Mkutano Mkuu
Amefufuka na Uponyaji katika Mbawa Zake: Tunaweza Kuwa Zaidi ya Washindi
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


“Amefufuka na Uponyaji katika Mbawa Zake”

Tunaweza Kuwa Zaidi ya Washindi

Yesu alishinda unyanyasaji wa ulimwengu huu ili kuwapa nguvu sio tu kunusurika, lakini siku moja, kumpitia Yeye, kushinda na hata kuwa washindi.

Marin, Mimi ni Mzee Holland, na mambo yanakaribia kuharibika.

Sisi Ni Zaidi ya Washindi

Sisi sote tunavutiwa sana na hadithi za kunusurika. Tunasikia simulizi za wavumbuzi jasiri na watu wa kawaida pia ambao wanajaribu kuwa hai dhidi ya ugumu na matarajio, na hatuwezi kusaidia bali kujiuliza wenyewe, “Ningeweza kufanya hilo?

Ninafikiria mara moja juu ya Mvumbuzi Miingereza Ernest Shackleton na kundi la meli yake HMS Endurance, iliyoangamia baharini katika barafu ya Antarctic na kisha kukwama kwenye kisiwa kame kwa karibuni miaka miwili. Uongozi wa ajabu wa Shackleton na azma ya nguvu kabisa iliokoa maisha ya watu hawa, licha ya hali ngumu.

Kisha ninafikiria kundi la Apollo 13 likiruka angani likielekea mwezini! Lakini maafa yakatokea wakati tangi la oksijeni lilipuka, na safari kutibuka. Ukosefu wa oksijeni, kundi na wasimamizi wa safari walifanya ufaraguzi na kuwarudisha wanaanga wote watatu salama duniani.

Ninashangazwa na kunusurika kwa ajabu kwa watu na familia walioumizwa na vita, wakafungwa katika kambi, na wakawa wakimbizi, ambao kishujaa na kwa ujasiri wanaweka hai miale ya tumaini kwa ajili ya waathiriwa wenzao, ambao hufanya wema kukabiliana na ukatili, na ambao kwa njia fulani wanawasaidia wengine kuvumilia tu siku moja zaidi.

Ungenusurika au ningenusurika katika hali moja yoyote ya hizi hali ngumu sana?

Pengine baadhi yenu, hata hivyo, fikiria matukio ya manusura na nafsi yako inalia kwamba wewe u hadithi hai ya kunusurika sasa hivi kama mhanga wa unyanyasaji, kutelekezwa, kuonewa, vurugu za kijamii, au kuteseka kwa aina yoyote. Uko katikati ya jaribio lako la kukata tamaa la kuishi katika hali ambayo inahisi kama ajali mbaya ya meli au misheni ya kuahidi iliyoghairishwa ghafla. Je, utawahi kuokolewa; utafanikiwa kupitia hadithi yako mwenyewe ya kuishi?

Jibu ni ndiyo. Mnaweza kunusurika. Kwa kweli tayari mmeokolewa; tayari mmeshaokolewa—na Mmoja ambaye ameshateseka mateso hayo hayo ambayo mnateseka na kuvumilia maumivu makubwa mnayoteseka.1 Yesu alishinda unyanyasaji wa ulimwengu huu2 ili kuwapa nguvu sio tu kunusurika lakini siku moja, kumpitia Yeye, kushinda na hata kushinda—kusimama kabisa juu ya maumivu, taabu, mahangaiko, na kuyaona kubadilishwa na amani.

Mtume Paulo aliuliza:

“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? …

“Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.”3

Ahadi kwa Agano la Israeli

Unakumbuka wakati Rais Russell M. Nelson alitoa mwaliko ufuatao katika mkutano mkuu. Alisema: “Unapojifunza maandiko yako … , ninakuhimiza kuandika orodha ya yale yote Bwana aliyoahidi Atayafanya kwa Israeli ya agano. Ninafikiri utashangazwa!”4

Hapa kuna tu ahadi chache za nguvu na za kufariji familia yangu ilipata. Fikiria Bwana akisema maneno haya kwako—kwa ninyi ambao mnahangaika—kwa sababu ni kwa ajili yenu:

Usiogope.5

Nayajua maumivu yao, nami nimeshuka ili niwaokoe.6

Sitakuacha.7

Jina langu liko juu yao, na malaika zangu wawalinde.8

Nitatenda mambo ya ajabu kati yenu.9

Tembea pamoja nami, nitegemee mimi, nami nitawapumzisha.10

Niko katikati yako.11

Wewe ni wangu.12

Kwa Wale Ambao Wanahangaika

Ukiwa na uhakikisho akilini mwako, ninataka kuongea moja kwa moja na wale ambao wanahisi kama vile hakuna njia yoyote ya kujinasua kutoka kwenye hadithi yao ya kunusurika kwa sababu ya kiwewe kinacholetwa na matendo ya ukatili ya wengine. Kama hii ndiyo hadithi yako ya kunusurika, tunalia pamoja nawe. Tunatamani wewe ushinde mkanganyiko, aibu, na hofu, na tunatamani wewe kupitia Yesu Kristo, ushinde.

Kutoka Mhanga, hadi Manusura hadi Mshindi

Kama umepitia aina yoyote ya unyanyasaji, vurugu, au mateso, unaweza kubakia na wazo ambalo matukio haya kwa namna fulani yakuwa makosa yako na kwamba wewe unafaa kubeba aibu na hatia unayohisi. Unaweza kuwa ulipata mawazo kama haya:

  • Ningezuia hilo.

  • Mungu hanipendi kabisa.

  • Hakuna yeyote atakaye nipenda.

  • Nimeharibika kupindukia.

  • Upatanisho wa Mwokozi ni kwa wengine bali si kwangu.

Haya mawazo na hisia zenye dosari zinaweza kuwa zimekuwa kikwazo cha kutafuta msaada kutoka kwa familia, marafiki, viongozi, au wataalamu, kwa hiyo unahangaika peke yako. Kama ukitafuta msaada kutoka kwa wale unaowaamini, bado unaweza kusumbuliwa na mawazo ya aibu na hata kujichukia. Athari za matukio haya zinaweza kubakia kwa miaka mingi. Unatumainia kwamba siku moja utahisi vyema, lakini kwa namna fulani siku haitafika.

Unyanyasaji haujakuwa, wala si, na kamwe hautakuwa makosa yako, bila kujali kile mnyanyasaji au yeyote mwingine anaweza kuwa alisema kinyume. Wakati umeshakuwa mhanga wa ukatili, kujamiana kwa maharimu, au ukaidi mwingine, sio wewe unahitaji kutubu; wewe hauwajibiki.

Wewe si kwamba haustahili au si bure au haupendwi kidogo kama wanadamu, au binti au mwana wa Mungu, kwa sababu ya kile mtu mwingine amekufanyia.

Mungu sasa hakuoni, wala Yeye ashakuona, wewe kama wa kudharauliwa. Chochote kilichokutokea, Yeye hajaaibishwa nawe au hajavunjwa moyo nawe. Yeye anakupenda katika njia bado haujaigudua. Na wewe utaigudua unapomtumaini katika ahadi Zake na unapojifunza kumwamini Yeye wakati Yeye anaposema wewe ni wa “thamani katika macho [Yake].”13

Wewe hautambuliwa kwa haya mambo mabaya ambayo umetendewa. Wewe, katika ukweli mtukufu, unatambuliwa kwa utambulisho wako uliopo wa milele kama mwana au binti ya Mungu, kwa upendo kamili , usio na mwisho wa Muumba wako na mwaliko kwa uponyaji mzima na kamili.

Ingawa inaweza kuonekana kuwa haiwezekani, kujisikia haiwezekani, uponyaji unaweza kuja kupitia muujiza wa ukombozi mkuu wa Upatanisho wa Yesu Kristo ambaye alifufuka na “uponyaji katika mabawa yake.”14

Mwokozi wetu mwenye rehema, mshindi juu ya giza na upotovu, ana uwezo wa kusawazisha makosa yote, ukweli wa kuleta uzima kwa wale waliokosewa na wengine.15

Tafadhali kumbuka kwamba Mwokozi alijishusha chini ya vitu vyote, hata kile kilichokutokea. Kwa sababu ya hilo, Yeye anajua hasa vile hofu kuu na aibu uhisika na jinsi inahisika kutelekezwa na kuvunjwa.16 Kutoka kina cha kuteseka Kwake kwa upatanisho, Mwokozi hukupatia tumaini ambalo ulifikiria umepoteza milele, nguvu ambayo uliamini kamwe haungeweza kuipata, na uponyaji ambao usingeweza kufikira unawezekana.

Tabia ya Unyanyasaji Inashutumiwa kwa Uwazi na Bwana na Manabii Wake

Unyanyasaji wa aina yoyote haukubaliwi kabisa—kimwili, kijinsia, kimhemko, au kimaneno—katika nyumba yoyote, nchi yoyote, au tamaduni yoyote. Hakuna chochote mke, mtoto au mme anaweza kufanya au kusema huwafanya “wapaswe” kupigwa. Hakuna mtu, katika nchi au tamaduni yoyote, anayewahi “kuomba” uchokozi au jeuri kutoka kwa mtu mwingine mwenye mamlaka au na mtu mkubwa zaidi na mwenye nguvu zaidi.

Wale ambao wananyanyasa na wanajaribu kuficha dhambi zao nzito wanaweza kufanya hivyo kwa muda. Lakini Bwana, ambaye huona yote anajua vitendo na mawazo na nia ya moyo.17 Yeye ni Mungu wa haki, na haki Yake takatifu itatolewa.18

Kimiujiza, Bwana pia ni Mungu wa rehema kwa wale wanaotubu kwa kweli. Wanyanyasaji—ikijumuisha wale ambao wakati mmoja wao wenyewe walinyanyaswa—wale wanakiri, na kuacha dhambi zao, na kufanya yote yaliyo katika uwezo wao kufidia na kufanya malipizo, wanapata msamaha kupitia Upatanisho wa Kristo.

Kwa wale waliotuhumiwa kimakosa, uzito usioweza kusemeka wa tuhuma hizi huleta utakaso wake. Lakini wao pia wanabarikiwa na mateso ya Mwokozi kwa niaba yao na elimu kwamba hatimaye ukweli utashinda.

Wanyanyasaji wasiotubu watasimama mbele ya Bwana kuwajibika kwa ajili jinai yao.

Bwana Mwenyewe alisema wazi kabisa katika kushutumu unyanyasaji wa aina hii: “Bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa … yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.”19

Hitimisho

Marafiki wapendwa ambao mmeumizwa vibaya—na kwa ajili hiyo, mtu yeyote ambaye amepatwa na kukosa haki maishani—mnaweza kuwa na mwanzo mpya na kuanza upya. Katika Gethsemane na Kalivari, Yesu “alijuchukulia juu Yake … maumivu na masumbuko yote tuliyowahi wakati wowote kupata wewe na mimi,”20 na Yeye ameshinda yote! Kwa mikono iliyonyoshwa, Mwokozi anatoa kipawa cha uponyaji kwenu. Kwa ujasiri, subira, na fokasi ya uaminifu juu Yake, kabla ya muda mrefu mnaweza kuja kukubali kikamilifu kipawa hiki. Mnaweza kuacha maumivu yenu na kuyaacha miguuni pa Bwana.

Mwokozi wenu mpole alitangaza, “Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu: mimi nalikuja ili [ninyi] muwe na uzima, kisha [muwe] nao tele.”21 Wewe ni manusura, unaweza kupona, na unaweza kuamini kwamba kwa nguvu na neema ya Yesu Kristo, unaweza kushinda.

Yesu hubobea katika kinachonekana kutowezekana. Yeye alikuja hapa kufanya kisichowezakana kuwezekana, kisichokomboleka kukomboleka, kuponya kisichopenyeka, kusawazisha kisichosawazishika, kuahidi kisichoahidika.22 Na Yeye hasa ni mzuri katika haya. Hakika, Yeye ni bora katika haya. Katika jina la Yesu Kristo, Mponyaji wetu, amina.

Kwa habari zaidi na nyenzo, ona “Abuse” Help, Healing, and Protection at ChurchofJesusChrist.org and in the Gospel Library app