Vitabu vya Maelekezo na Miito
15. Seminari na Vyuo vya Dini


“15. Seminari na Vyuo vya Dini,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“15. Seminari na Vyuo vya Dini,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
msichana akiinua mkono wake darasani

15.

Seminari na Vyuo vya Dini

15.0

Utangulizi

Seminari na Vyuo vya Dini (S&V) huwasaidia wazazi na viongozi wa Kanisa katika kuwasaidia vijana na vijana wakubwa waongeze imani yao katika Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho.

Mwakilishi wa S&C amepangwa kwa kila kigingi ili kuwasaidia viongozi kusimamia programu za S&C.

15.1

Seminari

Seminari ni programu ya miaka minne ambayo vijana wanajifunza injili ya Yesu Kristo kama inavyopatikana katika maandiko na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho. Wanafunzi wa Seminari kwa kawaida wana umri wa miaka 14–18.

Uaskofu, viongozi wa vijana, na akidi na urais wa madarasa unamhimiza kila kijana ashiriki kikamilifu katika seminari.

15.1.1

Walimu

Walimu wa seminari wanapaswa kuwa waumini wa Kanisa ambao wana imani katika Bwana Yesu Kristo na ushuhuda juu ya injili Yake ya urejesho. Wanapaswa kuishi kanuni wanazozifundisha na kufanya kazi vizuri na vijana. Inapowezekana, walimu wanapaswa kuwa na kibali kilicho hai cha hekaluni.

Mshiriki wa urais wa kigingi au mshiriki wa baraza kuu aliyepangiwa anawaita, kuwasimika, na kuwapumzisha walimu wa seminari wa kigingi na wasimamizi wa kigingi.

Ili kuwalinda walimu na wanafunzi, watu wazima wawili wanapaswa kuwepo katika jengo au nyumba ambapo darasa la seminari linafundishwa.

15.1.2

Chaguzi za Seminari

Seminari inasaidia mno wakati wanafunzi wanapoweza kukutana na mwalimu kila siku ya wiki. Hata hivyo, hii yaweza kuwa isiwezekane kutokana na masuala ya kiusalama, umbali wa kusafiri, na sababu nyinginezo.

Viongozi wa Kanisa wanashauriana na mwakilishi wao wa S&C ili kuamua uchaguzi gani:

  • Utawasaidia vizuri zaidi wanafunzi wajifunze injili na wakue kiroho.

  • Utawaweka salama wanafunzi.

  • Hautawapa mzigo usio wa lazima wanafamilia.

Madarasa hayapaswi kufanyika siku ya Jumapili.

15.1.3

Majengo, Vifaa, na Nyenzo

Viongozi wa kigingi na wa kata wanahakikisha kwamba mahali kama vile nyumba za mikutano au nyumba za waumini zinapatikana kwa ajili ya madarasa ya seminari.

Wawakilishi wa S&C wanatoa nyenzo kwa ajili ya walimu na wanafunzi kwa ajili ya kila darasa. Wanafunzi wanapaswa kuja na maandiko yao wenyewe, yaliyochapishwa au ya kidijitali.

15.1.5

Alama za Ufaulu na Mahafali

Wanafunzi wa seminari wanaweza kujifunza kwa tija zaidi na kuongeza uongofu wao kama watahudhuria madarasa mara kwa mara, kushiriki, na kujifunza maandiko nje ya darasa. Wanapofanya vitu hivi pia wanapata alama nzuri za ufaulu kila mwaka na wanaweza kuhitimu kutoka katika seminari.

Ili kuhitimu kutoka seminari, mwanafunzi lazima apate alama za miaka minne ya ufaulu na kupokea cheti cha uhitimu kilichosainiwa na mshiriki wa uaskofu.

15.2

Chuo

Chuo kinatoa madarasa ya kujifunza injili kila siku ya juma ambayo yanaimarisha imani na ushuhuda katika Kristo na injili Yake ya urejesho. Vijana wote wakubwa waseja umri miaka 18–30 wanapaswa kuhimizwa kuhudhuria madarasa ya chuo, iwe wanahudhuria shule au la.

15.3

Shule za Kanisa na Mfumo wa Elimu wa Kanisa

Kwa ajili ya taarifa juu ya shule za msingi na sekondari za Kanisa, BYU–Pathway Ulimwenguni kote, na vyuo vya elimu ya juu, ona CES.ChurchofJesusChrist.org. Maelezo kuhusu kukamilisha idhinisho la viongozi wa dini kwa ajili ya wanafunzi kuhudhuria shule hizi pia yametolewa hapa.

Kwa nyongeza, maelezo kuhusu ruhusa za ajira za Kanisa kupitia Ofisi ya Ruhusa ya Kanisa ya CES yanaweza kupatikana kwenye help.ChurchofJesusChrist.org.