Maandiko
1 Nefi 6
iliyopita inayofuata

Mlango wa 6

Nefi anaandika kuhusu vitu vya Mungu—Kusudi la Nefi ni kushawishi watu kumjia Mungu wa Ibrahimu ili waokolewe. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na sasa mimi, Nefi, sitaandika nasaba ya baba zangu katika sehemu ahii ya maandishi yangu; wala sitaiandika baadaye wakati wowote katika mabamba haya bmabamba ambayo ninaandika; kwani imeandikwa kwenye maandishi ambayo yamewekwa na cbaba yangu; kwa hivyo, sitaiandika katika mabamba haya.

2 Kwani inanitosha kusema kuwa sisi ni kizazi cha aYusufu.

3 Na sio muhimu kwangu kutoa taarifa kamili ya vitu vya baba yangu, kwani haviwezi kuandikwa kwenye mabamba amabamba haya, kwani nahitaji nafasi ya kuandika vitu vya Mungu.

4 Kwani lengo langu kamili ni akuwashawishi watu bwaje kwa Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo ili waokolewe.

5 Kwa hivyo, sitaandika vitu vile ambavyo avinafurahisha ulimwengu, bali nitaandika yale ambayo yanamfurahisha Mungu na wale wasio wa ulimwengu.

6 Kwa hivyo, nitatoa amri kwa uzao wangu, kwamba hawataandika vitu visivyo na thamani kwa watoto wa watu kwenye mabamba haya.