Miito ya Misheni
Sura ya 6: Tafuta Sifa Kama za Kristo


“Sura ya 6: Tafuta Sifa Kama za Kristo,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Sura ya 6,” Hubiri Injili Yangu

Picha
Kuitwa kwa Wavuvi (Kristo Akiwaita Petro na Andrea), na Harry Anderson

Sura ya 6

Tafuta Sifa Kama za Kristo

Zingatia Hili

  • Je, ni kwa jinsi gani kutafuta sifa kama za Kristo kunanisaidia nitimize dhumuni langu kama mmisionari?

  • Je, ni kwa jinsi gani ninaweza kutafuta na kupokea sifa kama za Kristo?

  • Je, ni sifa zipi ninapaswa kufokasi juu yake hivi sasa?

Utangulizi

Mwanzo wa huduma Yake ya duniani, Yesu alitembea kwenye ufuko wa Bahari ya Galilaya na kuwaita wavuvi wawili, Petro na Andrea. “Nifuateni,” Yeye alisema, “nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19; ona pia Marko 1:17).

Bwana pia amekuita wewe katika kazi Yake, na pia anakualika umfuate Yeye. “Mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Yeye aliwauliza. “Amin nawaambia, hata vile nilivyo” (3 Nefi 27:27).

Baadhi ya sura katika Hubiri Injili Yangu zinafokasi juu ya kile unachohitaji kufanya kama mmisionari, kama vile jinsi ya kujifunza, jinsi ya kufundisha, na jinsi ya kuweka malengo. Kama vile ilivyo muhimu kwenye nini unachofanya wewe ni nani na nani unakuwa. Hiyo ndiyo fokasi ya sura hii.

Maandiko yanaelezea sifa kama za Kristo ambazo ni muhimu kwa ajili yako kuzitafuta kama mmisionari na kote katika maisha yako. Sifa kama za Kristo ni tabia au aina ya asili na hulka ya Mwokozi. Sura hii inaelezea baadhi ya sifa hizo. Jifunze kuhusu hizi na maandiko yanayohusiana nazo. Tafuta sifa zingine kama za Kristo wakati unapojifunza vifungu vingine vya maandiko.

Kujifunza Binafsi

Jifunze Mafundisho na Maagano 4. Ni sifa zipi Bwana anazibainisha kwamba ni muhimu kwa ajili ya wamisionari? Ni kwa jinsi gani sifa hizi zimekusaidia utimize dhumuni lako kama mmisionari?

“Mtafuteni Huyu Yesu”

Nabii Moroni alituhimiza, “Na sasa, nimekupendekeza kumtafuta huyu Yesu ambaye manabii na mitume wamemwandika” (Etheri 12:41). Njia mojawapo muhimu ya kumtafuta Yesu ni kufanya jitihada za bidii kujifunza kumhusu Yeye na kuwa zaidi kama Yeye. Misheni yako ni wakati mwafaka wa kufokasi kwenye hili.

Unapojitahidi kuwa zaidi kama Kristo, utatimiza vyema dhumuni lako kama mmisionari. Utapata uzoefu wa shangwe, amani, na ukuaji wa kiroho wakati sifa Zake zinapokuwa sehemu ya tabia yako. Pia utajenga msingi kwa ajili ya kuendelea kumfuata Yeye katika maisha yako yote.

Vipawa kutoka kwa Mungu

Sifa kama za Kristo ni vipawa kutoka kwa Mungu. Kama ilivyo kwa vitu vyote vizuri, vipawa hivi vinakuja kupitia “neema ya Mungu Baba, na pia Bwana Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu” (Etheri 12:41).

Fokasi juu ya Kristo unapotafuta kukuza sifa Zake (ona Mafundisho na Maagano 6:36). Sifa hizi siyo orodha ya vitu vya kutia alama ya vema. Hizo siyo mbinu unazokuza katika mpango wa kujiendeleza. Hazipatikani kupitia tu maamuzi binafsi. Badala yake, unaweza kuzipokea unapojitahidi kuwa mfuasi mwaminifi zaidi wa Yesu Kristo.

Sali ili Mungu akubariki upate sifa hizi. Kwa unyenyekevu kubali udhaifu wako na uhitaji wako wa nguvu Zake katika maisha yako. Unapofanya hivyo, Yeye “atafanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu [kwako]” (Etheri 12:27).

Mchakato wa Taratibu

Kuwa zaidi kama Mwokozi ni mchakato wa taratibu, wa maisha yote. Kwa tamanio la kumpendeza Mungu, boresha uamuzi mmoja kwa wakati mmoja.

Kuwa na subira kwako mwenyewe. Mungu anajua kwamba badiliko na ukuaji vinachukua muda. Yeye anapendezwa na tamanio lako la dhati na atakubariki kwa kila jitihada unayoifanya.

Unapotafuta kuwa zaidi kama Kristo, hamu yako, mawazo yako, na matendo yako yatabadilika. Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo na uwezo wa Roho Mtakatifu, asili yako itatakaswa (ona Mosia 3:19).

Picha
Parley P. Pratt

Roho Mtakatifu hukuza na kupanua uwezo wetu. Yeye “anahimiza usafi, ukarimu, wema, huruma, upole, na hisani. … Kwa kifupi, ni, kama ilivyokuwa, uroto mifupani, shangwe moyoni, nuru machoni, muziki masikioni, na uzima kwa mwili wote” (Parley P. Pratt, Key to the Science of Theology [1855], 98–99).

Kujifunza Maandiko

Maandiko haya yanafundisha nini kuhusu kufuata mfano wa Yesu Kristo?

Unaweza kujifunza nini kutoka katika maandiko yafuatayo kuhusu sifa kama za Kristo?

Picha
Inuka na Utembee, na Simon Dewey

Imani katika Yesu Kristo

Ili imani iongoze hadi kwenye wokovu, lazima kiini chake kiwe katika Yesu Kristo (ona Matendo 4:10–12; Mosia 3:17; Moroni 7:24–26). Unapokuwa na imani katika Kristo, unamtumainia Yeye kama Mwana Pekee wa Mungu. Unaamini kwamba unapotubu, utasamehewa dhambi zako kupitia dhabihu Yake ya kulipia dhambi na kutakaswa na Roho Mtakatifu (ona 3 Nefi 27:16, 20).

Imani si kuwa na ufahamu kamili. Badala yake, ni hakikisho kutoka kwa Roho juu ya vitu usivyoviona lakini ni vya kweli. (Ona Alma 32:21.)

Unaonyesha imani yako kupitia matendo. Matendo haya yanajumuisha kufuata mafundisho na mfano wa Mwokozi. Yanajumuisha kuwatumikia wengine na kuwasaidia wachague kumfuata Kristo. Pia unaonyesha imani yako kupitia bidii, toba, na upendo.

Imani ni kanuni ya nguvu. Unapoonesha imani katika Yesu Kristo, utabarikiwa kwa nguvu Zake zinazofaa kwa hali yako. Utaweza kuona miujiza kulingana na mapenzi ya Bwana. (Ona Yakobo 4:4–7; Moroni 7:33; 10:7.)

Imani yako katika Yesu Kristo itakua kadiri unavyomfahamu vyema Yeye na mafundisho Yake. Itaongezeka unapopekua maandiko, kusali kwa dhati, na kutii amri. Shaka na dhambi vinadhoofisha imani.

Picha
Mzee Neil L. Andersen

“Imani siyo tu hisia; ni uamuzi. Kwa sala, kujifunza, utiifu, na maagano, tunajenga na kuimarisha imani yetu. Kusadiki kwetu juu ya Mwokozi na kazi Yake ya siku za mwisho inakuwa lenzi yenye nguvu ambayo kupitia hiyo tunahukumu vitu vyote. Kisha, tunapojikuta kwenye sulubu ya maisha, … tunakuwa na nguvu za kuchukua njia sahihi” (Neil L. Andersen, “Ni kweli, Sivyo? Basi ni Kipi Kingine cha Maana?Liahona, Mei 2007, 74).

Kujifunza Maandiko

Imani ni Nini?

Ni kwa jinsi gani unaipata imani, na unaweza kufanya kipi kupitia imani?

Ni baraka zipi huja kupitia imani?

Picha
Tumaini la Kufufuka, na Joseph Brickey

Tumaini

Tumaini si tu fikra za kutamani. Badala yake, ni kujiamini kunakodumu, kulikojikita kwenye imani yako katika Kristo, kwamba Mungu atatimiza ahadi Zake kwako (ona Moroni 7:42). Ni tegemeo la “mambo mema yatakayokuwako” kupitia Kristo (Waebrania 9:11).

Chanzo chako cha msingi cha tumaini ni Yesu Kristo. Nabii Mormoni aliuliza: “Na ni kitu gani mtakachotumainia?” Kisha akajibu, “Mtakuwa na tumaini kupitia upatanisho wa Kristo na uwezo wa kufufuka kwake, kuinuliwa katika uzima wa milele, na hii kwa sababu ya imani yenu ndani yake kulingana na ile ahadi” (Moroni 7:41; ona mstari wa 40–43).

Unapofanya kiini cha tumaini lako kiwe katika Kristo, una hakikisho kwamba mambo yote yatafanyika pamoja kwa faida yako (ona Mafundisho na Maagano 90:24). Hakikisho hili hukusaidia ustahimili kwa imani wakati unapokabiliwa na majaribu. Linaweza pia kukusaidia ukue kutokana na majaribu na kukuza ukakamavu na nguvu za kiroho. Tumaini katika Kristo hutoa nanga kwa ajili ya nafsi yako (ona Etheri 12:4).

Tumaini hukupa kujiamini kwamba Mungu atakuza bidii yako, jitihada zako za haki (ona Mafundisho na Maagano 123:17).

Njia mojawapo ya kuongeza tumaini ni kupitia toba. Kutakaswa na kusamehewa kupitia dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi huzalisha na kufufua tumaini (ona Alma 22:16).

Nefi alihimiza, “Usonge mbele ukiwa na imani imara katika Kristo, ukiwa na mg’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote” (2 Nefi 31:20). Kadiri unavyoishi injili, utaongezeka katika uwezo wako wa “kuzidi sana katika tumaini” (Warumi 15:13).

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

“Katika nyakati za dhiki, tunaweza kushikilia kwa nguvu kwenye tumaini kwamba mambo ‘yatafanyika pamoja kwa faida [yetu]’ pale tunapofuata ushauri wa manabii wa Mungu. Aina hii ya tumaini katika Mungu, uzuri Wake, na nguvu Zake hutufanya upya kwa ujasiri wakati wa changamoto ngumu na huwapa nguvu wale wanaohisi kutishwa na kuta zinazowazunguka za hofu, mashaka, na kukata tamaa” (Dieter F. Uchtdorf, “Nguvu Zisizo na Mwisho za Tumaini,” Liahona, Nov. 2008, 23).

Kujifunza Maandiko

Tumaini ni nini, na ni kitu gani tutakachokitumainia?

Picha
Kristo na Watoto, na Minerva Teichert

Hisani na Upendo

Mtu mmoja wakati fulani alimuuliza Yesu, “Ni amri gani iliyo kuu katika sheria?” Yesu alijibu: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. “Na ya pili yafanana nayo, Mpende jirani yako kama nafsi yako” (Mathayo 22:36–39).

Hisani ni “upendo msafi wa Kristo” (Moroni 7:47). Hujumuisha upendo wa milele wa Mungu kwa watoto Wake wote.

Nabii Mormoni alifundisha, “Ombeni kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, kwamba mjazwe na upendo huu” (Moroni 7:48). Unaposali ili hisani ijaze moyo wako, utaonja upendo wa Mungu. Upendo wako kwa ajili ya watu utaongezeka, na utakuja kuhisi wasiwasi wa dhati kwa ajili ya furaha yao. Utawaona wao kama watoto wa Mungu wenye uwezekano wa kuwa kama Yeye, na utafanya kazi kwa niaba yao.

Unaposali kwa ajili ya karama ya hisani, hutakubali kukaa kwenye hisia hasi kama vile hasira au wivu. Utakuwa na uwezekano mdogo wa kuwahukumu au kuwakosoa wengine. Utakuwa na hamu zaidi ya kujaribu kuwaelewa wao na mitazamo yao. Utaweza kuwa na subira zaidi na kujaribu kuwasaidia watu wakati wanapojitahidi au wanapokuwa wamevunjika moyo. (Ona Moroni 7:45.)

Hisani, kama imani, huongoza kwenye matendo. Unaiimarisha hisani unapowatumikia wengine na kujitolea.

Hisani huleta mabadiliko. Baba wa Mbinguni huitoa “kwa wote ambao ni wafuasi wa kweli wa Mwanaye, Yesu Kristo; … kwamba wakati atakapoonekana tutakuwa kama yeye, … ili tutakaswe hata vile alivyo mtakatifu” (Moroni 7:48).

Kujifunza Maandiko

Hisani ni nini?

Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo anaonesha hisani?

Ni kipi unaweza kujifunza kuhusu hisani kutoka katika maandiko yafuatayo?

Picha
Esta (Malkia Esta), na Minerva Teichert

Utu Wema

“Tunaamini katika kuwa … wema” Makala ya Imani inasema (1:13). Utu wema ni mpangilio wa mawazo na tabia zilizojengwa katika viwango vya juu vya maadili. Ni uaminifu kwa Mungu na kwa wengine. Sehemu muhimu ya utu wema ni kujitahidi kuwa msafi na halisi kiroho na kimwili.

Usafi huanzia katika mawazo yako na matamanio. “Na wema uyapambe mawazo yako bila kukoma,” Bwana alisema (Mafundisho na Maagano 121:45). Fokasi kwenye mawazo ya haki, ya kuinua. Weka mawazo yasiyostahili nje ya akili yako badala ya kukaa nayo.

Akili yako ni kama jukwaa katika ukumbi. Kama utaruhusu mawazo yasiyofaa kubaki katika jukwaa la akili yako, una uwezekano mkubwa wa kutenda dhambi. Kama utashughulika kuijaza akili yako mambo yanayofaa, una uwezekano mkubwa wa kukumbatia kile kilicho chema na kuepukana na uovu. Kuwa na busara kuhusu kile unachokiruhusu kiingie na kubaki kwenye jukwaa la akili yako.

Unapojizatiti kuishi kwa wema, “kujiamini kwako kutakuwa imara katika uwepo wa Mungu; na … Roho Mtakatifu atakuwa mwenzi wako daima” (Mafundisho na Maagano 121:45–46).

Kujifunza Maandiko

Inamaanisha nini kuwa mwema?

Uadilifu

Uadilifu hutiririka kutoka kwenye amri kuu ya kwanza ya kumpenda Mungu (ona Mathayo 22:37). Kwa sababu unampenda Mungu, wewe ni mkweli Kwake nyakati zote. Kama wana wa Mosia, “utatembea wima mbele yake” (Alma 53:21).

Unapokuwa mwadilifu, unaelewa kwamba kuna usahihi na kosa, na kwamba kuna ukweli kamili—ukweli wa Mungu. Unatumia haki yako ya kujiamulia kuchagua kulingana na ukweli wa Mungu, na unatubu haraka pale ambapo unaenda kinyume. Kile unachochagua kufikiria—na kile unachofanya wakati unaamini hakuna mtu anayetazama—ni kipimo thabiti cha uadilifu wako.

Picha
Danieli katika Pango la Simba, na Clark Kelley Price

Uadilifu humaanisha kutoshusha viwango vyako au tabia ili uweze kuwapendeza watu au kukubalika kwa wengine. Unafanya kile kilicho sahihi hata wakati wengine wanapodhihaki hamu yako ya kuwa mkweli kwa Mungu (ona 1 Nefi 8:24–28). Unaishi kwa heshima katika mazingira yote, ikijumuisha jinsi unavyojiweka mtandaoni.

Unapokuwa mwadilifu, unashika maagano yako na Mungu vile vile ahadi zako za haki kwa wengine.

Uadilifu hujumuisha kuwa mwaminifu kwa Mungu, wewe mwenyewe, viongozi wako na watu wengine. Husemi uongo, hauibi, haulaghai. Unapofanya kitu kimakosa, unakubali kuwajibika na kutubu badala ya kujaribu kuhalalisha au kutafuta sababu.

Unapoishi kwa uadilifu, utakuwa na amani ya ndani na mtu mwenye kujiheshimu. Bwana na wengine watakuamini.

Kujifunza Maandiko

Ni kwa jinsi gani Yesu alionesha uadilifu hata katika nyakati zisizo salama?

Ni jinsi gani vijana mashujaa katika jeshi la Helamani walionesha uadilifu?

Ni jinsi gani Danieli alionesha uadilifu? Ni jinsi gani Mungu alimbariki Danieli kwa uadilifu wake?

Kwa nini Bwana alimpenda Hyrum kaka wa Joseph Smith?

Picha
Ongeza kwenye Imani, Wema, na Walter Rane

Maarifa

Bwana alishauri, “Tafuteni maarifa, hata kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118). Wakati wa misheni yako na kote katika maisha yako, tafuta maarifa, hasa maarifa ya kiroho.

Jifunze maandiko kila siku, vile vile maneno ya manabii walio hai. Kupitia kujifunza na sala, tafuta msaada kwa ajili ya maswali mahususi, changamoto, na fursa. Tafuta vifungu vya maandiko unayoweza kuvitumia katika kufundisha na katika kujibu maswali kuhusu injili.

Unapojifunza kwa bidii na kwa sala, Roho Mtakatifu ataangaza akili yao. Yeye atakufundisha na kukupa uelewa. Yeye atakusaidia utumie mafundisho ya maandiko na manabii wa siku za mwisho katika maisha yako. Kama vile Nefi, unaweza kusema:

“Moyo wangu unafurahia katika maandiko, na moyo wangu huyatafakari. … Tazama, nafsi yangu hufurahia vitu vya Bwana; na moyo wangu huvitafakari mara kwa mara vitu ambavyo nimeviona na kuvisikia” (2 Nefi 4:15–16).

Kujifunza Maandiko

Ni jinsi gani maarifa yanaweza kukusaidia uifanye kazi ya Bwana?

Ni jinsi gani unaweza kupata maarifa?

Picha
kivuli cha mtu kutokana na mwangaza wa jua

Subira

Subira ni uwezo wa kumtumainia Mungu wakati unapokabiliwa na uchelewaji, upinzani, au mateso. Kupitia imani yako, unatumainia mpangilio wa Mungu kwa ajili ya baraka Zake alizoahidi kutimizwa.

Unapokuwa na subira, unayatazama maisha kutoka kwenye matazamo wa milele. Hutegemei baraka au matokeo ya papo hapo. Matamanio yako ya haki kwa kawaida yatatambulika “mstari juu ya mstari, … hapa kidogo na pale kidogo” (2 Nefi 28:30). Baadhi ya matamanio ya haki yanaweza yasipatikane hadi baada ya maisha haya.

Subira siyo kuwa mzembe au kukata tamaa pasipo kufanya juhudi. Ni “kwa furaha [kuyafanya] mambo yote yaliyo katika uwezo [wako]” pale unapomtumikia Mungu (Mafundisho na Maagano 123:17). Unapanda, unaimwagilia maji, na unairutubisha mbegu, na Mungu anatoa ongezeko “pole pole” (Alma 32:42; ona pia 1 Wakorintho 3:6–8). Unafanya kazi kwa ubia na Mungu, ukitumainia kwamba wakati utakapokuwa umefanya sehemu yako, Yeye atatimiza kazi Yake katika wakati Wake na kulingana na haki ya kujiamulia ya mtu.

Subira pia humaanisha kwamba wakati kitu fulani hakiwezi kubadilishwa, unakikubali kwa ujasiri, neema, na imani.

Kuza subira kwa wengine, ikijumuhisha mwenza wako na wale unaowahudumia. Kuwa na subira kwako wewe mwenyewe. Jitahidi kuwa bora zaidi ndani yako mwenyewe huku ukifahamu kwamba utakua hatua kwa hatua.

Kama zilivyo sifa zingine kama za Kristo, kukua katika subira ni mchakato wa maisha yote. Kuonesha subira kunaweza kuwa na ushawishi wa uponyaji juu ya nafsi yako na juu ya wale wanaokuzunguka.

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

“Subira inamaanisha kusuburi kwa uchangamfu na uvumilivu. Inamaanisha kubaki na jambo fulani na kufanya yale yote tunayoweza—kufanya kazi, kutumaini, na kuonesha imani; kustahimili ugumu kwa ushupavu, hata wakati matamanio ya mioyo yetu yanapochelewa. Subira si tu kuvumilia, ni kuvumilia vyema!” (Dieter F. Uchtdorf, “Endelea kwa Subira,” Liahona, Mei 2010, 57).

Kujifunza Binafsi

Jifunze Mosia 28:1–9.

  • Je, matamanio ya wana wa Mosia yalikuwa yapi?

  • Je, ushauri wa Bwana kwa wamisionari hao ulikuwa upi? (Ona Alma 17:10–11; 26:27.)

  • Yapi yalikuwa matokeo ya subira na bidii yao? (Ona Alma 26.)

Andika majibu yako katika shajara yako ya kujifunzia.

Kujifunza Maandiko

Kwa nini subira ni muhimu? Ni jinsi gani subira na imani vinahusiana?

Picha
Akimpendeza Mungu (Yesu Akisali pamoja na Mama Yake), na Simon Dewey

Unyenyekevu

Unyenyekevu ni utayari wa kujiweka chini ya mapenzi ya Bwana. Ni utayari wa kumpa Yeye heshima kwa kile kilichokamilishwa. Ni kuwa wenye kufundishika (ona Mafundisho na Maagano 136:32). Unyenyekevu hujumuisha shukrani kwa ajili ya baraka za Mungu na kutambua uhitaji wako wa kila mara wa msaada Wake. Yeye huwasaidia wale walio wanyenyekevu.

Unyenyekevu ni ishara ya nguvu za kiroho, wala si udhaifu. Unyenyekevu ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa kiroho (ona Etheri 12:27).

Unapomtumainia Bwana kwa unyenyekevu, unaweza kuwa na hakikisho kwamba amri Zake ni kwa faida yako. Unakuwa na ujasiri kwamba unaweza kufanya lolote Yeye analohitaji kutoka kwako kama utamtegemea Yeye. Pia upo tayari kuwatumainia watumishi Wake na kufuata ushauri wao. Unyenyekevu utakusaidia uwe mtiifu, ufanye kazi kwa bidii, na utumikie.

Kinyume cha unyenyekevu ni kiburi. Kuwa na kiburi humaanisha kuweka tumaini kubwa juu yako mwenyewe kuliko katika Mungu. Pia humaanisha kuweka mambo ya ulimwengu juu ya mambo ya Mungu. Kiburi ni ushindani; wale walio na kiburi wanatafuta kuwa na vingi na kudhania wao ni bora kuliko wengine. Kiburi ni kikwazo kikubwa sana.

Kujifunza Maandiko

Je, inamaanisha nini kuwa mnyenyekevu?

Je, ni baraka zipi unapokea unapokuwa mnyenyekevu?

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kutambua kiburi ndani yako?

Picha
Paulo, mtume, akiwafundisha umati

Bidii

Bidii ni juhudi endelevu, na ya dhati. Katika kazi ya umisionari, bidii ni dhihirisho la upendo wako kwa Bwana. Unapokuwa na bidii, utapata shangwe na kuridhika katika kazi ya Bwana (ona Alma 26:16).

Bidii hujumuisha kufanya mambo mengi mazuri kwa hiari yako mwenyewe badala ya kuwangoja viongozi wakuambie nini cha kufanya (ona Mafundisho na Maagano 58:27–29).

Endelea kufanya mambo mazuri hata yanapokuwa magumu au unapokuwa umechoka. Lakini tambua hitaji la usawa na kupumzika ili “usikimbie zaidi kuliko nguvu [ulizo nazo]” (Mosia 4:27).

Fokasi moyo wako na mapendeleo yako kwa Bwana na kazi Yake. Epukana na mambo ambayo yanavuruga mawazo kutoka kwenye vipaumbele vyako. Fokasi muda na juhudi zako kwenye shughuli ambazo zitakuwa na manufaa zaidi katika eneo lako na zenye msaada sana kwa watu unaowafundisha.

Picha
Rais Henry B. Eyring

“Hili ni Kanisa la Bwana. Yeye alituita na kutuamini hata katika udhaifu ambao Yeye alijua tunao. Yeye alijua majaribu ambayo yangetukabili. Kwa huduma ya uaminifu na kupitia Upatanisho Wake, tunaweza kuja kutaka kile ambacho Yeye anakitaka na kuwa kile ambachi sisi lazima tuwe ili kuwabariki wale tunaowatumikia kwa niaba Yake. Tunapomtumikia Yeye muda mrefu vya kutosha na kwa bidii, tutabadilika. Daima tunaweza kuwa zaidi kama Yeye” (Henry B. Eyring, “Tenda kwa Bidii Yote,” Liahona, Mei 2010, 62–63).

Kujifunza Maandiko

Inamaanisha nini kuwa na bidii?

Je, ni kwa nini Bwana anategemea uwe mwenye bidii?

Je, ni kwa jinsi gani bidii inahusiana na haki ya kujiamulia?

Picha
Vijana Mashujaa Elfu Mbili (Askari Vijana Elfu Mbili), na Arnold Friberg

Utiifu

Huduma yako kama mmisionari ni mwendelezo wa maagano uliyoyafanya na Mungu wakati wa ubatizo na ndani ya hekalu. Ulipopokea ibada za ubatizo na endaumenti, ulifanya agano kwamba ungezishika amri Zake.

Mfalme Benjamini alifundisha: “Ningetamani kwamba mtafakari juu ya hali ya baraka na yenye furaha ya wale wanaotii amri za Mungu. Kwani tazama, wamebarikiwa katika vitu vyote, vya kimwili na vya kiroho; na kama watavumilia kwa uaminifu hadi mwisho watapokewa mbinguni, kwamba hapo wanaweza kuishi na Mungu katika hali ya furaha isiyo na mwisho” (Mosia 2:41).

Kutii amri ni dhihirisho la upendo kwa ajili ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo (ona Yohana 14:15). Yesu alisema, “Kama mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; hata kama nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake” (Yohana 15:10).

Fuata miongozo katika Viwango vya Umisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo. Pia fuata ushauri wa rais wako wa misheni na mke wake kama walivyokushauri kwa haki.

Picha
Mzee Dale G. Renlund

“Utiifu ni chaguo letu. Mwokozi aliliweka hili wazi. Kama ilivyotamkwa katika Tafsiri ya Joseph Smith ya Luka 14:28, Yesu alielekeza, ‘Kwa hiyo wekeni hii, mioyoni mwenu, kwamba mtatenda mambo ambavyo nitawafundisha, na kuwaamuru.’ Ni rahisi hivyo. … Tunapofanya hivyo, uimara wetu wa kiroho utaongezeka sana. Tutaepukana na kufuja rasilimali zilizotolewa na Mungu na kufanya uasi usio na faida na wenye kuangamiza katika maisha yetu (Dale G. Renlund, “Kujenga Uimara wa Kiroho” [Brigham Young University devotional, Sept. 16, 2014], 2, speeches.byu.edu).

Kujifunza Maandiko

Je unaweza kujifunza nini kuhusu utiifu kutokana na maandiko yafuatayo?

Picha
Kristo na Wavuvi (Wewe Wanipenda Kuliko Hawa), na J. Kirk Richards

Mpangilio wa Kuwa Zaidi Kama Kristo

Mpangilio ufuatao unaweza kukusaidia ukuze na upokee sifa zilizoelezwa katika sura hii na sifa zingine zilizoelezwa katika maandiko.

  • Tambua sifa unazotaka kuzitafuta.

  • Andika maelezo ya sifa hizi.

  • Orodhesha na jifunze vifungu vya maandiko ambavyo vinaonesha mifano ya sifa au vile vinavyofundisha kuhusu sifa hizo.

  • Andika hisia zako na misukumo yako.

  • Weka malengo na mipango ya kusonga katika sifa hizi.

  • Sali kwa Mungu akusaidie ukuze na upokee sifa hizi.

  • Tathimini maendeleo yako mara kwa mara.

Picha
Mzee Jeffrey R. Holland

“Bwana huwabariki wale ambao wanataka kuendelea, ambao wanakubali haja ya amri na kujaribu kuzitii, wanaothamini tabia za Kristo na kujitahidi kwa uwezo wao wote kuzipata. Kama unajikwaa katika harakati hiyo, kila mtu hujikwaa; Mwokozi yupo kukusaidia usonge mbele. … Punde vya kutosha utakuwa na ufanisi unaoutafuta” (Jeffrey R. Holland, “Kesho Bwana Atafanya Miujiza Miongoni Mwenu,” Liahona,, Mei 2016, 126).

Kujifunza Binafsi

Bainisha sifa moja kutoka katika sura hii au kutoka kwenye maandiko. Fuata mpangilio kama iliyoelezewa ili kuelewa na kutafuta sifa hii.

Tazama beji yako ya umisionari. Je, ni kwa jinsi gani inatofautiana na zile zinazovaliwa na waajiriwa wa kampuni? Fahamu kwamba sehemu mbili muhimu zaidi ni jina lako na jina la Mwokozi.

  • Je, ni kwa jinsi gani unaweza kumwakilisha vyema Mwokozi kama mmoja wa wafuasi Wake?

  • Kwa nini ni muhimu kwa watu kuhusisha jina lako na la Mwokozi katika njia chanya?

Andika fikra zako katika shajara yako ya kujifunzia.

Kujifunza Maandiko

Rejelea sifa zilizoorodheshwa katika maandiko yafuatayo. Andika misukumo yoyote katika shajara yako ya kujifunzia.


Mawazo kwa ajili ya Kujifunza na Kutumia

Kujifunza Binafsi

  • Mara kwa mara timiza “Shughuli ya Sifa” mwisho wa sura hii.

  • Bainisha sifa katika sura hii. Jiulize:

    • Ni jinsi gani ninaweza kujifunza zaidi kuhusu sifa hii?

    • Ni jinsi gani kutafuta sifa hii kunanisaidia niwe mtumishi bora wa injili ya Yesu Kristo?

  • Tafuta mifano ya sifa kama za Kristo katika maisha ya wanaume na wanawake katika maandiko. Andika misukumo yako katika shajara yako ya kujifunzia.

  • Tafuta mifano ya sifa kama za Kristo katika muziki mtakatifu wa Kanisa. Unapoitafuta sifa, kariri maneno ya nyimbo za dini au nyimbo ili kupata nguvu na uwezo. Rudia au imba maneno haya wewe mwenyewe kwa ajili ya mwongozo na kualika ushawishi wa Roho.

Kujifunza pamoja na Mwenza na Kubadilishana Mwenza

  • Jifunzeni marejeleo ya sifa kama za Kristo katika Maktaba ya Injili au nyenzo zingine zilizoidhinishwa. Jadilini jinsi ya kutumia kile mnachojifunza. Mnaweza pia kujadili kile mlichojifunza katika juhudi zenu binafsi za kuwa kama Kristo.

Baraza la Wilaya, Mikutano ya Kanda na Baraza la Uongozi la Misheni

  • Siku kadhaa kabla ya baraza au mkutano, waombe wamisionari waandae hubiri la dakika tano juu ya sifa kama za Kristo. Ruhusu muda katika mkutano kwa ajili ya wamisionari wachache kushiriki mazungumzo yao.

  • Wagawe wamisionari katika vikundi vinne na uwape majukumu yafuatayo:

    Kundi la 1: Lisome 1 Nefi 17:7–16 na lijibu maswali yafuatayo:

    • Je, ni kwa jinsi gani Nefi alifanyia kazi imani yake?

    • Je, ni kitu gani Nefi alikifanya ambacho kilikuwa kama cha Kristo?

    • Je, ni ahadi zipi Bwana alizifanya kwa Nefi?

    • Je, ni kwa jinsi gani tukio hili linahusika katika kazi ya umisionari?

    Kundi la 2: Lisome Marko 5:24–34 na lijibu maswali yafuatayo:

    • Ni jinsi gani mwanamke huyu alionesha imani katika Yesu Kristo?

    • Kwa nini aliponywa?

    • Ni jinsi gani tunaweza kufuata mfano wake katika juhudi zetu za umisionari?

    Kundi la 3: Lisome Yakobo 7:1–15 na lijibu maswali yafuatayo:

    • Kwa nini imani ya Yakobo ilikuwa imara vya kutosha kukinza shambulio la Sheremu?

    • N jinsi gani Yakobo alionesha imani wakati alipokuwa akizungumza na Sheremu?

    • Ni jinsi gani matendo ya Yakobo yalikuwa kama ya Kristo?

    Kundi la 4: Lisome Joseph Smith—Historia ya 1:8–18 na lijibu maswali yafuatayo:

    • Ni kwa njia gani Joseph Smith alionesha imani katika Kristo?

    • Ni jinsi gani imani yake ilijaribiwa?

    • Ni kipi alikifanya ambacho kilikuwa kama cha Kristo?

    • Ni jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Joseph Smith?

    Baada ya makundi kumaliza, walete wamisionari pamoja na uwaombe washiriki kile walichojadili.

Viongozi wa Misheni na Washauri wa Misheni

  • Waombe wamisionari wasome mojawapo ya injili nne katika Agano Jipya au 3 Nefi 11–28. Waruhusu wapigie mstari kile ambacho Mwokozi alifanya na ambacho wao pia wanaweza kukifanya.

  • Tumia kuweka malengo na kupanga ili kuwafundisha wamisionari kuhusu bidii. Onesha jinsi bidii katika kufokasi kwa watu ni dhihirisho la upendo.

  • Wakati wa mahojiano au mazungumzo, waombe wamisionari wazungumze kuhusu sifa kama za Kristo wanazozitafuta.

Shughuli ya Sifa

Kusudi la shughuli hii ni kukusaidia utambue fursai za ukuaji wa kiroho. Soma kila kipengele hapo chini. Amua jinsi gani kauli hiyo ni kweli kuhusu wewe, na chagua jibu sahihi. Andika majibu yako katika shajara yako ya kujifunzia.

Hakuna anayeweza kujibu “daima” kwa kila kauli. Ukuaji wa kiroho ni mchakato wa maisha yote. Hiyo ni sababu mojawapo ya kuwa yenye kusisimua na inayoleta tuzo—kwa sababu kuna fursa zisizo na hesabu za kukua na kupata uzoefu wa baraka za ukuaji.

Kuwa huru kuanzia pale ulipo. Jiwekee ahadi ya kufanya kazi ya kiroho inayohitajika kwa ajili ya ukuaji. Tafuta msaada wa Mungu. Unapokuwa na vikwazo, kuwa na ujasiri kwamba Yeye atakusaidia. Unaposali, tafuta mwongozo kuhusu ni sifa zipi za kufokasi juu yake katika nyakati tofauti wakati wa misheni yako.

Ufunguo wa Majibu

  • 1= kamwe

  • 2= nyakati fulani

  • 3= mara kwa mara

  • 4= karibu kila wakati

  • 5= kila mara

Imani

  1. Ninaamini katika Kristo na kumkubali Yeye kama Mwokozi wangu. (2 Nefi 25:29)

  2. Ninahisi kujiamini kwamba Mungu ananipenda. (1 Nefi 11:17)

  3. Ninamtumainia Mwokozi vya kutosha kukubali mapenzi Yake na kufanya kile ambacho Yeye anataka. (1 Nefi 3:7)

  4. Ninaamini kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo na uwezo wa Roho Mtakatifu, ninaweza kusamehewa dhambi zangu na kutakaswa pale ninapotubu. (Enoshi 1:2–8)

  5. Nina imani kwamba Mungu husikia na kujibu sala zangu. (Mosia 27:14)

  6. Ninafikiria kuhusu Mwokozi wakati wa mchana na kukumbuka kile ambacho Yeye amefanya kwa ajili yangu. (Mafundisho na Maagano 20:77, 79)

  7. Nina imani kwamba Mungu ataleta mambo mazuri katika maisha yangu na maisha ya wengine kadiri wanavyojitolea wenyewe Kwake Yeye na Mwanaye. (Etheri 12:12)

  8. Ninajua kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. (Moroni 10:3–5)

  9. Nina imani ya kutimiza kile ambacho Yesu ananitaka nifanye. (Moroni 7:33)

Tumaini

  1. Mojawapo ya tamanio langu kuu ni kuurithi uzima wa milele katika ufalme wa selestia. (Moroni 7:41)

  2. Nina hakika kwamba nitakuwa na misheni yenye furaha na yenye ufanisi. (Mafundisho na Maagano 31:3–5)

  3. Ninahisi kuwa na amani na kuwa na tumaini kuhusu siku zijazo. (Mafundisho na Maagano 59:23)

  4. Ninaamini kwamba siku moja nitaishi na Mungu na kuwa kama Yeye. (Etheri 12:4)

Hisani na Upendo

  1. Ninahisi tamanio la kweli kwa ajili ya ustawi na furaha ya milele ya wengine. (Mosia 28:3)

  2. Ninaposali, ninaomba kwa ajili ya hisani—upendo msafi wa Kristo. (Moroni 7:47–48)

  3. Ninajaribu kuelewa hisia za wengine na kuona mtazamo wao. (Yuda 1:22)

  4. Ninawasamehe wengine ambao wamenikwaza au kunikosea. (Waefeso 4:32)

  5. Ninafikia kwa upendo ili kuwasaidia wale walio wapweke, wanaotaabika, au wenye kuvunjika moyo. (Mosia 18:9)

  6. Pale ambapo inafaa, ninaonesha upendo wangu na kuwajali wengine kwa kuwatumikia kwa maneno na vitendo. (Luka 7:12–15)

  7. Ninatafuta fursa za kuwahudumia wengine. (Mosia 2:17)

  8. Ninasema mambo chanya kuhusu wengine. (Mafundisho na Maagano 42:27)

  9. Mini ni mkarimu na mwenye subira kwa wengine, hata wakati inapokuwa vigumu kupatana nao. (Moroni 7:45)

  10. Ninapata shangwe katika mafanikio ya wengine. (Alma 17:2–4)

Wema

  1. Mimi ni msafi na halisi moyoni. (Zaburi 24:3–4)

  2. Nina tamanio la kufanya mema. (Mosia 5:2)

  3. Ninafokasi juu ya mawazo ya haki, ya yenye kuinua na kuyaweka mawazo yasiyostahili nje ya akili yangu. (Mafundisho na Maagano 121:45)

  4. Ninatubu dhambi zangu na kujitahidi kushinda udhaifu wangu. (Mafundisho na Maagano 49:26–28; Etheri 12:27)

  5. Ninahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yangu. (Mafundisho na Maagano 11:12–13)

Uadilifu

  1. Mimi ni mkweli kwa Mungu nyakati zote. (Mosia 18:9)

  2. Mimi sishushi viwango vyangu au tabia yangu ili niweze kuwapendeza au kukubalika kwa wengine. (1 Nefi 8:24–28)

  3. Mimi ni mwaminifu kwa Mungu, kwangu mimi mwenyewe, kwa viongozi wangu na kwa wengine. (Mafundisho na Maagano 51:9)

  4. Mimi ni wa kutegemewa. (Alma 53:20)

Maarifa

  1. Ninahisi kujiamini katika uelewa wangu wa mafundisho na kanuni za injili. (Alma 17:2–3)

  2. Ninajifunza maandiko kila siku. (2 Timotheo 3:16–17)

  3. Ninatafuta kuelewa ukweli na kupata majibu ya maswali yangu. (Mafundisho na Maagano 6:7)

  4. Ninatafuta maarifa na mwongozo kupitia Roho. (1 Nefi 4:6)

  5. Ninathamini mafundisho na kanuni za injili. (2 Nefi 4:15)

Subira

  1. Ninangojea kwa subira baraka na ahadi za Bwana kutimia. (2 Nefi 10:17)

  2. Ninaweza kungojea mambo bila kukasirika au kukata tamaa. (Warumi 8:25)

  3. Mimi ni mwenye subira katika changamoto za kuwa mmisionari. (Alma 17:11)

  4. Mimi nina subira kwa wengine. (Warumi 15:1)

  5. Mimi nina subira kwangu mimi mwenyewe na ninamtegemea Bwana kadiri ninavyofanya kazi ili kuyashinda madhaifu yangu. (Etheri 12:27)

  6. Ninakabiliana na dhiki kwa subira na imani. (Alma 34:40–41)

Unyenyekevu

  1. Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo. (Mathayo 11:29)

  2. Ninamtegemea Mungu kwa ajili ya msaada. (Alma 26:12)

  3. Mimi nina shukrani kwa ajili ya baraka ninazopokea kutoka kwa Mungu. (Alma 7:23)

  4. Sala zangu ni za dhati na za kweli. (Enoshi 1:4)

  5. Ninashukuru kwa maelekezo kutoka kwa viongozi au walimu wangu. (2 Nefi 9:28–29)

  6. Ninajitahidi kujiweka chini ya mapenzi ya Mungu. (Mosia 24:15)

Bidii

  1. Ninafanya kazi kwa ufanisi, hata wakati siko chini ya usimamizi wa karibu. (Mafundisho na Maagano 58:26–27)

  2. Ninafokasi juhudi zangu kwenye mambo muhimu zaidi. (Mathayo 11:23)

  3. Nina sala binafsi angalau mara mbili kwa siku. (Alma 34:17–27)

  4. Ninafokasi mawazo yangu kwenye wito wangu kama mmisionari. (Mafundisho na Maagano 4:2, 5)

  5. Ninaweka malengo na kupanga kila mara. (Mafundisho na Maagano 88:119)

  6. Ninafanya kazi kwa bidii mpaka kazi inapomalizika. (Mafundisho na Maagano 10:4)

  7. Ninapata shangwe na kuridhika katika kazi yangu. (Alma 36:24–25)

Utiifu

  1. Ninaposali, ninaomba kwa ajili ya nguvu za kukinza majaribu na kufanya kile kilicho sahihi. (3 Nefi 18:15)

  2. Mimi ni mwenye kustahili kuwa na kibali cha hekalu. (Mafundisho na Maagano 97:8)

  3. Mimi niko radhi kutii sheria za misheni na kufuata ushauri wa viongozi wangu. (Waebrania 13:17)

  4. Ninajitahidi kuishi kulingana na sheria na kanuni za injili. (Mafundisho na Maagano 41:5)