Mkutano Mkuu
Wito Uliotukuka Zaidi
Mkutano mkuu wa Aprili 2020


Wito Uliotukuka Zaidi

Kama wanawake wa imani, tunaweza kupata kanuni za kweli kutoka kwenye uzoefu wa Nabii Joseph ambao unatoa utambuzi wa kupokea ufunuo wetu wenyewe.

Ninashukuru kuelekeza mazungumzo yangu leo kwenye majukumu endelevu ya akina mama katika Urejesho. Ni wazi kwamba kote katika historia wanawake wamebeba nafasi ya kipekee katika mpango wa Baba yetu wa Mbinguni. Rais Russell M. Nelson alifundisha, “Itakuwa vigumu kupima ushawishi ambao … wanawake wanao, sio tu kwa familia lakini pia katika Kanisa la Bwana, kama wake, akina mama, na akina bibi; kama akina dada na mashangazi; kama walimu na viongozi; na hususani kama mifano na walinzi wa dhati wa imani.” 1

Mwanzo wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama huko Nauvoo, miaka 178 iliyopita, Nabii Joseph Smith aliwashauri akina dada “kuishi [kulingana] na fursa zao.” 2 Mfano wao unatufundisha sisi leo. Kwa umoja walifuata sauti ya Nabii na kuishi kwa imani thabiti katika Yesu Kristo pale waliposaida kujenga msingi ambao juu yake tunasimama leo. Akina Dada, ni zamu yetu. Tuna wajibu uliotukuka kutoka kwa Bwana, na michango yetu ya uaminifu, ya kipekee ni muhimu.

Rais Spencer W. Kimball alieleza: “Kuwa mwanamke mwaminifu katika matukio ya mwisho wa dunia hii, kabla ya kuja mara ya pili kwa Mwokozi wetu, ni wito wa juu zaidi. Nguvu na ushawishi wa mwanamke mwaminifu leo inaweza kuwa mara kumi katika kile kinachoweza kuwa nyakati za utulivu.” 3

Rais Nelson vilevile aliongeza: “Ninawasihi dada zangu [wa] Kanisa … kujitokeza mbele! Chukueni nafasi yenu sahihi na inayohitajika katika nyumba zenu, katika jumuia zenu, na katika ufalme wa Mungu—zaidi ya ambavyo mmewahi kufanya hapo awali.” 4

Hivi karibuni, nilibahatika, sambamba na kundi la watoto wa msingi, kukutana na Rais Russell M. Nelson katika eneo la nyumba ya familia ya Smith huko Palmyra, New York. Sikiliza wakati nabii wetu mpendwa anapofundisha watoto kile wanachoweza kufanya kujitokeza mbele.

Dada Jones: “Ninatamani kujua ikiwa mnaweza kuwa na swali ambalo mngependa kumuuliza Rais Nelson. Mmekaa hapa pamoja na nabii. Kuna chochote ambacho mara zote umetaka kumwuliza nabii? Ndiyo, Pearl.”

Pearl: “Je ni vigumu kuwa nabii? Je, unakuwa na kazi nyingi?”

Rais Nelson: “Kwa kweli ni vigumu. Kila kitu kinachohusiana na kuwa kama Mwokozi ni kigumu. Kwa mfano, wakati Mungu alipotaka kumpa Musa Amri Kumi, alimwambia Musa aende wapi? Juu kwenye kilele cha mlima, kwenye kilele cha Mlima Sinai. Kwa hivyo Musa alilazimika kutembea hadi juu ya kilele cha mlima huo ili kupata Amri Kumi. Sasa, Baba wa Mbingu angeweza kusema, ‘Musa, anzia hapo, na Mimi nitaanzia hapa, na Nitakutana nawe katikati.’ Hapana, Bwana anapenda bidii, kwa sababu bidii huleta tuzo ambazo haziwezi kuja bila hiyo. Kwa mfano, je, mmewahi kuchukua masomo ya piano?”

Watoto: “Ndiyo.”

Pearl: “nachukua somo la fidla.”

Rais Nelson: “Na je, mnafanya mazoezi?”

Watoto: “Ndiyo.”

Rais Nelson: “Nini kinatokea kama hufanyi mazoezi?”

Pearl: “Unasahau.”

Rais Nelson: “Ndio, huna maendeleo, sivyo? Kwa hivyo jibu ni ndio, Pearl. Inahitaji bidii, kazi kubwa sana, kujifunza kwingi, na hakuna mwisho. Hiyo ni nzuri! Hiyo ni nzuri, kwa sababu tunaendelea kusonga kila wakati. Hata katika maisha yajayo tunafanya maendeleo.

Majibu ya Rais Nelson kwa watoto hawa wazuri yanakuja hata kwetu sisi. Bwana anapenda bidii, na bidii huleta tuzo. Tunaendelea kufanya mazoezi. Tunaendelea daima kadiri tunavyojitahidi kumfuata Bwana. 5 Yeye hatarajii ukamilifu leo. Tunaendelea kupanda Mlima wetu binafsi wa Sinai. Kama nyakati zilizopita, safari yetu hakika inahitaji bidii, kazi kubwa sana, na kujifunza, lakini nia yetu thabiti ya kuendelea huleta tuzo za milele. 6

Nini zaidi tunajifunza kutoka kwa Nabii Joseph Smith na Ono la Kwanza kuhusu bidii, kazi kubwa sana, na kujifunza? Ono la Kwanza linatupa maelekezo katika majukumu yetu ya kipekee na endelevu. Kama wanawake wa imani, tunaweza kupata kanuni za kweli kutoka kwenye uzoefu wa Nabii Joseph ambao unatoa utambuzi wa kupokea ufunuo wetu wenyewe. Kwa mfano:

  • Tunafanya kazi kwa shida.

  • Tunageukia maandiko kupokea hekima ya kutenda.

  • Tunaonesha imani yetu na tumaini katika Mungu.

  • Tunaweka nguvu zetu kumwomba Mungu kutusaidia kushinda ushawishi wa majaribu.

  • Tunatoa haja za mioyo yetu kwa Mungu.

  • Tunafokasi kwenye nuru Yake kuongoza chaguzi zetu za maisha na kuwa juu yetu wakati tunapomgeukia Yeye.

  • Tunatambua Anatujua kila mmoja wetu kwa jina na ana jukumu kwa kila mmoja wetu kukamilisha. 7

Kwa nyongeza, Joseph Smith alirejesha ufahamu kwamba tuna uwezekano wa kiungu na thamani ya milele. Kwa sababu ya uhusiano huo na Baba yetu wa Mbinguni, naamini Yeye anategemea sisi tupokee ufunuo kutoka Kwake.

Bwana alimuagiza Emma Smith “kupokea Roho Mtakatifu,” kujifunza mengi, “kuweka kando mambo ya ulimwengu huu, … kuyatafuta mambo ya ulimwengu ulio bora,” na “kuyashikilia maagano [yake]” na Mungu. 8 Kujifunza kumeungana na kuendelea, hasa wakati wenza wa kudumu wa Roho Mtakatifu hutufundisha kile kilicho muhimu kwa kila mmoja wetu kuweka mbali mbali—ikiwa na maana kwamba kile ambacho kingeweza kutuzuia sisi au kuchelewesha kuendelea kwetu.

Rais Nelson alisema, “Ninawasihi muongeze uwezo wenu wa kiroho wa kupokea ufunuo.” 9 Maneno ya nabii wetu daima yako nami wakati ninapotafakari uwezo wa wanawake wa kujitokeza mbele. Anatusihi sisi, ambacho kinaashiria kipaumbele. Anatufundisha namna ya kunusurika kiroho katika dunia iliyojaa dhambi kwa kupokea na kufuata ufunuo. 10 Tunapofanya hivyo, kuheshimu na kuishi amri za Bwana, tunaahidiwa, kama vile Emma Smith alivyoahidiwa, “taji la haki.” 11 Nabii Joseph alifundisha juu ya umuhimu wa kujua kuwa njia tunayofuata katika maisha haya imethibitishwa na Mungu. Bila ya ufahamu huo, “tutachoka katika akili [zetu] na kukata tamaa.” 12

Katika mkutano huu, tutasikia kweli zinazotupa sisi msukumo wa kubadilika, kuwa bora, na kutakasa maisha yetu. Kupitia ufunuo binafisi, tunaweza kuzuia kile ambacho wengine hukiita “kuchoshwa na mkutano mkuu”—tunapoondoka tukiwa tumeazimia kuyatekeleza yote sasa. Wanawake huvaa kofia nyingi, lakini haiwezekani, na si muhimu, kuzivaa zote kwa wakati mmoja. Roho hutusaidia sisi kuamua ni majukumu yapi tuyape fokasi kwa leo. 13

Ushawishi wa upendo wa Bwana kupitia Roho Mtakatifu hutusaidia kujua kipaumbele Chake kwa ajili ya maendeleo yetu. Utii wa ufunuo binafisi huelekeza kwenye maendeleo binafisi. 14 Tunasikiliza na kutenda. 15 Bwana alisema, “Mwombe Baba katika jina langu katika imani, ukiamini kwamba utapokea, na utapata Roho Mtakatifu, ambaye hudhihirisha mambo yote yaliyo muhimu.” 16 Jukumu letu endelevu ni kupokea ufunuo unaoendelea.

Kadiri tunavyopata ujuzi mkubwa wa kufanya hivyo, tunaweza kupata nguvu zaidi katika majukumu yetu binafisi ya kuhudumu na kutimiza kazi ya wokovu na kuinuliwa—kwa uhakika “kuweka kando mambo ya ulimwengu huu, na kuyatafuta mambo ya ulimwengu ulio bora.” 17 Tunaweza kisha vizuri zaidi kuhamasisha kizazi chetu kinachoinukia kufanya vivyo hivyo.

Akina kaka na akina dada, sote tunatafuta nguvu za Mungu katika maisha yetu. 18 Kuna umoja wa kupendeza kati ya akina mama na akina baba katika kukamilisha kazi ya Bwana leo. Tunapata nguvu za ukuhani kupitia maagano, yaliyofanywa kwanza katika maji ya ubatizo na kisha ndani ya kuta za hekalu takatifu. 19 Rais Nelson alitufundisha, “Kila mwanamke na kila mwanamume anayefanya maagano na Mungu na kutunza maagano hayo, na anayeshiriki kwa kustahili katika ibada za ukuhani, ana fursa ya moja kwa moja kwenye nguvu za Mungu.” 20

Kukubali kwangu binafsi leo ni kwamba kama mwanamke sikuwahi kutambua, mapema katika maisha yangu, kuwa mimi ninaweza kufikia, kupitia maagano yangu, nguvu ya ukuhani. 21 Akina dada, ninaomba kwamba tutambue na kuthamini nguvu za ukuhani pale tunapokuwa “tukishikamana na maagano [yetu],” 22 kukubali ukweli wa maandiko, na kutii maneno ya manabii wetu walio hai.

Acha tutangaze kwa ujasiri kujitolea kwetu kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, “kwa imani isiyotingishika ndani yake, tukitegemea kabisa ustahili wa yule aliye mkuu kuokoa.” 23 Acha kwa furaha tuendeleze safari hii kuelekea uwezekano wetu wa juu zaidi wa kiroho na tuwasaidie wale walio karibu nasi kufanya vivyo hivyo kupitia upendo, huduma, uongozi, na huruma.

Mzee James E. Talmage kwa upole alitukumbusha sisi, “Shujaa mkuu duniani wa mwanamke na uanamke ni Yesu Kristo.” 24 Katika tathmini ya mwisho ya mwendelezo wa majukumu ya wanawake katika Urejesho, na kwa ajili yetu sote, ni jukumu lipi la juu zaidi? Nashuhudia kwamba ni kumsikiliza Yeye, 25 kumfuata Yeye, 26 kumwamini Yeye, 27 na kuwa mwendelezo wa upendo Wake. 28 Ninajua Anaishi. 29 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.