Misaada ya Kujifunza
TJS, Kutka 33


TJS, Kutoka 33:20, 23. Linganisha na Kutoka 33:20, 23

Hakuna mtu mwenye dhambi anayeweza kuuona uso wa Mungu na akaishi.

20 Na yeye akamwambia Musa, Wewe hutaweza kuuona uso wangu wakati huu, isije hasira yangu ikawaka dhidi yako pia, na nikakuangamiza wewe, na watu wako; kwani hakutakuwa na mtu yeyote miongoni mwao atakayeniona mimi kwa wakati huu, na kuishi, kwa maana wao ni wenye dhambi kupindukia. Na hakuna mtu mwenye dhambi kwa wakati wowote, wala hatakuwa mwenye dhambi yeyote kwa wakati wowote, ambaye atauona uso wangu na kuishi.

23 Nami nitauondoa mkono wangu, nawe utaziona sehemu zangu za nyuma, lakini uso wangu hautaonekana, kama nyakati zingine; kwa maana nimekasirishwa na watu wangu Waisraeli.