EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 25: Kurejelea


“Somo la 25: Kurejelea,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 25,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

wavulana wana tabasamu

Lesson 25

Review

Shabaha: Nitarejelea EnglishConnect 2 na kutafakari juu ya uzoefu wangu.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Learn by Study and by Faith

Jifunze Kwa Kusoma na Kwa Imani

I can rely on God to seek learning by study and by faith.

Ninaweza kumtegemea Mungu ili kutafuta kujifunza kwa kusoma na kwa imani.

Bwana ametupatia mpangilio wa kujifunza:

“Tafuteni kwa bidii na kufundishana maneno ya hekima; ndiyo, tafuteni kutoka kwenye vitabu vizuri maneno ya hekima, tafuteni maarifa hata kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118).

Tafakari juu ya uzoefu wako katika EnglishConnect. Je, umetumiaje mpangilio huu? Tafakari juu ya kanuni za kujifunza na kauli tulizojifunza pamoja.

  • “Wewe ni mtoto wa Mungu”—Mimi ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano na kusudi la milele.

  • “Kutumia imani katika Yesu Kristo”—Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoweka imani katika Yeye.

  • “Wajibika”—Nina uwezo wa kuchagua, na ninawajibika kwa ajili ya kujifunza kwangu mwenyewe.

  • “Pendaneni na fundishaneni”—Ninaweza kujifunza kutoka kwa Roho ninapowapenda, kuwafundisha na kujifunza pamoja na wengine.

  • “Songa mbele”—Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ninapokabiliana na vikwazo.

  • “Shauriana na Bwana”—Ninaweza kuboresha kujifunza kwangu kwa kushauriana na Mungu kila siku kuhusu juhudi zangu.

Wakati wako pamoja na EnglishConnect kinaweza kuwa kinaisha, lakini kuna mambo mengi zaidi Mungu anayokutaka ujifunze na uyapitie. Baba yako wa Mbinguni anakupenda na anataka kukubariki ufikie uwezekano wako wa kiungu. Una weza kumtegemea Mungu na kuendelea “kutafuta kujifunza kwa kusoma na kwa imani.”

mwanaume na mwanamke wakitabasamu

Ponder

  • Ni kwa jinsi gani wewe umepata uzoefu wa upendo wa Mungu na msaada katika kujifunza Kiingereza?

  • Ni kwa jinsi gani umetumia kanuni za kujifunza katika EnglishConnect?

  • Ni kwa jinsi gani utatumia kanuni za kujifunza katika maeneo mengine ya maisha yako?

ikoni b
Prepare for Activity 1

Soma maelekezo ya shughuli ya 1. Andika maswali matatu na majibu yake kuhusu shughuli hilo. Yasome kwa sauti. Ona somo la 4 na somo la 5 kwa msamiati na mipangilio.

ikoni c
Prepare for Activity 2

Soma maelekezo ya shughuli ya 2. Chagua picha moja. Andika maswali manne na majibu kuhusu lile tukio. Yasome kwa sauti. Ona somo la 12 na somo 23 kwa msamiati na mipangilio.

ikoni d
Prepare for Activity 3

Soma maelekezo ya shughuli ya 3 sehemu ya 1. Andika maswali matatu na majibu yake ili kupanga tukio. Yasome kwa sauti. Ona somo la 17 na somo la 22 kwa msamiati na mipangilio.

Rudia Shughuli ya 3 sehemu ya 2.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Learn by Study and by Faith

(20–30 minutes)

mwanaume na mwanamke wakitabasamu

ikoni ya 1
Activity 1: Create Your Own Conversations

(10–15 minutes)

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila familia. Sema mara nyingi uwezavyo. Kuwa mbunifu! Fanyeni zamu.

Example

Picha ya familia ya vizazi vingi kwenye kochi
  • A: How many grandchildren does he have?

  • B: He has two grandchildren.

  • A: Tell me about his daughter-in-law.

  • B: She is thirty years old, short, intelligent, and thoughtful.

  • A: How are the grandfather and the grandmother different?

  • B: The grandfather is more generous than the grandmother.

  • A: How are this sister and that sister different?

  • B: This sister is older. That sister is younger.

Image 1

picha ya familia ya mama na mwana

Image 2

picha ya familia ya watu tisa

Image 3

familia wakizungumza sebuleni

Image 4

Babu na bibi na wajukuu wakiwa nje

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Conversations

(10–15 minutes)

Fanya Igizo. Mwenza B alihudhuria tukio katika picha. Mwenza A anauliza maswali kuhusu tukio. Sema mengi kadiri uwezavyo. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

Example

marafiki wakifurahia tafrija na kusherehekea
  • A: Where were you last night?

  • B: I was at a birthday party.

  • A: How was the birthday party?

  • B: It was fun. I had a wonderful time. There were lots of gifts.

  • A: What did you do?

  • B: We listened to music, danced, and shared memories.

  • A: Was there cake at the birthday party?

  • B: Yes, there was cake!

Image 1

wakina dada wakicheka na wakila mlo wa jioni

Image 2

baba akiwasaidia watoto kuweka tayari mishipi ya kuvulia samaki

Image 3

wanandoa wakiwa harusini

Image 4

familia ikijenga kasri mchangani

ikoni 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(10–15 minutes)

Part 1

Fanya Igizo. Mwenza B anapanga tukio katika jumuiya yenu. Mwenza A anauliza maswali ili kusaidia kupanga tukio hilo. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

Example
Kusherehekea kurushwa kwa baruti
  • A: What will we do?

  • B: We will have a celebration.

  • A: OK! What will happen at the celebration?

  • B: It will be a celebration of our city. There will be games, snacks, a band, and fireworks.

  • A: Who will be there?

  • B: People from our community.

  • A: What day will it be?

  • B: It will be on August 1st.

  • A: When is it going to be?

  • B: It’s going to start at 6:30 p.m. It’s going to end after midnight.

Part 2

Fanya Igizo. Mwenza A anamwalika mwenza B kwenye tukio ulilopanga katika sehemu ya 1 Uliza na jibu maswali ya ziada. Mwenza B hawezi kuhudhuria. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

Example
  • A: Do you want to come to a celebration with me?

  • B: When is it?

  • A: It’s on Friday, May 10th at 6:30 p.m.

  • B: What will happen at the celebration?

  • A: There will be fireworks and games.

  • B: Sorry, I can’t come to the celebration because I need to study for a test.

  • A: Can you please come to the celebration with me?

  • B: No, I can’t come because I have to get a good grade on my test.

Reflection

(5–10 minutes)

Hongera! Umetoka mbali. Tunajivunia juhudi zako zote na muda uliotumia katika kujifunza Kiingereza.

Tafakari juu ya uzoefu wako katika EnglishConnect 2 na uweke malengo ya siku zijazo.

  • Shiriki mambo matatu uliyojifunza ambayo yalikuwa yenye msaada zaidi kwako.

  • Ni kwa jinsi gani utaendelea kuboresha Kiingereza chako?

  • Fikiria kuhusu kanuni za kujifunza. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia kanuni hizi katika maisha yako?

Hatua Yako Inayofuata

Sasa kwamba umekamilisha EnglishConnect 2, fikiria kuendelea na English Connect 3. Ili kujifunza zaidi, tembelea join.englishconnect.org.

Je, hauko tayari kuanza EnglishConnect 3? Endelea kujifunza Kiingereza katika EnglishConnect 2.

Chochote utakachofanya baada ya hapa, kumbuka kwamba wewe ni mtoto wa Mungu na Yeye anaweza kukusaidia kuendelea.

Act in Faith to Practice English Daily

“Pata elimu yote ambayo unaweza. … Elimu ni ufunguo ambao utafungua mlango wa mafanikio kwako. Ni thamani kujitoa ili kuipata. Inastahili kuifanyia kazi, na kama mnaelimisha akili zenu na mikono yenu, mtaweza kuleta mchango mkubwa kwa jamii ambayo wewe ni sehemu yake, na utaweza kutazama nyuma kwa heshima kwa Kanisa ambalo wewe ni muumini” (Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley [2016], 241).