Mkutano Mkuu
Ripoti ya Idara ya Ukaguzi wa Hesabu za Kanisa, 2022
Mkutano mkuu wa Aprili 2023


Ripoti ya Idara ya Ukaguzi wa Hesabu za Kanisa, 2022

Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Ndugu Wapendwa: Tukiongozwa na ufunuo, kama ilivyorekodiwa katika sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Mpangilio wa Zaka—linalojumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Kiongozi—huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Mashirika ya Kanisa hugawa fedha kwa mujibu wa bajeti, sera, na taratibu zilizoidhinishwa.

Idara ya Ukaguzi wa Hesabu za Kanisa, inayojumuisha wataalamu walioidhinishwa na isiyofungamana na idara zingine zote za Kanisa, ina wajibu wa kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na ulinzi wa mali za Kanisa.

Kwa kuzingatia ukaguzi uliofanywa, Idara ya Ukaguzi wa Hesabu za Kanisa inatoa msimamo kwamba, katika nyanja zote, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na mali za Kanisa kwa mwaka 2022 vimerekodiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa bajeti ya Kanisa, sera, na utendaji wa kiuhasibu ulioidhinishwa. Kanisa linafuata utaratibu uliofundishwa kwa waumini wake wa kuishi ndani mipaka ya bajeti, kuepuka madeni, na kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa uhitaji.

Kwa heshima imewasilishwa,

Idara ya Ukaguzi wa Hesabu za Kanisa

Jared B. Larson

Mkurugenzi Mkuu