Maandiko Matakatifu
Moroni 3


Mlango wa 3

Wazee wanawatawaza makuhani na walimu kwa kuwawekea mikono. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Njia ambayo wanafunzi, ambao waliitwa wazee wa kanisa, waliwatawaza makuhani na walimu—

2 Baada ya wao kuomba kwa Baba katika jina la Kristo, waliwawekea mikono, na kusema:

3 Katika jina la Yesu Kristo ninakutawaza uwe kuhani (au kama atakuwa mwalimu, ninakutawaza uwe mwalimu) kuhubiri toba na msamaha wa dhambi kupitia kwa Yesu Kristo, kwa kuvumilia kwa imani kwa jina lake hadi mwisho. Amina.

4 Na katika njia hii waliwatawaza makuhani na walimu, kulingana na karama na wito wa Mungu kwa watu; na waliwatawaza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ambaye alikuwa ndani yao.