EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Kiambatisho: Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo


“Kiambatisho: Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

Appendix

Conversation Group Games

Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo

Kilichojumuishwa katika kitabu cha kiada hiki ni michezo ya burudani ili kufanyia mazoezi Kiingereza. Unaweza kucheza michezo hii wakati wa mkutano wowote wa kikundi. Tumia mpangilio na msamiati kutoka katika somo ambalo upo au somo la awali. Mingi ya michezo hii inakuhitaji wewe kufanya kazi na mwenza au kikundi kidogo.

Questions (10–15 minutes)

Maswali (dakika 10–15)

alama za kuuliza tatu

Steps

Hatua

  1. Chagua swali kutoka kwenye orodha. Kumbuka unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno mengine na virai.

  2. Shiriki jibu lako na kikundi.

  3. Chukueni zamu. kuchagua maswali na kushiriki majibu.

Questions to Review Patterns:

Maswali ya Kurejelea Mipangilio:

  • What do you like doing? Why?

  • Tell me about your extended family.

  • How are you and your sister different?

  • Are you happy? Why or why not?

  • Tell me about where you live.

  • What were you like as a child?

  • Tell me about your weekly routine.

  • What did you do yesterday?

  • Where were you yesterday? Why?

  • When did you finish school?

  • What happened when you moved to the United States?

  • Tell me about shopping in your city.

  • Which phone is better?

  • Tell me about your neighborhood.

  • What will you do tomorrow?

  • Tell me about your favorite holiday.

  • Tell me about your plans for the summer.

  • What do you do when you are sick?

  • Tell me about a time when you got hurt. What happened?

  • Tell me about an event next week.

  • Tell me about your last vacation.

  • What are your future plans?

More Questions:

Maswali Zaidi:

  • What’s your favorite thing to do on the weekend?

  • What’s your favorite place to visit?

  • Tell me about your favorite memory from your childhood.

  • Describe your favorite family tradition.

  • Name one great thing about your family.

  • What is something you really want to do in the future?

  • What adjectives best describe you?

  • Where would you like to go on vacation?

  • What is your favorite movie?

  • Tell me about your greatest adventure.

  • Tell me about your favorite food.

  • What is your dream job?

  • Who is your role model? Why?

  • Why do you want to learn English?

  • Tell me about your best friend.

  • What is one of your current goals?

Notes

Mihutasari

  • Unaweza kucheza mchezo huu pamoja na kikundi chote au vikundi vidogo vya watu watatu hadi watano.

  • Hauzuiliwi na maswali zaidi ya yaliyomo kwenye orodha hii. Unaweza kubuni maswali mapya. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mistari ili kubuni maswali zaidi.

  • Kama unataka kufanya mchezo huu kuwa wenye changamoto zaidi, chukueni zamu kushiriki majibu unayokumbuka kutoka kwa kila mshiriki wa kikundi.

  • Unaweza kutumia maswali haya pamoja na michezo mingine kama vile “mnyororo wa Baiskeli” au “Kutupiana Mpira.”

Hot Seat (10–20 minutes)

Kiti cha Moto (dakika 10–20)

Mwanamke ameketi mgongo ukitazama ubaoni

Steps

Hatua

  1. Gawanyika katika timu mbili.

  2. Chagua wanafunzi wawili (mwanafunzi mmoja kutoka kwenye kila timu). Wanafunzi hawa waketi kwa kukitazama kikundi (katika “kiti cha moto”) migongo yao ikitazama ubaoni.

  3. Mwalimu wenu anaandika neno la msamiati au kirai ubaoni. Wanafunzi walio katika “kiti cha moto” hawawezi kuona lile neno.

  4. Timu zinachukua dakika mbili kuwasaidia wenzao wa timu moja walio katika “kiti cha moto” kubahatisha lile neno lililo ubaoni bila kulisema lile neno.

  5. Mtu aliye katika “kiti cha moto” ambaye anasema lile neno kwanza anapata alama moja kwa ajili ya timu yake. Kama timu inasema lile neno lililo ubaoni huku wakijaribu kumsaidia mwanatimu wao kubahatisha, hawapati alama.

  6. Rudia na maneno mapya.

Notes

Mihutasari

  • Unda timu moja hadi tatu kutegemeana na ukubwa wa kikundi.

  • Kama mnafanya mkutano mtandaoni, chezeni mchezo wa kikundi chote badala ya timu. Mtu mmoja anakuwa katika “kiti cha moto.” Mtu huyu hajui lile neno. Mtu mmoja anakuwa “mtoa kidokezo.” Yule “mtoa kidokezo” anachagua neno na kutoa vidokezo ili yule katika “kiti cha moto” aweze kubahatisha lile neno.

Ball Toss (10–15 minutes)

Kutupiana Mpira (dakika 10–15)

msichana akiwa na mpira

Steps

Hatua

  1. Tafuta mpira, kitu laini, au kipande cha karatasi kilichoviringishwa.

  2. Chagua swali. (Tumia swali mojawapo kutoka katika somo au ona “Maswali” katika kiambatisho hiki.)

  3. Uliza swali na umtupie mwanafunzi mpira.

  4. Mwanafunzi anadaka mpira na anajibu lile swali.

  5. Yule mwanafunzi anauliza swali tena na anamtupia mwanafunzi mwingiine mpira.

  6. Rudia mpaka kila mwanafunzi katika kundi lako amejibu swali. Kisha anza tena na swali jipya.

Notes

Muhtasari

  • Ili kufanya mchezo huu kuwa wenye changamoto zaidi, badilisha swali kila mara unapotupa mpira.

  • Kama mnafanya mkutano mtandaoni, ita majina ya wahusika badala ya kutupa mpira.

Give One, Get One (10–20 minutes)

Toa Moja, Pata Moja (dakika 10–20)

Steps

Hatua

  1. Chagua mada kwa ajili ya kikundi (kwa mfano: familia, michezo au chakula).

  2. Andika chini maneno mengi kadiri unavyojua kuhusu mada kwa dakika moja au mbili.

  3. Simama na utembee kuzunguka chumba. Tafuta mwenza.

  4. Shiriki neno lako kutoka kwenye orodha yako na mwenzako. Mwenza wako anashiriki neno na wewe. Kama ni neno jipya, ongeza neno lile kwenye orodha yako.

  5. Tembea kuzunguka chumba tena. Tafuta mwenza mpya. Rudia.

Example

Mada: familia

Mwenza A anaandika:

  • mom

  • dad

  • sister

  • brother

Mwenza B anaandika:

  • grandfather

  • grandmother

  • mother

  • father

  • aunt

  • uncle

A: What’s one word from your list?
B: Grandmother.
A: I don’t have that word. I’ll add it to my list.
B: What’s a word from your list?
A: Mom.
B: I have mother. I will write mom next to mother.

Wanafunzi wote wawili wanaongeza maneno mapya kwenye orodha zao.

Orodha ya Mwenza A:

  • mom

  • dad

  • sister

  • brother

  • grandmother

Orodha ya Mwenza B:

  • grandfather

  • grandmother

  • mother, mom

  • father

  • aunt

  • uncle

Notes

Mihutasari

  • Hii ni njia nzuri ya kujifunza au kufanya mazoezi ya msamiati mpya ambao hauko katika somo.

  • Kama mnafanya mkutano mtandaoni, acha kila mtu ashiriki na kikundi chote neno moja kutoka kwenye orodha zao badala ya kucheza katika jozi.

Speculation—“I think that you …” (15–20 minutes)

Ubahatishaji—“Ninafikiri kwamba wewe …” (dakika 15–20)

wanawake wawili wakicheka

Steps

Hatua

  1. Fikiria kitenzi.

  2. Sema kitenzi kwa sauti.

  3. Ukitumia kitenzi hiki, unda sentensi ya kweli kuhusu mwanafunzi mwingine. Sema, “Nadhani wewe …” ili kuanza sentensi yako.

  4. Mwanafunzi mwingine anasema kama kauli yako ni kweli au la.

  5. Kama ni kweli, unapata alama moja. Kama si kweli, haupati alama.

  6. Mwanafunzi wa kwanza ambaye anafikisha alama 5 anashinda!

  7. Kamilisha raundi 10 hadi 20. Badilisha kitenzi kila mzunguko.

Example

Mwanafunzi A (kwa mwanafunzi B): The verb is like. I think that you like chocolate.

Mwanafunzi B: That’s true! (Mwanafunzi A anapata alama.)

Mwanafunzi B (kwa mwanafunzi C): I think that you like to play basketball.

Mwanafunzi C: That’s not true! (Mwanafunzi B hapati alama.)

Notes

Mihutasari

  • Unda vikundi vya watu watatu hadi watano.

  • Mchezo huu utajumuisha raundi 10 hadi 20. Utahitaji kuwa na kitenzi kwa kila raundi. Chukueni zamu kusema kitenzi kipya kila wakati raundi inapoanza.

Tell Me a Story! (5–15 minutes)

Simulia hadithi!

Steps

Hatua

  1. Fanya kazi na mwenza au kikundi kidogo.

  2. Mtu mmoja anasema sentinsi ya kwanza ya hadithi ya kutunga.

  3. Kisha mtu mwingine anasemma sentensi ya pili.

  4. Kila mtu anachukua zamu kusema sentensi moja ya hadithi mpaka hadithi imalizike.

Example

A: Yesterday, Sara and Mari missed the bus to come to conversation group.
B: They waited for the next bus, but it didn’t come.
C: They started to walk to the church.
A: Luke was driving to conversation group and saw them walking.
B: He stopped so they could go with him.
C: Sara, Mari, and Luke arrived 20 minutes late.
A: Luke was happy to help Sara and Mari.
B: He said it was a blessing in disguise that he was late.
C: They all had a fun time.

Notes

Mihutasari

  • Unda vikundi vya watu watatu hadi watano.

  • Unaweza kufanya shughuli hii kuwa rahisi zaidi kwa kuonyesha picha ili kuanza hadithi hiyo.

  • Njia nyingine ya kufanya hadithi kuwa rahisi zaidi ni kufanya kila kikundi kuanza na sentensi hiyo hiyo. Kwa mfano, kila kikundi kingeweza kuanza na “nilikuwa na wiki ngumu sana” au “Ilikuwa siku nzuri sana ya maisha yangu.”

Two Truths and One Lie (10–15 minutes)

Kweli Mbili au Uongo Mmoja (dakika 10–15)

Steps

Hatua

  1. Fikiria mambo mawili ambayo ni ya kweli kukuhusu wewe. Buni kimoja ambacho si kweli. Jaribu kutumia msamiati na virai kutoka kwenye somo.

  2. Soma maelezo yako kwa sauti kwa mwenzako au kikundi kidogo cha watu watatu hadi watano.

  3. Washiriki wa kikundi chako wanakuuliza maswali ili kubahatisha ni kauli ipi ambayo si kweli. Jibu maswali yao.

Example

Mshiriki wa 1 wa Kikundi: “I like pizza. I like French fries. I like chocolate. Which is not true?

Washiriki wengine wa kikundi wanauliza maswali:

Q: What is your favorite kind of pizza?
A: I like cheese pizza.
Q: What is your favorite candy bar?
A: I like chocolate and caramel.
Q: Where do you like to get French fries?
A: I don’t have a favorite place.

Washiriki wengine wa kikundi wanabahatisha: “I think you don’t like French fries.

Mshiriki 1 wa Kikundi: “That’s right! I don’t like French fries.

Vocabulary Cards (10–15 minutes)

Kadi za Msamiati (dakika 10–15)

mtu akisikiliza

Steps

Hatua

  1. Andika maneno 5 hadi 10 ya msamiati kwenye vipande vidogo vya karatasi (vipande vyenye gundi ni bora). Weka vipande hivyo vya karatasi katika rundo.

  2. Tafuta mwenza.

  3. Gueza rundo la maneno juu chini ili wewe usione maneno yale. Badilishana marundo na mwenzako.

  4. Chagua karatasi. Usiangalie lile neno. Shikilia karatasi ile kwenye paji lako la uso. Mwenza wako anaelezea neno lile (au anatoa tafsiri), ili kwamba wewe uweze kubahatisha lile neno lililo kwenye karatasi. Kama ukibahatisha vizuri, unapata alama moja.

  5. Chukueni zamu. Rudia kwa kila karatasi kwenye rundo lako.

Notes

Muhtasari

  • Hii ni njia nzuri ya kufanyia mazoezi msamiati.

  • Kama mnafanya mkutano mtandaoni, chezeni mchezo wa kikundi chote badala ya jozi. Kila mtu anaandika orodha ya maneno. Usionyeshe orodha yako kwa kikundi. Chukueni zamu kuchagua neno moja kutoka kwenye orodha zenu. Lielezee kwa kikundi bila kusema neno lile. Washiriki wa kikundi wanabahatisha lile neno.

Dice Game 2 (10–15 minutes)

Mchezo wa Kete 2 (dakika 10–15)

Steps

Hatua

dadu mbili
  1. Unahitaji kete mbili (au kadi ya namba iliyo na namba 1-6).

  2. Chagua vitenzi sita na uviandike kwenye ubao namba 1 -6.

  3. Chagua maneno mengine, viwakilishi, au njeo na uviandike kwenye ubao namba 1 hadi 6.

  4. Fanya kazi na mwenza au kikundi kidogo cha watu watatu hadi watano. Bilingisha kete. Tumia namba zote mbili unabingirisha ili kuunda sentensi pamoja na maneno yanayoshabihiana Chukueni zamu.

Example

Mwalimu anaandika vitenzi na njeo zifutazo ubaoni:

Vitenzi

  1. eat

  2. play

  3. talk

  4. laugh

  5. go

  6. buy

Njeo

  • 1, 3, 5 = past tense

  • 2, 4, 6 = present tense

Mwanafunzi wa 1 anabingirisha dadu na anapata namba 6 na 3. Anaunda sentesni akitumia nunua + njeo iliyopita.

  • I bought rice and chicken at the store last night.

Mwanafunzi wa 2 anabingirisha dadu na anapata namba 6. Anaunda sentensi akitumia cheka + njeo iliyopo.

  • I always laugh at my dog. He’s so silly

Mwanafunzi wa 3 anabingirisha kete na anapata namba 1 na 5. Anaunda sentensi akitumia kula + njeo iliyopita.

  • I ate pizza for lunch.

Notes

Muhtasari

  • Hii ni njia nzuri ya kufanyia mazoezi njeo (iliyopita, iliyopo, ijayo) au muundo mwingine wa sarufi (ukitumia kabla na baada, maswali, kauli hasi, na kadhalika).

  • Kama mnafanya mkutano mtandaoni, chezeni mchezo na kikundi chote. Tumia dadu za mtandaoni na mchukue zamu kuunda sentensi.

Bicycle Chain (in person) (10–20 minutes)

Mnyororo wa Baiskeli (ana kwa ana) (dakika 10–20)

Hii shughuli hufanya vyema tu kwa makundi yanayokutana ana kwa ana.

Steps

Hatua

  1. Chagua swali. (Tumia mojawapo ya swali kutoka kwenye somo au ona “Maswali” katika kiambatisho hiki.)

  2. Jipangeni katika mistari miwili ambayo mtatazamana uso kwa uso.

    mchoro wa safu mbili ya watu wanao tazamana.
  3. Watu wanaotazamana wao ni wenza.

  4. Wenza wanauliza na kujibu swali.

    mchoro wa safu mbili za watu ambapo wanatembea kwenda kwenye sehemu ya mtu aliye kulia kwao.
  5. Wanatembea katika duara ili kila mtu awe na mwenza mpya.

    mchoro ukionyesha safu mbili za watu wakiwatazama watu wapya tofauti na wale walioanza nao.
  6. Wenza wanauliza na kujibu swali.

  7. Rudia hatua ya 5 na 6.

Notes

Mihutasari

  • Kama una watu wa namba witiri, unda kikundi kimoja cha watu watatu.

Mingle and Share (in person) (10–15 minutes)

Changamana na Shiriki (ana kwa ana) (dakika 10–15)

Hii shughuli hufanya vyema tu kwa makundi yanayokutana ana kwa ana.

watu wawili wakizungumza

Steps

Hatua

  1. Chagua swali. (Tumia mojawapo kutoka kwenye somo au ona “Maswali” katika kiambatisho hiki.)

  2. Simama na utafute mwenza.

  3. Muulize mwenza wako swali. Kumbuka jibu la mwenza wako. Jibu swali la mwenza wako.

  4. Tembea chumbani na utafute mwenza mpya. Uliza maswali na ujibu maswali. Rudia mara kadhaa na wenza wapya. Kumbuka majibu ya wenza wako wote.

  5. Rudi kwenye kiti chako. Shiriki pamoja na kundi lako kile ulichojifunza.

Example

Question: What do you like to do?

Wanafunzi wanatembea wakiuliza na kujibu swali wakiwa na wenza tofauti.

  • Sara: What do you like to do?

    Mei: I like to dance. What do you like to do?

    Sara: I like to go to karaoke.

    Mei: What’s your favorite song to sing?

    Sara: I don’t have a favorite song. I really like to sing with other people.

    Mei: What do you like to do?

    Lee: I like to play video games. What do you like to do?

    Mei: I like to dance. What is your favorite game?

    Lee: I like strategy games.

Shiriki pamoja na kundi lako kile ulichojifunza.

  • Teacher: What does Mei like to do?

    Sara: She likes to dance.

    Teacher: What does Lee like to do?

    Mei: He likes to play video games.