EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 19: Kwenda Likizo


“Somo la 19: Kwenda Likizo,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 19,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

familia ikitabasamu

Lesson 19

Going on Vacation

Lengo: Nitajfunza kusimulia kuhusu mipango ya wakati wa likizo.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

Tumia imani katika Yesu Kristo.

Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.

Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoonyesha imani Kwake.

Siku moja, Yesu Kristo alikuwa akifundisha maefu ya watu jangwani. Yesu na wanafunzi Wake walikuwa na wasi wasi kwa sababu watu hawakuleta chakula chochote. Mvulana mmoja katika kundi alitoa mikate mitano na samaki wawili. Watu wengi walishangaa jinsi mikate mitano na samaki wawili vingeweza kuwalisha wale watu wote. Lakini Yesu alimshukuru Mungu kwa ajili ya chakula kile, alikibariki, akakigawa katika vikapu na kuwatuma wanafunzi wakagawe. Biblia inasema:

“Wakala wote wakashiba; na … [kukawa kumebakia] vikapu kumi na viwili, vimejaa” (Mathayo 14:20).

Kila mtu alikula, na kukawa na chakula zaidi. ulikuwa ni muujiza. Vivyo hivyo, wewe unaweza kuhisi huna muda wa kutosha kujifunza Kiingereza. Fuata mfano wa Yesu katika hadithi hii. Mshukuru Mungu kwa ajili ya muda na nguvu ulizo nazo na muombe Yeye azibariki. Kama utatoa kile ulichonacho kwa imani, Mungu anaweza kuongeza uwezo wako. Hata kama una wakati mdogo tu, pengine unaweza kujifunza mipangilio michache au kujaribu kutumia maneno machache mapya kila siku. Mungu anaweza kuzifanya juhudi zako ziwe na mafanikio zaidi. Kuwa na imani katika Yesu Kristo na kufuata mfano Wake kunaweza kukusaidia wewe kufanya mengi zaidi kuliko unavyofikiria inawezakana.

Kristo akiwalisha makutano

Ponder

  • Ni kwa jinsi gani Mungu anaweza kukusaidia wewe kujifunza Kiingereza?

  • Fikiria wakati ambapo Mungu alikusaidia wewe kufanya zaidi kuliko vile ulivyofikiri ilikuwa inawezekana. Je, ulifanya nini? Je, Yeye alifanya nini?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo.

How are you going to get there?

Je, utafikaje huko?

What are you going to do?

Je, utakwenda kufanya nini?

When are you going?

Je, ni lini unakwenda?”

Where are you going?

Je, unakwenda wapi?”

I am going …/I’m going …

Mimi ninakwenda …/ninakwenda …

vacation

likizo

Nouns 1

beach

ufukweni

mountains

milima

Nouns 2

boat

boti

bus

basi

car

gari

plane

ndege

train

treni

Verbs

explore the city

talii jijini

fish

samaki

go to the zoo

nenda bustani ya wanyama

relax

pumzika

visit museums

tembelea makumbusho

Time

in July

Katika mwezi Julai

on August 5th

mwezi Agosti 5

at 9:00 a.m.

saa 3:00 asubuhi

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: Where are you going on vacation?A: I’m going to the (noun 1).

Questions

swali la mpangilio wa 1 unaenda wapi wakati wa likizo

Answers

jibu la mpangilio wa 1 ninaenda nomino 1

Examples

mandhari ya milima na ziwa

Q: Where are you going on vacation?A: I’m going to the mountains.

Q: When are you going on vacation?A: We’re going in July.

Q: When are you going on vacation?A: I’m going on September 12th.

Treni ya reli nyepesi

Q: How are you going to get there?A: We’re going by train.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kujifunza zaidi kuhusu mipangilio katika somo hili. Fikiria kutumia vitabu vya sarufi au tovuti.

Q: What will you do?A: We will (verb).

Questions

swali la mpangilio wa 2 wewe utafanya nini

Answers

jibu la mpangilio wa 2 uta kitenzi

Examples

Q: What will you do?A: We will relax.

Q: What are you going to do?A: I will visit museums.

mwanamume akivua samaki wakati wa machweo ya jua

Q: What will you do?A: We are going to fish.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

(20–30 minutes)

Kristo akiwalisha makutano

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2.

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Fanya Igizo. Wewe unaenda mapumziko ya wikiendi kwenye eneo lililoko katika kila picha. Mwenzako anauliza maswali kuhusu mahali unakokwenda, jinsi utakavyo fika huko, na utafanya nini huko. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

New Vocabulary

amusement park

bustani ya burudani

city

jiji

historic site

eneo la Kihistoria

lake

ziwa

Example: amusement park

bustani ya burudani
  • A: Where are you going on vacation?

  • B: I’m going to the amusement park.

  • A: When are you going?

  • B: I’m going to the amusement park in February.

  • A: How are you going to get there?

  • B: I am going by bus.

  • A: What will you do?

  • B: I will relax and play games.

Image 1: beach

familia ufukweni

Image 2: city

jiji kubwa

Image 3: historic site

eneo la kihistoria

Image 4: lake

mandhari ya milima na ziwa

Image 5: mountains

milima na theluji

ikoni 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Fanya Igizo. Mwenza B anakwenda likizo. Mwenza A anauliza maswali kuhusu likizo. Mwenza B anajibu. Sema mengi kadiri uwezavyo. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

New Vocabulary

swim

ogelea

Example

  • A: Where are you going?

  • B: I’m going to the lake.

  • A: When are you going?

  • B: I’m going in October.

  • A: Great! How will you get there?

  • B: I’m going by train.

  • A: What will you do?

  • B: On Friday night, I will relax. On Saturday, I will swim and explore the lake.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Ask about others’ vacations.

    Uliza kuhusu likizo za wengine.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Talk about what I will do on vacation.

    Zungumza kuhusu nitafanya nini kwenye likizo.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri Msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Kuweka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Kweli, imani ni nguvu ambayo inawezesha uwezekano wa kutimiza yasiyowezekana. Usidunishe imani uliyo nayo tayari” (Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 104).