Watoto na Vijana
Anza!


“Anza!” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana (2019)

“Anza!” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana

Anza!

Picha
watu wakipanda mlima

Jaribu kutumia mpangilio wa Gundua, Panga, Tenda, na Tafakari ili kukusaidia kufuata mfano wa Mwokozi pale unapokua. Fikiria kuweka malengo katika kila moja ya sehemu hizo nne ili kuweka maisha yako kwenye usawa. Unaweza kutumia kurasa zifuatazo kukuongoza. Au unaweza kutumia shajara nyingine au mbinu ya kuweka lengo ambayo inakufaa wewe.

Kumbuka, ukuaji wako ni jukumu lako, lakini hauhitajiki kuushughulikia peke yako. Baba yako wa Mbinguni anataka kukusaidia, na unaweza kuwaomba wazazi wako, viongozi, na marafiki wakupe msaada. Tafuta fursa za kuwasaidia wengine katika ukuaji wao pia. Baba wa Mbinguni anawataka watoto Wake wapendane na kusaidiana.

Gundua

Ni nini unahisi unahitaji kujifunza au kuboresha? Andika hisia na mawazo unapofikiria kuhusu maswali kama haya: Ni jinsi gani naweza kukuza vipaji vyangu? Nini ninapenda kufanya? Ni majukumu gani niliyonayo hivi sasa? Nawezaje kumtambua Roho Mtakatifu? Nani naweza kumtumikia?

Picha
kiroho, kijamii, kiakili, kimwili

Kiroho

Mifano: Andika kwenye shajara, sali kila asubuhi, jifunze maandiko kila siku, itakase siku ya Sabato.

Kijamii

Mifano: Watumikie wengine, epuka kusengenya, kuwa na marafiki wapya

Kiakili

Mifano: Kuza jambo ulipendalo au ujuzi, fanya mazoezi ya kufundisha, jifunze jinsi ya kubajeti

Kimwili

Mifano: Pika na kula chakula bora, fanya mazoezi, safisha au boresha mazingira yako

Mpango

Lengo langu:

Kwa nini hili ni muhimu kwangu?

Je, hili litanisaidia vipi kuwa zaidi kama Yesu Kristo?

Jinsi nitakavyofanya:

Ni hatua gani ndogo au matendo ambayo naweza kufanya ili kufikia lengo langu?

Tarehe/Mara Ngapi

Tarehe/Mara Ngapi

Tarehe/Mara Ngapi

Ni nani anaweza kunisaidia?

Tenda

  • Ninajifunza nini?

  • Ni marekebisho yapi ninahitaji kufanya?

Tafakari

  • Nimejifunza nini?

  • Ni jinsi gani niko karibu na Mwokozi?

  • Ninawezaje kutumia kile ambacho nimejifunza kuwatumikia wengine?

Picha
ikoni, sherehekea

Tarehe ya kukamilisha:

Nitasherehekea ukuaji wangu kwa:

Picha
nembo, Maendeleo ya Watoto na Vijana

Ninafanya nini baada ya hapa?

Rudi kwenye fomu ya Gundua kwa ajili ya mawazo.