Agano la Kale 2022
Mawazo ya Kuweka Akilini: Nyumba ya Israeli


“Mawazo ya Kuweka Akilini: Nyumba ya Israeli,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mawazo ya Kuweka Akilini: Nyumba ya Israeli,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
ikoni ya mawazo

Mawazo ya Kuweka Akilini

Nyumba ya Israeli

Mahali fulani nyikani mashariki mwa Kanaani, Yakobo akiwa mwenye wasiwasi alisubiria kukutana na Esau kaka na pacha wake. Mara ya mwisho Yakobo kumuona Esau, ilikuwa takribani miaka 20 iliyopita, Esau alikuwa akitishia kumuua. Yakobo ametumia usiku mzima akipigana mieleka nyikani, akitafuta baraka kutoka kwa Mungu. Kama matokeo ya imani ya Yakobo, msimamo na azma yake, Mungu alijibu maombi yake. Usiku ule jina la Yakobo lilibadilishwa na kuwa Israeli, jina ambalo maana yake ni “alishindana na Mungu” (Mwanzo 32:28, tanbihi b; ona pia Mwanzo 32:24–32).1

Picha
mto Yaboki

Karibu na mto huu Yaboki, Yakobo alipokea jina la Israeli.

Hii ni mara ya kwanza jina Israeli linaonekana katika Biblia, na ni jina ambalo litabakia hadi mwisho wa kitabu na hadi mwisho wa historia. Jina ambalo punde likaja kuitwa kwa zaidi ya mtu mmoja. Israeli alikuwa na wana 12, na wazao wao kwa ujumla walijulikana kama “nyumba ya Israeli,” “kabila za Israeli,” “watoto wa Israeli,” au “Waisraeli.”

Kote katika historia, watoto wa Israeli walifahamika zaidi kutokana na kuzaliwa kwao kutoka katika moja ya kabila kumi na mbili za Israeli. Nasaba yao ilikuwa sehemu muhimu ya utambulisho wao wa agano. Mtume Paulo alitangaza kwamba yeye alikuwa “wa kabila ya Benyamini” (Warumi 11:1). Wakati Lehi alipowatuma wanawe Yerusalemu kuchukuwa mabamba ya shaba, moja ya sababu ilikuwa kwamba mabamba yale yalikuwa na “historia ya nasaba ya baba zake” (1 Nefi 5:14; ona pia 1 Nefi 3:3). Lehi aligundua kwamba yeye alikuwa wa uzao wa Yusufu, na uelewa wa watoto wake juu ya muunganiko wao kwenye nyumba ya Israeli ulithibitika kuwa wa muhimu kwao katika miaka ijayo (ona Alma 26:36; 3 Nefi 20:25).

Katika Kanisa leo, unaweza ukasikia kuhusu Israeli katika maongezi kama “kukusanywa kwa Israeli.” Tunaimba kuhusu “Redeemer of Israel,” “Hope of Israel,” na “Ye Elders of Israel.”2 Katika masuala haya, hatuongelei au kuimba tu kuhusu ufalme wa kale wa Israeli au lile taifa la sasa liitwalo Israeli. Bali, tunawataja wale ambao wamekusanywa kutoka mataifa ya ulimwengu kuja katika Kanisa la Yesu Kristo. Tunawataja watu ambao wameshindana na Mungu, ambao kwa dhati wanatafuta baraka Zake, na ambao, kupitia ubatizo, wamekuwa watu Wake wa agano.

Baraka zako za patriaki zinatamka uhusiano wako na moja ya kabila za nyumba ya Israeli. Hiyo ni zaidi ya kipande cha kufurahisha cha taarifa ya historia ya familia. Kuwa sehemu ya nyumba ya Israeli inamaanisha kwamba wewe una uhusiano wa kiagano na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Ina maana kwamba wewe, kama Ibrahimu, unakusudiwa “kuwa baraka” kwa watoto wa Mungu (Mwanzzo 12:2; Ibrahimu 2:9–11). Ina maana, katika maneno ya Petro, kwamba “ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu; mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Peter 2:9). Inamaanisha kwamba wewe ni mtu ambaye “umeshindana na Mungu” kwa kadiri unapoheshimu maagano yako wewe na Yeye.

Mihtasari

  1. Kuna uwezekano wa maana nyingine kwa ajili ya jina Israeli, ikijumuisha “Mungu anatawala” au “ Mungu anapigana au anashindana”

  2. Nyimbo za Kanisa, na. 6, 259, na 319.

Picha
Mti wa Familia ya Yakobo

Kielelezo cha mti wa familia ya Yakobo, na Keith L. Beavers