Mkutano Mkuu
Asili Yako ya Kiungu na Kudura ya Milele
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Asili Yako ya Kiungu na Takdiri ya Milele

Ninakualikeni kuyakita maisha yenu kwa Yesu Kristo na kukumbuka kweli za msingi katika Dhima ya Wasichana.

Akina dada wapendwa, asanteni kwa kuwa hapa. Ni heshima kwangu kushiriki kwenye kikao hiki cha wanawake cha mkutano mkuu. Wakati fulani pia nimepata fursa ya kuhudhuria madarasa ya Wasichana. Lakini acha niseme yaliyo dhahiri—mimi si mdogo, na wala mimi si mwanamke! Nilijifunza, hata hivyo, kwamba nahisi kutokuwa sehemu yao kama ninaweza kukariri Dhima ya Wasichana nikiwa pamoja na wasichana. Mafundisho ya kuvutia yanayofundishwa katika Dhima ya Wasichana1 ni muhimu kwa wasichana, lakini yanatumika kwa wote, ikiwa ni pamoja na sisi ambao si wasichana.

Dhima ya Wasichana huanza, “Mimi ni binti mpendwa wa wazazi wa mbinguni, mwenye asili ya kiungu na kudura ya milele.”2 Kauli hii ina kweli nne muhimu. Kwanza,wewe ni binti mpendwa. Hakuna unachofanya—au usichofanya—kinachoweza kubadilisha hilo. Mungu anakupenda kwa sababu wewe ni binti Yake wa kiroho. Wakati mwingine tunaweza tusihisi upendo Wake, lakini daima upo. Upendo wa Mungu ni mkamilifu.3 Uwezo wetu wa kuhisi upendo huo sio mkamilifu.

Roho ana jukumu muhimu katika kuwasilisha upendo wa Mungu kwetu.4 Walakini, ushawishi wa Roho Mtakatifu unaweza kufichwa na “hisia kali, kama vile hasira, chuki, … [au] woga … kama kujaribu kuonja ladha tamu ya zabibu huku unakula pilipili ya jalapeno. … [Ile ladha moja] kabisa inashinda ile nyingine.”5 Vivyo hivyo, tabia zinazotuweka mbali na Roho Mtakatifu, ikijumuisha dhambi,6 hufanya iwe vigumu kutambua upendo wa Mungu kwetu.

Pia, hisia zetu za upendo wa Mungu zinaweza kufanywa kuwa butu na hali ngumu na magonjwa ya kimwili au kiakili, kati ya mambo mengine. Katika visa hivi vyote, ushauri wa viongozi wanaoaminika au wataalamu mara nyingi unaweza kuwa wa manufaa. Tunaweza pia kujaribu kuboresha upokeaji wetu wa upendo wa Mungu kwa kujiuliza, “Je, upendo wangu kwa Mungu ni wa kudumu au ninampenda ninapokuwa na siku nzuri lakini si sana ninapokuwa na siku mbaya?”

Ukweli wa pili ni kwamba tuna wazazi wa mbinguni, baba na mama.7 Mafundisho ya Mama wa Mbinguni huja kwa ufunuo na ni imani ya kipekee miongoni mwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Rais Dallin H. Oaks alieleza umuhimu wa ukweli huu: “Theolojia yetu huanza na wazazi wa mbinguni. Matarajio yetu ya juu ni kuwa kama wao.”8

Ni machache sana yamefunuliwa kuhusu Mama wa Mbinguni, lakini tunachojua kimefupishwa mada ya injili inayopatikana kwenye programu yetu ya Maktaba ya Injili.9 Mara tu ukisoma kile kilichopo hapo, utajua kila kitu ninachojua kuhusu somo hilo. Natamani ningejua zaidi. Ninyi pia bado mnaweza kuwa na maswali na kutaka kupata majibu zaidi. Kutafuta uelewa zaidi ni sehemu muhimu ya ukuaji wetu kiroho, lakini tafadhali kuwa makini. Kutafuta uelewa hakuwezi kuondoa ufunuo.

Kubahatisha hakutapelekea uelewa mkubwa wa kiroho, lakini itapelekea kwenye udanganyifu au kugeuza mwelekeo wetu kutoka kwa kile kilichofunuliwa.10 Kwa mfano, Mwokozi aliwafundishwa Wafuasi Wake, “Ninyi lazima msali daima kwa Baba kwa jina langu.”11 Tunafuata mtindo huu na kuelekeza kuabudu kwetu kwa Baba yetu wa Mbinguni katika jina la Yesu Kristo na hatusali kwa Mama wa Mbinguni.12

Tangu Mungu alipowateua manabii, wamepewa mamlaka ya kusema kwa niaba Yake. Lakini hawatamki mafundisho yaliyotungwa “kwa akili [zao] wenyewe”13 au kufundisha kile ambacho hakijafunuliwa. Fikiria maneno ya nabii wa Agano la Kale Balaamu, ambaye alipewa rushwa ili kuwalaani Waisraeli ili kuifaidisha Moabu. Balaamu alisema, “ Hata kama [mfalme wa Moabu] angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la Bwana, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.”14 Manabii wa siku za mwisho vivyo hivyo wamebanwa. Kudai ufunuo kutoka kwa Mungu ni kiburi na hakutozaa matunda. Badala yake, tunamngojea Bwana na ratiba Yake ili kufunua kweli Zake kupitia njia ambazo Ameziweka.15

Ukweli wa tatu katika aya ya ufunguzi wa Dhima ya Wasichana ni kwamba tuna “asili ya kiungu.” Hii ndiyo asili ya sisi ni nani. Ni “nasaba,” ya kiroho iliyorithiwa kutoka kwa wazazi wetu wa mbinguni,16 na haihitaji juhudi yoyote kwa upande wetu. Huu ni utambulisho wetu wa muhimu zaidi, bila kujali jinsi tunavyochagua kujitambulisha. Kuelewa ukweli huu wa kina ni muhimu kwa kila mtu lakini hasa kwa watu binafsi walio katika makundi ambao wametengwa kihistoria, kukandamizwa, au kutiishwa. Kumbuka kwamba utambulisho wako wa muhimu sana unahusiana na asili yako ya kiungu kama mtoto wa Mungu.

Ukweli wa nne ni kwamba tuna “kudura ya milele.” Kudura hiyo haitalazimishwa kwetu. Baada ya kifo, tutapokea kile ambacho tumestahili na “kufurahia [tu] kile ambacho [sisi] tuko tayari kupokea”17. Kutambua kudra yetu ya milele inategemea na chaguzi zetu. Inahitaji kufanya na kuweka maagano matakatifu. Njia hii ya agano ndiyo njia ya kusonga kwa Kristo na inategemea na ukweli halisi na sheria ya milele, isiyobadilika. Hatuwezi kuunda njia yetu wenyewe na kutarajia matokeo yaliyoahidiwa na Mungu. Kutarajia baraka Zake bila kufuata sheria za milele ambazo kwazo baraka hutoka18 ni upotofu, kama kufikiri tunaweza kugusa jiko la moto na “kuamua” kutochomwa.

Mnaweza kujua kwamba nilikuwa natibu wagonjwa wenye matatizo ya moyo. Matokeo yao bora yalipatikana kwa kufuata mipango ya matibabu iliyowekwa, iliyothibitika. Licha ya kujua hili, baadhi ya wagonjwa walijaribu kujadili mpango tofauti wa matibabu. Walisema, “Sitaki kutumia dawa nyingi” au “Sitaki kufanyiwa vipimo vingi vya ufuatiliaji.” Bila shaka, wagonjwa walikuwa huru kufanya maamuzi yao wenyewe, lakini ikiwa wangeacha mipango bora ya matibabu, matokeo yao yalidorora. Wagonjwa wenye matatizo ya moyo hawawezi kuchagua mpango duni na kisha kulaumu daktari wao wa moyo kwa matokeo duni.

Hilo pia ni kweli kwetu. Njia iliyowekwa na Baba wa Mbinguni inaongoza kwenye matokeo bora ya milele. Tuko huru kuchagua, lakini hatuwezi kuchagua matokeo ya kutofuata njia iliyofunuliwa.19 Bwana Amesema, “Kile kivunjacho sheria, na hakiishi kwa sheria, lakini chatafuta chenyewe kuwa sheria, … hakiwezi kutakaswa kwa sheria, si kwa rehema, haki, wala hukumu.”20 Hatuwezi kupotoka kutoka kwenye njia ya Baba wa Mbinguni na kisha kumlaumu kwa matokeo duni.

Aya ya pili katika Dhima ya Wasichana inasomeka: “Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninajitahidi kuwa kama Yeye Alivyo. Ninatafuta na kufanyia kazi ufunuo binafsi na kuwatumikia wengine katika jina Lake takatifu.” Tunaweza kukuza ushuhuda wa Yesu Kristo kwa kutenda kwa imani.21 Tunaweza kudai karama ya kiroho ili “kujua kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, na kwamba alisulibiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.” Au tunaweza kupokea karama ya kuamini maneno ya wale wanaojua,22 mpaka nasi tujue wenyewe. Tunaweza kufuata mafundisho ya Mwokozi na kuwasaidia wengine kusonga Kwake. Kwa njia hii, tunaungana Naye katika kazi Yake.23

Dhima ya Wasichana inaendelea, “Nitasimama kama shahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote na katika mahali kote.” Washiriki wote wa Kanisa wanahitajika kama mashahidi wa Mungu,24 ingawa Mitume na wa Sabini wametumwa kama mashahidi maalum wa jina la Kristo.25 Hebu fikiria mechi ya mpira wa miguu ambapo kipa pekee ndiye hulinda lango. Bila msaada wa wachezaji wengine wa timu, kipa hataweza kulinda lango vya kutosha na timu itapoteza kila wakati. Vivyo hivyo, kila mtu anahitajika kwenye timu ya Bwana.26

Aya ya mwisho ya Dhima ya Wasichana inaanza, “Ninapojitahidi kustahili kwa ajili ya kuinuliwa, ninathamini zawadi ya toba na kutafuta kuwa bora kila siku.” Kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi, tunaweza kutubu, kujifunza kutokana na makosa yetu na kutohukumiwa kwayo. Rais Russell M. Nelson alifundisha “Watu wengi sana wanafikiria toba kama adhabu. … Lakini hisia hii ya kuwa unaadhibiwa inazalishwa na Shetani. Yeye hujaribu kutuzuia kutazama kwa Yesu Kristo, ambaye anasimama na mikono iliyonyooshwa, akitumaini na kuwa tayari kutuponya, kutusamehe, kutusafisha, kutuimarisha na kututakasa.”27

Tunapotubu kwa dhati, hakuna kovu la kiroho linalobaki, bila kujali kile tulichofanya, kikubwa kiasi gani au ni mara ngapi tumekirudia.28 Kadiri tunapotubu na kuomba msamaha kwa nia ya dhati, tunaweza kusamehewa.29 Ni karama ya ajabu iliyoje kutoka kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo!30 Roho Mtakatifu anaweza kutuhakikishia kwamba tumesamehewa. Tunapohisi furaha na amani,31 hatia inafagiliwa mbali,32 na hatuteswi tena na dhambi zetu.33

Hata baada ya toba ya dhati, hata hivyo, tunaweza kujikwaa. Kujikwaa hakumaanishi kwamba toba hiyo haikutosha bali inaweza kuonyesha udhaifu wa kibinadamu. Ni faraja iliyoje kujua kwamba “Bwana huona udhaifu kwa njia tofauti kuliko [Anavyoona] uasi.” Hatupaswi kutilia shaka uwezo wa Mwokozi wa kutusaidia kwenye udhaifu wetu, kwa sababu “Bwana anapozungumza juu ya udhaifu, daima ni kwa rehema.”34

Dhima ya Wasichana inahitimisha, “Kwa imani, nitaimarisha nyumba na familia yangu, kufanya na kushika maagano matakatifu, na kupokea ibada na baraka za hekalu takatifu.” Kuimarisha nyumbani na familia kunaweza kumaanisha kutengeneza kiungo cha kwanza katika mlolongo wa uaminifu, kuweka urithi wa imani au kurejesha.35 Kwa vyovyote vile, nguvu huja kupitia kwa imani katika Yesu Kristo na kwa kufanya maagano matakatifu.

Katika hekalu, tunaweza kujifunza sisi ni nani na wapi tumetoka. Mwanafalsafa wa Kirumi Cicero alisema, “Kutokuwa na maarifa ya kile kilichotokea kabla ya kuzaliwa ni kubakia daima kama mtoto.”36 Alikuwa, kwa kweli, anarejelea historia ya kidunia, lakini mtazamo wako mwerevu unaweza kukuzwa. Tunaishi kama watoto daima ikiwa hatujui mtazamo wa milele unaopatikana katika mahekalu. Hapo tunakua katika Bwana, “tunapokea utimilifu wa Roho Mtakatifu,”37 na kujitolea kikamilifu zaidi kama wafuasi wa Mwokozi.38 Tunapoweka maagano yetu, tunapokea nguvu za Mungu katika maisha yetu.39

Ninakualikeni kuyakita maisha yenu kwa Yesu Kristo na kukumbuka kweli za msingi katika Dhima ya Wasichana. Ikiwa uko tayari, Roho Mtakatifu atakuongoza. Baba yetu wa Mbinguni anakutaka uwe mrithi Wake na kupokea yote Aliyonayo.40 Hawezi kukupa zaidi. Hawezi kukuahidi zaidi. Anakupenda zaidi ya unavyojua na anataka uwe na furaha katika maisha haya na maisha yajayo. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.