Mkutano Mkuu
Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2021
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2021

Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Ndugu Wapendwa: Tukiongozwa na ufunuo uliorekodiwa katika sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Mpangilio wa Zaka—linalojumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi—huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Idara za Kanisa hutoa fedha kwa mujibu wa bajeti, sera, na taratibu zilizoidhinishwa.

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, inayojumuisha wataalamu walioidhinishwa na iliyo huru kutoka kwenye idara zingine zote za Kanisa na vitengo, ina wajibu wa kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na ulinzi wa mali za Kanisa.

Kwa mujibu wa ukaguzi uliofanywa, Idara ya Ukaguzi ya Kanisa inatoa msimamo kwamba, katika nyanja zote, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na mali za Kanisa kwa mwaka 2021 vimerekodiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa bajeti ya Kanisa, sera, na utendaji wa kiuhasibu ulioidhinishwa. Kanisa linafuata utendaji uliofundishwa kwa waumini wake wa kuishi ndani ya bajeti, kuepuka madeni, na kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa uhitaji.

Kwa heshima imewasilishwa,

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa

Jared B. Larson

Mkurugenzi Mtendaji