Maandiko Matakatifu
3 Nefi 30


Mlango wa 30

Wayunani wa siku za mwisho wanaamriwa watubu, wamkubali Kristo, na wahesabiwe na nyumba ya Israeli. Karibia mwaka 34–35 B.K.

1 Sikizeni, Ee ninyi Wayunani, na msikie maneno ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu anayeishi, ambaye aameniamuru kwamba nisizungumze kuwahusu kwani tazama, ameniamuru kwamba niandike nikisema:

2 Geukeni ninyi aWayunani wote, kutoka kwenye njia zenu za uovu; na bmtubu kutoka matendo yenu maovu, kutoka kwa uwongo wenu na udanganyifu, na ukahaba wenu, na makundi yenu ya machukizo na ya siri, na sanamu zenu, na mauaji yenu, na ukuhani wa uongo, na wivu wenu, na mashindano yenu ya machukizo ya siri, na kutokana kwa uovu wenu na maovu, na mje kwangu, na mpate kubatizwa kwa jina langu, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, na mjazwe na Roho Mtakatifu, ili cmhesabiwe na watu wangu ambao ni wa nyumba ya Israeli.