EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 24: Malengo na Ndoto


“Somo la 24: Malengo na Ndoto,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 24,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

msichana akitabasamu akiwa katika benchi

Lesson 24

Goals and Dreams

Shabaha: Nitajfunza kuelezea mipango ya baadaye na malengo.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Press Forward

Songa Mbele

With God’s help, I can press forward even when I face obstacles.

Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ninapokabiliana na vikwazo.

Nabii Lehi katika Kitabu cha Mormoni aliota ndoto ambayo inatufundisha jinsi ya kusonga mbele. Aliona watu wengi wakitembea katika njia kwenda kwenye mti mzuri ulio na tunda tamu. Tunda hili lilikuwa ni upendo wa Mungu. Safari yao katika njia hii ilikuwa ngumu kwa sababu “ukungu wa giza” ulificha njia hii (1 Nefi 8:23). Kwa bahati nzuri, kulikuwa na “fimbo ya chuma” wangeweza kushikilia ili kubaki katika njia ile (1 Nefi 8:24). Fimbo ya chuma ni neno la Mungu, ikijumuisha maandiko. Hapa kuna kile Lehi alichosema kuhusu safari yao.

“Wakasonga mbele, daima wameshikilia ile fimbo ya chuma, hadi wakafika … na kula matunda ya ule mti” (1 Nefi 8:30).

Watu walifika kwenye ule mti kwa sababu waliendelea kushikilia fimbo ya chuma na kuendelea kutembea kwenda mbele, wakimtumainia Mungu. Hawakuvutwa mawazo au kukata tamaa wakati giza lilipokuja. Wewe unafanya bidii ya kujifunza Kiingereza. Wakati mwingine unachoka na hauhisi kujifunza. Wakati mwingine kuna mambo mengine yanahitaji usikivu wako na muda wako. Umepata njia za kujifunza hata hivyo. Usiache sasa. Unaweza kuendelea kupata elimu unaposonga mbele ukiwa na tumaini katika Mungu.

watu wameshikilia fimbo ya chuma

Ponder

  • Ni nini kilicho “ukungu wa giza” kwako katika kujifunza Kiingereza?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kusonga mbele hata wakati ambapo kujifunza ni vigumu?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo.

I hope to …

Ninatumaini ku …

I plan to …

Ninapanga ku …

I want to …

Ninataka ku …

I would like to …

“Ningependa ku …

After I …

Baada ya …

When I …

Nitakapo …

Nouns

goal/goals

lengo/malengo

plan/plans

mpango/mipango

Verbs

become a teacher

kuwa mwalimu

buy a house

nunua nyumba

finish school

maliza shule

get a job

pata kazi

get married

oa/olewa

go to college

nenda chuo

move to New York City

hamia Jiji la New York

retire

staafu

save money

weka akiba ya fedha

study chemistry

soma kemia

travel

safiri

Times

in the future

katika siku za usoni

next year

mwakaujao

three years from now

miaka mitatu kutoka sasa

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: What are your future (noun)?A: I hope to (verb).

Questions

swali la mpangilio wa 1 ni nini nomino zako zijazo

Answers

jibu la mpangilio wa 1 mimi natumaini kitenzi

Examples

Q: What are your future goals?A: I hope to finish school.

mwalimu na mtoto

Q: What are your future plans?A: I want to move to another country and become a teacher.

Q: What do you plan to do next year?A: I plan to go to college and study chemistry.

Q: What do you plan to do three years from now?A: I would like to get a good job and save money.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutambua mipangilio hii wakati wa mazoezi yako ya kila siku.

Q: What do you plan to do when you (verb)?A: When I (verb), I plan to (verb).

Questions

swali la mpangilio wa 2 unapanga kufanya nini wakati unakitenzi

Answers

jibu la mpangilio wa 2 wakati nia kitenzi, nina kitenzi

Examples

mwanaume akitumia kompyuta

Q: What do you plan to do when you finish school?A: When I finish school, I plan to get a job.

sanduku la nguo uwanja wa ndege

Q: What do you plan to do after you retire?A: After I retire, I would like to travel.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Press Forward

(20–30 minutes)

watu wakishikilia fimbo ya chuma

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2.

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Fanya Igizo. Mwenza B ni mtu aliye katika picha. Mwenza B anauliza maswali kuhusu mipanga ya mtu kwa siku za usoni. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

Example

mwanamke ameshikilia stetoskopu
  • A: What are your future goals?

  • B: I hope to finish school.

  • A: What do you plan to do after you finish school?

  • B: After I finish school, I plan to become a doctor.

  • A: What do you plan to do when you become a doctor?

  • B: When I become a doctor, I would like to travel.

Image 1

mvulana kijana akizungusha mpira wa basketi kwa kidole

Image 2

mwalimu na mtoto

Image 3

wanandoa wakikaa mkao wa picha

Image 4

Wanandoa wazee anatembea nje

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Uliza na ujibu maswali kuhusu kile unachotaka, tumaini, na kupanga kufanya siku za usoni. Zungumzeni mwaka mmoja kutoka sasa, miaka mitano kutoka sasa, na miaka kumi kutoka sasa. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.

New Vocabulary

have children

kuwa na watoto

in one year

ndani ya mwaka mmoja

one year from now

mwakammoja kutoka sasa

work for a company

Fanya kazi ya kampuni

Example

  • A: What do you hope to do in one year?

  • B: I hope to work for a good company and get married.

  • A: What do you want to do ten years from now?

  • B: In ten years, I would like to have children. I also want to buy a house.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Ask about others’ goals and plans for the future.

    Uliza kuhusu malengo na mipango ya watu wengine kwa siku za usoni.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Talk about my goals and plans for the future.

    Zungumza kuhusu malengo na mipango yangu mimi kwa siku za usoni.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri Msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Kuweka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Akina kaka na akina dada, katika Kanisa hili, tunaamini katika uwezekano wa kiungu wa watoto wote wa Mungu na katika uwezo wetu wa kuwa kitu zaidi katika Kristo. Kwa wakati wa Bwana, siyo mahali gani tunapoanzia, bali ni wapi tunaelekea ndiyo muhimu zaidi” (Clark G. Gilbert, “Kuwa Zaidi katika Kristo: Mfano wa Mteremko,” Liahona, Nov. 2021, 19).