Misaada ya Kujifunza
TJS, Matendo 22


TJS, Matendo 22:29–30. Linganisha na Matendo 22:29–30

Jemadari akamfungua Paulo kamba alizofungwa.

29 Kisha mara moja wale waliokuwa wamhoji waliondoka na kumwacha, na jemadari pia aliogopa baada ya kujua kwamba alikuwa Mrumi, kwa sababu alikuwa amemfunga kamba, na alimfungua kamba alizomfunga.

30 Kesho yake, kwa sababu angeweza kujua kwa uhakika kwa nini alishitakiwa na wayahudi, aliwaamuru makuhani wakuu na baraza lao lote kuhudhuria, na wakamleta Paulo na kumweka mbele yao.