Misaada ya Kujifunza
TJS, Isaya 42


TJS, Isaya 42:19–23. Linganisha na Isaya 42:19–22

Bwana anamtuma mtumishi Wake ili awafundishe wale ambao wamechagua kutoona au kusikia ukweli; wale wasikiao na kutii watafanywa kuwa wakamilifu.

19 Kwani nitawatuma watumishi wangu kwenu ninyi mlio vipofu; ndiyo mjumbe wa kufungua machoya kipofu, na kuzibua masikio ya kiziwi;

20 Nao watakamilishwa licha ya upofu wao, kama watamsikiliza mjumbe huyo, mtumishi huyo wa Bwana.

21 Ninyi ni watu, wenye kuyaona mambo mengi, lakini hamyashiki; wenye kufungua masikio ili kusikia, lakini hamsikii.

22 Bwana hapendezwi na watu wa jinsi hii, lakini kwa sababu ya haki zake ataitukuza sheria na kuiadhimisha.

23 Ninyi ni watu walioibiwa na kutekwa; maadui zenu wote, wamewanasa katika mashimo, nao wamewaficha ninyi katika magereza; wamewachukuwa kwa ajili ya mawindo, na wala hapana aokoaye; maana wamewachukua mateka, na hapana hata mmoja asemaye, Rejesha.