Misaada ya Kujifunza
TJS, 1 Petro 4


TJS, 1 Petro 4:6. Linganisha na 1 Petro 4:6

Injili inahubiriwa kwa wale waliokufa.

6 Kwa sababu hii, injili inahubiriwa kwao waliokufa, ili kwamba wahukumiwe sawasawa na wanadamu katika mwili, lakini waishi katika roho sawa sawa na mapenzi ya Mungu.

TJS, 1 Petro 4:8. Linganisha na 1 Petro 4:8

Hisani hutuzuia sisi tusitende dhambi.

8 Zaidi ya yote iwe huruma na juhudi nyingi katika hisani miongoni mwenu; maana hisani huzuia wingi wa dhambi.