Agano la Kale 2022
Machi 7–3. Mwanzo 37–41: “Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu”


“Machi 7–3. Mwanzo 37–41: ‘Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Machi 7–3. Mwanzo 37–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Yusufu wa Misri kifungoni

Kielelezo cha Yusufu wa Misri kifungoni, na Jeff Ward

Machi 7–3

Mwanzo 37–41

“Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu”

Unaposoma Mwanzo 37–41, omba kwamba Roho Mtakatifu akusaidie kuona jinsi vipengele vya maandiko vinavyohusika na maisha yako. Andika utambuzi wowote unaopokea.

Andika Misukumo Yako

Wakati mwingine mambo mabaya hutokea kwa watu wema. Maisha yanatufundisha somo hilo kwa uwazi kabisa, na hivyo ndivyo yanavyofanya maisha ya Yusufu, mwana wa Yakobo. Yeye alikuwa mrithi wa agano Mungu alilofanya na baba zake, lakini alichukiwa na kaka zake na akauzwa utumwani. Yeye alikataa kukubali kulegeza masharti ya utu wake alipoendewa na mke wa Potifa na hivyo akatupwa gerezani. Ilionekana kwamba kadiri alivyokuwa mwaminifu zaidi, ndivyo alivyokabiliwa na magumu zaidi. Lakini uadui huo wote haukuwa ishara ya kibali cha Mungu. Ukweli, kupitia hayo yote, “Bwana alikuwa pamoja na yeye” (Mwanzo 39:3). Maisha ya Yusufu yalikuwa ni dhihirisho la ukweli huu muhimu: Mungu hatatuacha. “Kumfuata Mwokozi hakutaondoa majaribu yako yote,” Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha. “Badala yake, kutaondoa vizuizi kati yako na msaada ambao Baba yako wa Mbinguni anataka kukupatia. Mungu atakuwa pamoja na wewe” (“Hamu ya nyumbani,” Liahona, Nov. 2017, 22).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mwanzo 37:1–28; 39; 41:9–45

“Bwana alikuwa pamoja na Yusufu” katika shida zake.

Tena na tena, bahati njema ilionekana kukupotea kutoka kwa Yusufu, lakini Bwana kamwe hakumuacha. Unaposoma hadithi ya Yusufu, tafakari maswali kama haya: Je, Yusufu alifanya nini ili kukaa karibu na Bwana katika wakati wake wa majaribu? Je, ni kwa jinsi gani Bwana alikuwa “pamoja naye”? (Mwanzo 39:2–3, 21, 23).

Ungeweza kujiuliza maswali kama hayo hayo kuhusu maisha yako. Je, ni ushahidi gani umeuona kwamba Bwana hajakuacha katika nyakati zako za majaribu? Zingatia jinsi unavyoweza kushiriki uzoefu wako na washiriki wa familia na vizazi vya baadae (ona 1 Nefi 5:14). Je, unaweza kufanya nini sasa ili kujiandaa kubaki mwaminifu wakati utakapoyakabili majaribu katika wakati ujao?

Ona pia Yohana 14:18; Warumi 8:28; Alma 36:3; Mafundisho na Maagano 121:7–8; D. Todd Christofferson, “Shangwe ya Watakatifu,” Liahona, Nov. 2019, 15–18.

Mwanzo 37:5–11; 40; 41:1–38

Kama ntakuwa mwaminifu, Bwana ataniongoza na kunipa mwongozo wa kiungu.

Mzee David A. Bednar alifundisha, “Ufunuo hutolewa katika njia mbalimbali, ikiwemo, kwa mfano, ndoto, maono, mazungumzo na wajumbe wa mbinguni, na mwongozo wa kiungu” (“he Spirit of Revelation,” Liahona, Mei 2011, 88). Bwana alitumia ndoto kumfunulia ukweli Yusufu, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji wa Farao, na Farao. Bwana pia alimfunulia Yusufu jinsi ya kutafsiri ndoto hizo. Je, unaweza kujifunza nini kutoka Mwanzo 37:5–11; 40:5–8; 41:14–25, 37–38 kuhusu kupokea na kuelewa ufunuo kutoka kwa Bwana? Kwa mfano, unaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Yusufu wakati ufunuo unapoonekana mgumu kueleweka? (ona Mwanzo 40:8; 41:16).

Picha
Yusufu akiwa gerezani akitafsiri ndoto

Yusufu Anatafsiri Ndoto za Mnyweshaji na Mwokaji, na François Gérard

Tafakari jinsi Bwana anavyofunua mapenzi Yake kwako. Je, wewe unafanya nini ili kuufanyia kazi ufunuo ambao Bwana amekupatia? Je, ni kwa jinsi gani wewe unatafuta mwongozo wa ziada kutoka Kwake?

Ona pia Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili Ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 93–96; Michelle Craig, “Uwezo wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2019, 19–21.

Mwanzo 38; 39:7–20

Kwa msaada wa Bwana, ninaweza kuyakimbia majaribu.

Wakati unapokuwa unajaribiwa, mfano wa Yusufu unaweza kukutia moyo na nguvu. Unaposoma kuhusu uzoefu wake katika Mwanzo 39, tambua mambo ambayo Yusufu aliyafanya ili kupinga vishawishi. Kwa mfano:

  • Yeye “alikataa” kujipendekeza kwa mke wa Potifa (mstari wa 8).

  • Yeye alitambua kwamba kutenda dhambi angemkosea Mungu na wengine (mstari wa 8–9).

  • Yeye “hakuyasikiliza” majaribu hayo, ingawa yaliendelea “siku hadi siku” (mstari wa 10).

  • Yeye “aliacha nguo yake … na akakimbia, akatoka nje” (mstari wa 12).

Kwa mfano wa Yusufu ukiwa akilini, fikiria kutengeneza mpango kwa ajili ya kukwepa na kupinga vishawishi. Kwa mfano, ungeweza kufikiria juu ya kishawishi unachokabiliana nacho, andika chini hali za kuepuka, na tengeneza mpango wa kumtegemea Baba wa Mbinguni wakati kishawishi kinapoibuka (ona 2 Nefi 4:18, 27–33).

Kishawishi:

Hali za kuepuka:

Mpango wa kujibu:

Hadithi hii juu ya nguvu za Yusufu wakati akikabiliwa na kishawishi inatanguliwa na hadithi iliyo tofauti sana kuhusu kaka yake mkubwa Yuda, inayopatikana katika Mwanzo 38. Je, mlango wa 37, 38, na 39, ikichukuliwa pamoja, inakufundisha wewe kuhusu usafi wa kimwili?

Ona pia 1 Wakorintho 10:13; 1 Nefi 15:23–24; 3 Nefi 18:17–18.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mwanzo 37.Kama wewe ungekuwa mmoja wa kaka zake Yusufu, ungeweza kufanya nini ili kuzuia wivu usidhoofishe uhusiano wako na yeye? Je, ingetusaidiaje “kuongea kwa amani kabisa” na kila mtu? (mstari wa 4).

Mwanzo 39.Video “The Refiner’s Fire” and “After the Storm” (ChurchofJesusChrist.org) zinaelezea juu ya uzoefu wa watu ambao walipata nguvu kwa kumgeukia Bwana wakati wa majaribu yao. Labda mngeweza kuangalia mojawapo na mkaongelea kuhusu kile Yusufu anaweza kusema kama angetakiwa kutengeneza video kuhusu uzoefu wake. Mnaweza kuimba pamoja “I’m Trying to Be Like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79) na mtafute ushauri ambao familia yako ingeweza kushirikiana na Yusufu alipokabiliana na majaribu yake.

Mwanzo 39:7–12.Kusoma mistari hii ingeweza kukupa fursa ya kujadili sheria ya usafi wa kimwili pamoja na familia yako. Hapa kuna baadhi ya nyenzo ambazo zingeweza kusaidia katika mjadala huu: Yakobo 2:28; Alma 39:3–9; “Sexual Purity” (katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana [2011], 35–37); “Sexual Intimacy Is Sacred and Beautiful” (katika Help for Parents [2019], AddressingPornography.ChurchofJesusChrist.org).

Mwanzo 41:15–57.Je, tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu jinsi Bwana alivyowabariki watu wa Misri kupitia Yusufu? Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu kujitayarisha kwa ajili ya tahadhari za siku za usoni? Jadili mnaweza kufanya nini ili kujitayarisha vyema kama familia. Kwa mawazo, ona Mada za Injili, “Emergency Preparedness,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Jesus Is Our Loving Friend,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 58.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Linganisha maandiko na maisha Yako. Unaposoma, fikiria ni kwa jinsi gani hadithi na mafundisho katika maandiko yanahusika katika maisha yako. Kwa mfano, jinsi gani uaminifu wa Yusufu katika Misri kunaweza kukushawishi wewe kubaki mwaminifu kwa Bwana licha ya shida?

Picha
Kaka zake Yusufu wakimnyang”anya koti lake

Kielelezo cha kaka zake Yusufu wakimnyang”anya koti lake, na Sam Lawlor