyewe. Mtakuwa mmepata muda mfupi kuomba kwa ajili ya Roho kuangaza akili zenu. Kisha, wakati ni zamu yako kusoma, wanafamilia watahisi upendo wako kwa Mungu na kwa neno Lake. Watalelewa na Yeye na Roho Wake.

Mmiminiko ule ule unaweza kuja katika mkusanyiko wa familia yoyote kama mkiomba na kupanga kwa ajili yake. Unaweza kuchukua juhudi na muda, lakini utaleta miujiza. Nakumbuka somo mama yangu alilofundisha nilipokuwa mdogo. Naweza bado kuona akilini mwangu ramani iliyopakwa rangi aliyotengeneza ya safari za Mtume Paolo. Nashangaa jinsi alivyopata muda na nguvu ya kufanya hivyo. Na mpaka leo nimebarikiwa na upendo wake kwa Mtume yule mwaminifu.

Kila mmoja atapata njia ya kuchangia kwenye mmiminiko wa ukweli juu ya familia katika Kanisa la urejesho la Bwana. Kila mmoja wenu ataomba, kujifunza, na kutafakari kujua nini mchango wako wa kipekee utakuwa. Lakini hiki najua: kila mmoja wenu, kiusawa mkifungwa nira pamoja na wana wa Mungu, itakuwa sehemu kubwa ya muujiza wa kujifunza injili na kuishi ambako kutaharakisha mkusanyiko wa Israeli na kutaandaa familia ya Mungu kwa ajili ya ujio mtukufu wa Bwana Yesu Kristo. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.