Watoto na Vijana
Mpangilio kwa ajili ya Ukuaji


“Mpangilio kwa ajili ya Ukuaji,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana (2019)

“Mpangilio kwa ajili ya Ukuaji,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana

Mpangilio kwa ajili ya Ukuaji

Kukua ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Ili kukusaidia, Baba wa Mbinguni anakupa mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, maandiko, na manabii walio hai. Utajifunza kutoka kwenye uzoefu wako, hasa wakati unapomtegemea Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Huu ni mpangilio wa kukusaidia kuishi injili katika nyanja zote za maisha yako.

Gundua kile unachohitaji kukifanyia kazi.

Picha
kijana akisali na kuchunguza

Panga jinsi utakavyokitimiza.

Picha
kijana akiwa na ramani

Fanyia kazi mpango wako kwa imani.

Picha
kijana akitoa huduma

Tafakari kuhusu kile ulichojifunza.

Picha
kijana akitafakari

Gundua

Mahitaji Yako, Karama, na Vipaji

Picha
watu wakifanya shughuli

Baba wa Mbinguni amekupa karama, vipaji na uwezo. Anakutaka uvigundue na uvikuze ili uweze kujiboresha wewe, watu wengine, na hata ulimwengu. Unawezaje kuwa bora na kukua?

Jaribu kuuliza maswali kama:

  • Ni nini nahisi nahitaji kujifunza au kubadili katika maisha yangu?

  • Ni vipaji au ujuzi gani ningependa kuwa nao?

  • Ni tabia zipi za kiroho ninahitaji kukuza au kuboresha?

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kuishi maagano niliyofanya wakati nilipobatizwa?

  • Nani naweza kumtumikia?

Baba wa Mbinguni atajibu maswali haya unapomtegemea. Sali. Pekua maandiko na maneno ya manabii walio hai. Soma baraka yako ya baba mkuu, kama unayo. Jifunze kutambua hisia na mawazo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Atakusaidia kujua kile kilicho muhimu zaidi kwa ajili yako hivi sasa. Kama hauna uhakika wa nini cha kufanya, ona ukurasa wa 58–63.

Mpango

Kujiboresha

Picha
watu katika jiji

Mara tu unapoamua kile utakachofanyia kazi, tengeneza mpango wa jinsi utakavyotimiza hilo. Mpango wako unaweza kuwa na hatua na vitendo bayana, au unaweza kujumuisha njia za kukuza tabia au sifa binafsi.

Jaribu kuuliza maswali kama:

  • Kwa nini hili ni muhimu kwangu?

  • Je, hili litanisaidia vipi kuwa zaidi kama Yesu Kristo?

  • Ni kitu gani naweza kufanya ili kutekeleza hili?

  • Je, naweza kuvigawa vitendo hivi katika hatua ndogo ndogo?

  • Mipango gani naweza kufanya hivi sasa ili niweze kushinda changamoto ambazo naweza kukumbana nazo.

Sali kuhusu mpango wako, na zingatia hisia na mawazo unayopata. Unaweza kuomba usaidizi kutoka kwa Roho Mtakatifu, familia yako, na viongozi wako.

Tenda

Kukua katika Imani

Picha
watu wakifanya shughuli

Fuata mpango wako! Tengeneza ukumbusho kukusaidia kuendelea kubaki umefokasi. Unaweza kuandika muhtasari, kutumia saa ya kengele, au kumuomba mtu akusaidie. Wakati mwingine kuufanyia kazi mpango wako inaweza kuwa vigumu. Wakati mwingine hautafaulu. Hiyo ni sawa! Kujifunza kile kinacholeta mafanikio na kisicholeta mafanikio kunakusaidia kukua.

Unapokwama, jaribu kuuliza maswali kama:

  • Ni nini kimeleta mafanikio? Kwa nini?

  • Ni nini hakikuleta mafanikio? Kwa nini?

  • Nini kingine naweza kujaribu?

  • Wapi naweza kupata mawazo zaidi?

  • Je, naweza kuligawa lengo langu katika hatua au vitendo vidogo vidogo?

  • Nawezaje kujifunza kutokana na vikwazo?

Kufaulu katika njia bora huhitaji mazoezi na subira. Waombe familia yako, marafiki, au viongozi wakusaidie. Mwokozi anakufahamu wewe na changamoto unazokabiliana nazo. Anaweza kukusaidia kufanya mambo magumu. Sali kwa ajili ya msaada na mwongozo.

Tafakari

Kuhusu Kile Ulichojifunza

Picha
watu wakipanda ngazi

Tafakari kuhusu malengo na mipango yako wakati unapoifanyia kazi na wakati unapomaliza. Unahisi nini? Umejifunza nini? Kuandika mawazo na hisia zako kunaweza kukusaidia baadae.

Jaribu kuuliza maswali kama:

  • Ni jinsi gani nimekua?

  • Ninawezaje kutumia kile ambacho nimejifunza katika kuwatumikia wengine?

  • Je, vitendo vyangu vimenisaidia kumkaribia Mwokozi?

  • Ninawezaje kuendelea kukua katika sehemu hii?

Wakati unapomaliza kushughulikia lengo au mpango, mshukuru Baba wa Mbinguni na wale waliokusaidia. Tafakari juu ya wajibu wa Mwokozi katika maisha yako unaposhiriki sakramenti. Fikiria na usali kuhusu kile unachoweza kufanyia kazi baada ya hapo.