Watoto na Vijana
Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu


“Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana (2019)

“Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana

Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo waliumba vitu vyote, wanajua vitu vyote, na wameshinda vitu vyote. Na Wanataka uwe kama Wao! Unapofanya maagano na kufuata mpango wa Mungu, unaweza kutumia karama zako za kipekee kukua na kuwatumikia wengine.

Picha
roho wakiwa mbinguni

Ulikuja duniani kutoka mbinguni. Wewe ni sehemu ya familia.

Picha
mtu akibatizwa

Unaweka agano kumfuata Yesu Kristo wakati unapobatizwa na unapopokea sakramenti.

Picha
mtu akithibitishwa

Unapothibitishwa, unapokea kipawa cha Roho Mtakatifu ili akuongoze.

Picha
utawazo kwenye ukuhani

Unaweza kushiriki katika kazi ya Mungu na kuhudumu Kanisani chini ya mamlaka ya funguo za ukuhani.

Picha
watu nje ya kanisa

Unaweza kujifunza na kukua unaposoma, unapoishi, na kushiriki injili.

Picha
watu wakifanya shughuli

Unaweza kupata furaha wakati unapowapenda na kuwahudumia wengine kama Yesu alivyofanya.

Picha
Yesu akiwafundisha watu

Baba wa Mbinguni alimtuma Mwana Wake, Yesu Kristo, kuwa mfano kamili na kufanya iwezekane kwako kutubu na kubadilika.

Picha
watu nje ya hekalu

Hekaluni, unaweza kuhudumu na kufanya maagano ambayo yanawaunganisha watoto wa Mungu milele.