Misaada ya Kujifunza
TJS, Yakobo (Bib.) 2


TJS, Yakobo 2:1. Linganisha na Yakobo 2:1

Waumini hawapaswi kumwona mtu mmoja kuwa ni bora kuliko mwingine.

1 Ndugu zangu, hamuwezi kuwa na imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, na bado mkawapendelea watu.

TJS, Yakobo 2:14–21. Linganisha na Yakobo 2:14–22

Imani bila matendo imekufa na haiwezi kuokoa.

14 Ina faida gani, ndugu zangu, kwa mtu kusema ana imani, na hana matendo? Je ile imani itamwokoa?

15 Ndiyo, mtu anaweza kusema, Nitakuonesha nina imani bila matendo; bali ninasema, Nioneshe imani yako bila matendo, na nitakuonesha imani yangu kwa matendo yangu.

16 Kwani kama kaka au dada wako uchi na fukara, na mmoja wenu akasema, Ondokeni kwa amani mkaote moto na kushiba; ijapo kuwa hakuwapeni vitu vile ambavyo vinahitajika na mwili; imani yako inafaida gani katika hilo?

17 Hata hivyo imani, kama haina matendo imekufa ikiwa peke yake.

18 Kwa hiyo na ujue, Ewe mtu mwenye majivuno, kwamba imani bila matendo imekufa na haiwezi kukuokoa?

19 Wewe unaamini kuna Mungu mmoja; unafanya vyema; mashetani pia wanaamini, na kutetemeka; umejifanya kama wao, wasiothibitishwa.

20 Hakuwa Ibrahimu baba yetu aliyethibitishwa kwa matendo, wakati alipomtoa Isaka juu ya madhabahu?

21 Je mnaona jinsi matendo yalivyoguswa na imani yake, na kwa matendo imani ilikamilishwa?