EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 20: Afya na Ugonjwa


“Somo la 20: Afya na Ugonjwa,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 20,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

kijana akitabasamu pembeni ya mto

Lesson 20

Health and Sickness

Shabaha: Nitajifunza kuelezea afya ya mtu na nitaomba na kutoa ushauri.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Love and Teach One Another

Pendaneni na Fundishaneni

I can learn by the Spirit as I love, teach, and learn with others.

Ninaweza kujifunza kutoka kwa Roho ninapowapenda, kuwafundisha, na kujifunza pamoja na wengine.

Wewe ni Mtoto wa Mungu. Yeye anataka kukusaidia ukue na uendelee. Yeye anataka kukusaidia ukuze uwezo mpya na ujifunze mambo mengi mazuri. Njia mojawapo muhimu ya kujifunza ni kumfundisha mtu mwingine. Wakati unapomfundisha mtu mwingine, uelewa wako mwenyewe unaweza kukua. Mungu alikupa ahadi ya ajabu.

“Na ninatoa kwenu amri ya kuwa mfundishane mafundisho ya ufalme.

“Fundishaneni kwa bidii na neema yangu itakuwa pamoja nanyi, ili mpate kuelekezwa kiukamilifu zaidi, …

“Ili mpate kuandaliwa katika mambo yote” (Mafundisho na Maagano 88:77–78, 80).

Wakati tunapofundishana na kutumikiana, tunamwalika Roho kuwa pamoja nasi. Roho anaweza kutusaidia tuelewe vyema na kujifunza haraka. Kuwafundisha wengine ni njia mojawapo ambayo Mungu huongeza uwezo wetu wa kujifunza. Wakati mwingine tunaogopa kuwafundisha wengine. Wakati mwingine hatufikirii kuwa tuna chochote cha kutoa. Lakini Mungu anajua kwamba wewe una mengi sana mazuri ya kushiriki na wengine. Wakati tunashiriki kitu tunachojifunza, ni kwamba sisi tunafundishana. Unapowafundisha wengine na kushiriki uzoefu wako, Roho atakusaidia wewe kujifunza hata zaidi.

watu watatu wakitabasamu katika darasa la Kiingereza

Ponder

  • Je, ni kwa jinsi gani kumfundisha mtu mwingine kunakusaidia wewe kuongeza kujifunza kwako?

  • Ni baadhi ya njia gani ambazo unaweza kusaidia kuwafundisha na kuwainua wale walio katika kikundi chako za EnglishConnect?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno kutoka kwenye sehemu ya “Memorize Vocabulary” katika mazoezi yako ya kila siku.

feel/feeling

hisi/kuhisi

You should …

Unapaswa …

You shouldn’t …

Haupaswi

Adjectives

anxious

shauku

dizzy

kizunguzungu

sick

mgonjwa

tired

choka

Nouns

cold

mafua

cough

kikohozi

fever

homa

flu

mafua makali

headache

maumivu ya kichwa

sore throat

maumivu ya koo

stomachache

maumivu ya tumbo

Verbs

drink water

kunywa maji

exercise

zoezi

go home

nenda nyumbani

go to the doctor

Nenda kwa daktari

put ice on it

weka barafu juu yake

rest

pumziko

take some medicine

kunywa dawa

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: How are you feeling?A: I feel (adjective). I have a (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 1 hujambo

Answers

jibu la mpangilio wa 1 mimi nina hisi kivumishi

Examples

mwanamke mgonjwa kitandani

Q: How are you feeling?A: I feel sick.

mwanamke akihisi kizunguzungu

Q: How is she feeling?A: She feels dizzy.

mwanamke mwenye homa

Q: How are you feeling?A: I have a fever.

Q: How is he feeling?A: He has the flu.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kufanya shughuli ya 1 na ya 2 za kikundi cha mazungumzo kabla ya kikundi chako kukutana.

Q: What should I do?A: You should (verb).

Questions

swali la mpangilio wa 2 nitafanya nini

Answers

jibu la mpangilio wa 2 unapaswa kitenzi

Examples

daktari akiongea na mgonjwa

Q: What should I do?A: You should go to the doctor.

Q: What shouldn’t she do?A: She shouldn’t exercise.

mwanaume amelala kitandani

Q: What should he do?A: He should go home and rest.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Love and Teach One Another

(20–30 minutes)

watu watatu wakitabasamu katika darasa la Kiingereza

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2.

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.

New Vocabulary

exhausted

amechoka

go to work

nenda kazini

stuffy nose

mafua

Example: Andrea

“I have a fever.”

mwanamke ana homa
  • A: How is she feeling?

  • B: She has a fever.

  • A: What should Andrea do?

  • B: She should take some medicine.

  • A: What shouldn’t Andrea do?

  • B: She shouldn’t go to work.

Image 1: Tasha

“I feel sick. I have a stuffy nose.”

mwanamke mgonjwa amelala kitandani

Image 2: Becca

“I feel exhausted.”

mwanamke anapumzika juu ya dawati

Image 3: Ramesh

“I have a headache.”

mwanamume ameshikilia kichwa kilicho jeruhiwa

Image 4: Jean

“I have a stomachache.”

mtu ameshika tumbo linalouma

Image 5: Lupe

“I feel tired. I don’t want to eat.”

mwanamke amkikodolea macho chakula kwenye sahani

Image 6: Marcus

“I feel anxious. I’m worried about work.”

Mwanamume anasikia maumivu kifuani

ikoni 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Fanya Igizo. Mwenza B ana tatizo la afya. Mwenza A anauliza maswali na anatoa ushauri. Toa ushauri mzuri na ushauri mbaya. Badilishaneni nafasi.

New Vocabulary

Do you have a fever?

Je, una homa?

I think I ate some bad food.

Nadhani nilikula chakula kibaya.

Example

  • A: How are you feeling?

  • B: I feel very sick.

  • A: Do you have a fever?

  • B: Yes, and I also have a headache.

  • A: Do you have a stomachache?

  • B: Yes, I have a stomachache. I think I ate some bad food. What should I do?

  • A: OK. You shouldn’t go to work today. You should go to bed and rest. You shouldn’t eat a lot. You should drink a lot of water.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Ask how others are feeling.

    Uliza wengine wanajisikiaje.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Talk about how I and others are feeling.

    Zungumza kuhusu mimi na wengine tunajisikiaje.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Ask for health advice.

    Omba ushauri wa kiafya.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Give health advice.

    Toa ushauri wa kiafya.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri Msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Kuweka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Kama tunafundisha na kujifunza kwa njia ya Bwana aliyoelekeza, yeye atamtuma Roho Wake kutujenga na kutuelimisha tunapofanya hivyo” (Dallin H. Oaks, “Kufundisha na Kujifunza kwa Roho,” Ensign, Machi 1997, 6).