Miito ya Misheni
Utangulizi wa Hubiri Injili Yangu


“Utangulizi wa Hubiri Injili Yangu,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Utangulizi,” Hubiri Injili Yangu

Utangulizi wa Hubiri Injili Yangu

Bwana anawaelekeza watumishi Wake “hubiri injili yangu kwa njia ya Roho, hata Mfariji aliyetumwa kufundisha ukweli” (Mafundisho na Maagano 50:14).

Hubiri Injili Yangu imesanifiwa ili kukusaidia utimize dhumuni lako kama mmisionari. Inafokasi juu ya mambo muhimu ya kazi ya umisionari. Haijibu kila swali au kutoa mwelekeo wa kila hali utayokabiliana nayo. Hata hivyo, ni nyenzo muhimu kwa ajili yako ili ukue katika nguvu na uwezo wa kiroho. Jifunze na utumie mafundisho na kanuni za injili kama zinavyopatikana katika maandiko na katika kitabu hiki.

Picha
Yohana Mbatizaji akimbatiza Yesu Kristo

Hubiri Injili Yangu imepangiliwa ili kukusaidia wewe katika njia zifuatazo:

Jifunze sura hizi ukirudiarudia katika misheni yako yote. Tathmini kazi yako. Weka malengo na ufanye mipango ya kuyatimiza. Wamisionari ambao wanajiandaa kila siku na kujiboresha kila mara watabariki maisha ya wale wanaowafundisha na kuwatumikia. Pia watapokea baraka katika maisha yao wenyewe.

Fursa za Kujifunza na Kufundisha

Ujifunzaji wenye tija wakati wa misheni yako utakusaidia uimarishe ushuhuda wako juu ya injili na uwe mfuasi mwaminifu zaidi wa Yesu Kristo.

Kujifunza maandiko na Hubiri Injili Yangu kutakusaidia ufundishe kwa nguvu ya roho. Pia kutakusaidia ufanye mafundisho yako yawe yenye kufaa kwa mahitaji ya watu binafsi.

Fursa muhimu za kujifunza na kujifundisha zinajumuisha:

  • Kujifunza Binafsi

  • Kujifunza na mmisionari mwenza

  • Mabadilishano ya mmisionari mwenza.

  • Mikutano ya baraza la wilaya.

  • Mikutano mikuu ya kanda.

  • Baraza la uongozi wa ummisionari (kwa ajili ya viongozi wa wamisionari vijana.)

Mara nyingi, ratiba yako ya ummisionari hujumuisha muda wa kujifunza binafsi na pamoja na mmisionari mwenza. Ona Viwango vya Umisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo, 2.4, kwa maelezo kuhusu ratiba yako ya kila siku.

Kile unachosoma katika kujifunza kwako binafsi kitakusaidia katika kujifunza na mmisionari mwenza na fursa zingine zilizoorodheshwa hapo juu. Katika mazingira haya “fundishaneni mafundisho ya ufalme” (Mafundisho na Maagano 88:77).

Picha
Yesu Kristo akiwafundisha umati

Mawazo ya Kuboresha Ujifunzaji Wako wa Hubiri Injili Yangu

Hubiri Injili Yangu inafungamanisha maandiko na kanuni za injili pamoja ili kukusaidia uje kumjua Mwokozi na Injili Yake. Inakusudiwa kusaidia kukuvuta wewe ndani ya maandiko na kuboresha kujifunza kwako maandiko hayo. Jifunze marejeleo ya maandiko katika kila sura katika misheni yako yote.

Kila sura katika Hubiri Injili Yangu inajumuisha mawazo na shughuli za kukusaidia ujifunze na utumie kile unachojifunza. Vitumie hivi katika kujifunza kwako binafsi na pamoja na mwenza (ona Viwango vya Umisionari, 2.4). Unaweza pia kuyatumia wakati wa mikutano ya baraza la wilaya na mikutano mikuu ya kanda. Kujifunza kwako kutakuwa na tija zaidi wakati unapotafuta njia za kutumia kile ulichojifunza.

Inasaidia kuwa na mpango kwa ajili ya kujifunza binafsi. Ungeweza kutengeneza mpango wako mwenyewe ambao unatoa kipaumbele kwa kanuni za injili ambazo ungependa uzielewe vizuri zaidi. Ungeweza pia kupanga kujifunza kwako kuwe kwenye sura katika Hubiri Injili Yangu. Kwa mfano, ungeweza kutumia masomo katika sura ya 3 ili kuongoza kujifunza kwako mafundisho na kanuni utakazozifundisha. Unahitaji kuyaelewa masomo haya vyema ili uweze kufundisha kwa Roho kwa kutumia maneno yako mwenyewe.

Andika mihutasari wakati unapojifunza. Tumia karatasi au shajara ya kielektroniki ya kujifunzia (kama vile Maktaba ya Injili) ili ikusaidie uelewe, ufafanue, na ukumbuke kile unachojifunza.

Anza kujifunza kwako kwa maombi kwa ajili ya Roho Mtakatifu ili akusaidie ujifunze. Atakuletea maarifa, uelewa, na uthibitisho ambao utabariki maisha yako na kukuruhusu uwabariki wengine. Fungua akili na moyo wako kupokea misukumo na umaizi unaopokea kutoka Kwake. Jumuisha umaizi huu katika mihutasari yako.

Pitia mara kwa mara shajara yako ya kujifunzia ili kukumbuka uzoefu wa kiroho, kuona utambuzi mpya, na kutambua ukuaji wako.

Aplikesheni ya Hubiri Injili Yangu

Tumia app ya Hubiri Injili Yangu ili ikusaidie utumie kanuni unazojifunza. App hii inapatikana kwenye kifaa chako cha simu ya kiganjani. Ina vipengele vya kukusaidia utimize vyema dhumuni lako la umisionari. Vipengele hivi vinajumuisha:

  • Taarifa kuhusu mahitaji na maendeleo ya watu unaowafundisha.

  • Mahali pa kuandika maendeleo yako kuelekea kwenye malengo muhimu ya kiashirio.

  • Kalenda ya kuandika mipango yako na ratiba ya shughuli.

  • Ramani ya eneo lako na taarifa zingine muhimu za kukusaidia utimize malengo yako.

Hubiri Injili Yangu hujumuisha mawazo mengi ya matumizi ya app ili kukusaidia utafute, ufundishe, na ubatize watu.

Picha
familia ikijifunza maandiko

Matumizi ya Hubiri Injili Yangu kwa Waumini wa Kanisa

Hubiri Injili Yangu ni nyenzo ya thamani siyo tu kwa wamisionari bali pia kwa waumini wote wa Kanisa. Kwa mfano, kujifunza Hubiri Injili Yangu kutawasaidia waumini:

  • Wajifunze na wafundishe injili ya Yesu Kristo (jifunze sura ya 1, 2, 3, na 10).

  • Wajibu maswali kuhusu injili (jifunze sura ya 3 na 5).

  • Waelewe zaidi kuhusu kutafuta na kumtegemea Roho Mtakatifu (jifunze sura ya 4).

  • Waelewe nguvu ya Kitabu cha Mormoni (jifunze sura ya 5).

  • Watafute sifa kama za Kristo (jifunze sura ya 6).

  • Watimize jukumu lao la agano la kushiriki injili kwa kuishi kanuni za kupenda, kushiriki, na kualika (jifunze sura ya 9 na 13).

  • Wajenge umoja na wamisionari wa muda wote (jifunze sura ya 13).

Kujifunza Hubiri Injili Yangu—hususani sura ya 3—kutakuwa na msaada mkubwa hasa kwa wote vijana na watu wazima ambao wanajiandaa kwa huduma ya umisionari.